April 1, 2006: JK akiwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar Mh. Amani Abeid Karume, Spika wa Bunge Mh. Samwel Sitta, na wabunge siku alipokwenda kuhutubia bunge mara ya kwanza kama Rais. Kesho JK anatarajiwa kulihutubia Bunge hilo kwa mara ya pili na tayari kila mtu anajiuliza ataongea nini, ikizingatiwa kuna maswala nyeti kadhaa ambayo yanasubiri kauli yake. Atahutubia bunge takriban siku tatu baada ya kupokea ripoti ya EPA na pia huku kukiwa na marumbano kibao juu ya Zanzibar kuwa nchi au la. Wadau mnasemaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kutokana na hali inavyoonekana katika vyombo vya habari ,blogs na hisia za wananchi nashauri kuwa:

    Hotuba hiyo inabidi iwe ya kihistoria na nzito isiyojaa vichekesho ndani.Ibebe ujumbe mzito na wa kihistoria . Uso wake wakati anahutubia aonyeshe seriousness ya hali ya juu kuanzia mwanzo hadi mwisho wa hotuba.

    Waandika hotuba wajihadhari wasimwandikie tu hotuba iliyojaa taarifa za kitalii na mambo ya kitalii yanayolenga kulipa bunge taarifa za safari za Raisi Kikwete huko nje ya Nchi na manufaa kwa nchi.Kwa kuangalia hisia za watu watu wamechoka hawataki kusikia habari za taarifa hizo za safari za nje hata kama ni za maana hasa kwa kipindi hiki.Wanataka kusikia mambo ya ndani ya nchi yao na muelekeo wake wake na hatima zake.Alenge zaidi kwenye mambo ya ndani ya nchi zaidi yanayogusa na kuwaumiza wananchi na mikakati wazi ya kueleweka ya kuyakabili hayo yawagusayo.

    Asiongelee matarajio aongelee ufumbuzi wa hayo yawagusayo wananchi.Aende na ufumbuzi kuliko yale maneno ya “serikali inafikiria itafanya ….. huko mbeleni”.Aende na maneno kama “Serikali imeamua ………”

    Huo ndio ushauri wangu wa haraka.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  2. Michu huyo mbembeni ya Amina ni Chacha au? rip wapendwa...
    Kuhusu hotuba ya JK...kama mnavyojua JK ni msanii tosha japo hajahitimu Chuo cha Sanaa bagamoyo. Yale mambo yote ambayo yanatuumiza vichwa na tunategemea kauli yake lazima atazuga, atagusia kila jambo na mwisho atasema yanashughulikiwa na vyombo husika. Tunajua kwamba uchunguzi wa swala la EPA ni kutuzuga wadanganyika, JK ni miongoni mwa vinara waliotumbua mfuko huu...unafikir atasema nini? kuna mengine mengi kuhusu utekelezaji wa maoni ya tume ya Harrison kuhusu richmond na kibwena ambayo nikiongezea lazima Mithupu utaibania comment hii....mtake msitake JK hana jipya la kutuambia coz katika yote aliyoahaidi kipindi kile Bungeni nadhani ametekeleza asilimia tano ivi tukichukulia na mazonge yaliyoongezeka, kwa mfano badala ya kushughulikia mpasuko wa kisiasa znz ndo taflani zimeongezeka...ukijumlisha yote haya tunasema hajafanya kitu, nitafurahi kama atatuomba radhi wadanganyika na kusema ahadi zake hazitekelezeki.

    Flat screen
    Maryland,US

    ReplyDelete
  3. Yaani jamani Marehemu AMINA alikuwa na shughuli mno, yaani kujitia mbele na kupenda kujiweka karibu na huyo "Mhishimiwa wa kASI MPYA.........MUNGU amsamehe sana huko aliko.

    ReplyDelete
  4. Kesho ni kinyan'anyiro nguo kuchanika asiye na mwana na aeleke jiwe. Ila wadau mshishangae kusiwe na la maana lolote litakalozungumzwa kuhusu EPA

    ReplyDelete
  5. JK hapo alikuwa bado mshamba mshambaa!

