



BAO la kipa Richard Kingston wa Ghana ndilo lililozima furaha ya Watanzania waliofika kwenye uwanja mpya Dar es Salaam leo jioni kuishuhudia timu ya taifa, Taifa Stars, ikimenyana na Ghana ambapo matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1.
Kingston, aliyeidakia timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia 2006 Ujerumani, alifunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika saba mpira kumalizikia, kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na nduguye Larea Kingston.
Bao hilo ambalo limetokana na wachezaji wa Taifa Stars kutokuwa makini kwani kipa huyo alifika katika eneo la kupigia adhabu na kuzungumza na Larea kabla ya kwenda kuunganisha kwa kichwa.
Stars ambayo ilionekana kuelewana kwa dakika nyingi za mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki, ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya 34 kupitia kwa nahodha wake Henry Joseph aliyefunga kwa kichwa baada ya kuunasa mpira wa adhabu uliopigwa na Juma Jabu.
Katika mchezo huo, wachezaji wa Stars walionekana kuelewana kipindi cha kwanza ingawa dakika 20 za mwisho baadhi ya wachezaji walionekana kuchoka na kumlazimisha kocha Marcio Maximo kufanya mabadiliko.
Ghana ilishuka dimbani bila wachezaji wake nyota wanaocheza soka la kulipwa isipokuwa Amamoo William anayecheza soka Misri, lakini akiwa benchi.
Taifa Stars: Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Salum Swed, Nadir Haroub, Geofrey Bonny, Mrisho Ngasa, Joseph/Kigi Makasi, Tegete/ Mgosi, Athuman Idd/Shaban Nditi, Nizar Khalfan/Adam King’wande.
Ghana: Richard Kingston, Boye John, Yeboah Godfred, Quartey Jonathan, Issah Gabriel, Apimah Barusso, Larea Kingston, King Osei Gyan/Kumordji Benard, Dickson Christoper, Tiero Kwabena/Ayew Yeboha na Moussa Narry/Kojo Poku.
Mm nashindwa kumuelewa Maximo kwa kumng'ang'ania mtu ambaye kila siku anafanya mambo ya ajabu gorini, leo ilikuwa tupigwe nyingi tuu ila mabeki wetu walikuwa makini, Jamani kwani Amani Simba kaitwa wa nini huko national team kama kupangwa kwenyewe hapangwi, Maximo jaribu kubadilisha gorikipa hapo gorini, ondoa hilo pazia lako hapo gorini, jaribu mapazia mengine bwana! mechi kama ya ilikuwa ya kuwajaribu wachezaji wapya katika kikosi chako, kama huyu Amani simba na wengineo!!! ni hayo tu!
ReplyDeletehongera kwa kurudi hewani kikamili nanihii wa nanihino. Vipi picha za chini hizi, shutter ya camera yako ilikuwa slow slow kidogo mzee? Maana naona winguwingu kidogo
ReplyDeleteAkiwepo Ivo Mapunda golini watanzania tujihesabu tupo pungufu kwa hiyo lazima mabeki wafanye kazi ya ziada sijui kwa nini Maximo hata kulikubali hili, kama magolikipa wengine hawakubali ni afadhali tuwarudishe wa zamani kama Peter Manyika n.k
ReplyDeleteMdau wa 8.43PM,ujumbe wako mzuri lakini lafudhi yako haifai kusomwa
ReplyDelete