nimebahatika kutembelewa na ugeni mzito katibu wa ccm taswi la london, mh. suzan mzee (kulia), ambaye yupo bongo kwa vekesheni fupi. shoto ni mdogo wake anaitwa nanihii...
nachukua nafasi hii kutoa asante kwa mh. kunitembelea na wakati huo huo kutoa ufafanuzi na kuomba radhi wadau wote kwa kwikwi iliyotuandama juma zima.
ni kwamba, katika juhudi za kufanya globu ya jamii iwe bora zaidi, tumepata server ambayo ina nafasi kubwa hata za kuanzisha libeneke la video kama tulivyoahidi awali. tatizo linakuja kwamba mitambo ya host wetu inakuwa ikiteleza mara kwa mara kudaka link ya globu ya jamii na kusababisha kwikwi ya mara kwa mara.
na ili kukomesha kwikwi hiyo imeonekana bora tuendeleze libeneke kwenye anuani ya issamichuzi.blogspot.com kama ilivyokuwa zamani wakati tukisubiri wahandisi wa host wetu arekebishe mambo.
kunradhi kwa usumbufu unaowapata wadau na nashukuru kwa jinsi maelfu ya wadau wanavyolifuatilia swala hili na kunipa moyo kuwa nisikate tamaa. nami naahidi kuendeleza libeneke bila kusita pamoja na kukumbwa na changamoto za kiufundi ambazo ziko nje ya uwezo wetu.
natumai mtaendelea kutuelewa na kutuvumilia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Tupo pamoja Kaka mpaka kieleweke..

    Ila nina ombi moja, kuhusu hili suala la word verification ambalo mara kwa mara limekuwa mzigo kwangu wakti nikitaka kutuma comment kiasi kwamba hufikia kipindi huwa ninaacha kuandika komenti yangu pale muda unapokuwa unanibana. Sasa Kaka unaonaje ikiwa utaitoa hiyo word verification ili kuturahisishia wadau kuandika komenti na kuituma bila kukumbana na matuta kama hayo ambayo hayana ulazima sana?

    Ni hayo tu Mkuu, natumaini kuwa ombi langu utalifanyia kazi au utalipatia ufafanuzi iwapo ni kinyume na msimamo wako.

    Ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  2. ADVICE
    Kaka michuzi kama vipi baki na address hihii maana naona kama wanakuzingua sana hao mahost wako.
    tunamis sana mambo mkuu wa wilaya ya naniiiii

    ReplyDelete
  3. MICHUZI,
    MJUMBE SI AUWAWI??- MI HUYU DADA KILA SIKU NASEMA HATA MUME WAKE AKINICHUKIA; SI SUPER ELEGANT, POSSES SOME QUALITY ON HER LOOK I CANT EXPLAIN. KAZANA DADA. KAKA UNATAKA KUWA KIONGOZI U HAV THAT PERSONA!

    SHABIKI WAKO # 1 USA.

    ReplyDelete
  4. hana lolote uyo katibu wa ccm,kutafuta umaarufu tu mmeletwa ulaya mje msome mnashabikia mambo ya chama hamna lolote just waste your time
    utakufa bado mdogo wewe wewe unafikiri ccm mchezo shauri yako kuna wazeee pale wanataka kul mpk kufa kwao
    CCM MKEREKETWA

    ReplyDelete
  5. We Michuzi we,
    Achana na Mikonozzzzz hiyo.
    Mwanawasa KAVUTA huku.
    Lete Breking Nyuuuzzzzzzzzzzzz hizo!

    ReplyDelete
  6. watu wanatafuta majina jamani ehee kweli kazi hipo

    ReplyDelete
  7. Mkuu michuzi tuletee mambo achana na hao wakina dada wanakalia kujishauwa kwanza kuna mtu aliwauliza....Na pia mkuu badilisha host kwanza uliponunua hiyo domain name hakuna host??Badilisha bana achana na hao blogger wanakupotezea mda tu maana kila siku site yako ipo down wapige chini wanavyokusumbua watazani hela wanakutokea ya kulipia host au hiyo host ni ya bure???Pamoja mkuu host zipo nyingi na za uwakika kabisa sio hao blogger washamba tu....Pamoja

    ReplyDelete
  8. Umemwambia kwamba kuna kijana wetu anaenda london kutibiwa na tulikuwa tuna tafuta mtu wa kumpa hifadhi kwa wakati atafika pale kwa mda au umesahau kaka?

    ReplyDelete
  9. Naona mpogolo unawakilishwa...... hahahaha, wapi mtu na nusu?

    ReplyDelete
  10. Bw. Misupu huyo dada hajafikia HADHI ya kuitwa MHESHIMIWA kwani tunafahamu fika kuwa Waheshimiwa wanaitwa watu kuanzia ngazi ya Ubunge na SI VINGINEVYO !!!!! Huwa nashangaa kila nisikiapo hata DIWANI wa KATA anaitwa MHESHIMIWA !!!!!! Wadau wenzangu ebu naomba MSAADA wenu kwa hili !!!!

    ReplyDelete
  11. jamani tafadhali mheshimiwa gani anavaa tight jeans wakati wa safari ya publicity?maana kuja kwa michuzi ni publicity flani hivi.

    ReplyDelete
  12. MICHIZI,
    MBONA UNABANIA MAONI YANGU??MIE MDAU NAMBA 1 WA BI SUZY, WALA SINA NIA MBAYA KAMA UNAVOYFIKIRI, KUMTAJA MUMEWE NI KWAVILE NAJUA KAOLEWA. KHAAAA MICHUZI KUMBE MCHUKIZI (HATER) NA WEWE.

    BI SUZY-LAZIMA TULIENDELEZA MIE CAMPAING MANAGER WAKO USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...