    Alikuwa hajaanza KUWIVA bado.

    Si mnamcheki siku hizi alivyokuwa WA PINKI?
    We acha tu

    ReplyDelete
  6. Hivi watanganyika na wazanzibar hamjui kikwete ataongea nini kesho? Ngoja niwadokoleeni!

    Kwanza atatoa pole kwa wabunge na wananchi wa Tarime kwa kupoteza mbunge wao (chachawangwe)atatumia kama dk 10 hivi.

    Pili atazungumzia masikitiko yake kwa kuuwawa kwa maalbino kama dk 20 hivi.

    Tatu atazungumzia kupanda kwa bei ya mafuta hivyo wananchi wafunge mikanda atatumia dk 20,

    Nne atasema report ya epa ndo amekabidhiwa bado anaifanyia kazi wananchi wavute subra matunda yake watayaona (atatumia dk 5)

    Tano na mwisho atasema zanzibar hata yeye mwenyewe hajui kama ni nchi au si nchi, kama alivyosema mzee mwinyi, ataongeza kusema kwamba waasisi nyerere na karume ndo wanajuwa zaidi na bahati mbaya wote ni marehemu sasa, zaidi atasemaikiwa mwinyi ambAe aliingia kwenye madaraka baada ya nyerere hajui jee mimi wa awamu ya nne, tena naingia madarakani nyerere na karume washakufa ntajuwa kweli? Kwa kuwatuliza wazanzibar atasema kama alivyoagiza waziri mkuu wanasheria wakae wajadiliane kisha watoe ufumbuzi!(dk 10)

    Ahsante sana kwa kuniskiliza. Huyo atapeana mikono na spika na waheshimiwa wengine na mafisadi, kisha atapanda gari yake ya bei mbaya (benzi new model) huyooooo ikulu ya cha mwino!!!!

    ReplyDelete
  7. Jk tunakusubiri mkuu maana tayari taarifa iko mikononi sasa ni maamuzi yako ya kiume ndio yatakupa kura tena na kurudisha imani zetu kwani hali ni mbaya sana sasa tunasubiri tukusikie na wewe unasemaje kuhusu hilo je yawezekana kubadili mfumo mzima??

    ReplyDelete
  8. ,,,,mh hii picha!!!
    ila jamani hiyo kesho sijui ataongea nini kweeeli,,,ingawa k, raisi lzm ayaongee maswala aya mazito ambayo nchi yetu inayo sasa,,adi inatia huzuni ila siku yatamwagika ata wakikwepa vp,,,ofkoz dhambi izi zawagusa weeengi sana ambao ndo viongozi now.
    poa let us see tmr

    ReplyDelete
  9. mnh! Jamani wa tz wenzangu hiyo kesho hamna cha maana kitakacho semwa hapo zaidi ya kukatambulishwa kwa mfalme mabinti bungeni kwetu, kwaiyo walala hoi wenzangu tuendelee kuchoma mahindi maana tusipoteze muda wa kusikiliza redio/tv wakati twafwaaa na njaaa, nothing! nothing ! nothing! 3 bila,Bora Mkapa

    ReplyDelete
  10. MAALIM ISSA POLE KWA YANAYOKUSIBU KATIKA SHUGHULI ZA MTANDAO WA “JAMII”. TUNASHUKURU KWA PICHA “MAHIRI” YA MHESHIMIWA “J.K” NA “WALIOMZUNGUKA”.

    USTAADH ..J.K.. NAONA “NYARAKA” ZIMEZUNGUKA KUANZIA “BUNGENI”, MPAKA ZIKAFIKIA “MIKONONI MWAKO”.…..MAMBO YA ”..SWAHIBA..” HAYO YAMETAPAKAA HUMO NDANI….GHABARI KUBWA !!!….. “..SWAHIBA WANAMARADHI..” NA DAWA YA MARADHI NI “..TIBA..”. LAKINI…..INASEMEKANA KWAMBA… “..KINGA NI BORA KULIKO TIBA..”… NA NANIHII….” IS ON YOUR HAND..”

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...