ndugu jamaa na marafiki wakiwa uwanja wa ndege wa eapoti kumpokea katibu wa ccm tawi la london mh. suzan mzee alipotua majuzi kwa vekesheni fupi. akihutubia uwanjani hapo mh. mzee alisema kwamba chama kimeshika hatamu huko ughaibuni na kwamba mashina yanazidi kufunguliwa kila mahali, ikionesha jinsi wananchi walivyohamasika kudumisha umoja


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. NI KWELI KABISA, FRIKRA ZA MWENYEKITI KWA "ZINADUMISHA IMANI YA CHAMA" HUKO LONDON NA BILA KUSAHAU VISIWA VYA "JERSEY"

    ReplyDelete
  2. hivi bado mpaka leo watu wanapokelewa na ukoo mzima airport?? duhhh....

    ReplyDelete
  3. Inavyoonekana huyo ilikuwa mara yake ya kwanza kurudi bongo...maana ukooo mzima umekuja,walikuja na daladala nini
    mbona huyo katibu hatumjui huku watu wengine kutafuta umaarufu

    ReplyDelete
  4. Samahani dada lakini umoja unaoutaja hapa ni wa wana ccm sio wa watanzania! sisemi kuwa watanzania hatuna umoja lakini kwa mtazamo wangu matawi ya ccm yanabagua, kwa mtizamo wa kuwa ni lazima uwe mwana ccm, ukiwa ni mtu wa siasa au ni mwiongoni mwa vyama vya upinzani huu sio umoja wako. unaona point yangu hapo? Jumuia yeyote ya watanzania nje ya nchi ni kweli inaweza kuwa na lengo la kudumisha umoja wa watanzania, matawi ya ccm ni kwa wana ccm tu.

    Pia nilisema kwenye post za zamani kidogo kuwa malengo ya matawi haya nje ni kujinufaisha baadhi yenu tu, na kujipatia umaarufu, na sikukosea, imekuwaje unafika tanzania na kutowa hutuba uwanja wa ndege, makatibu wangapi wa matawi ya ccm nyumbani wamefanya hvyo wanapowasili katika mji wowote wa tanzania?

    ReplyDelete
  5. Mdau, unajua ukoo huwa unakuja airport ikiwa wewe ndiye pekee kwenye ukoo uliyebahatika kukanyaga majuu...lol.

    ReplyDelete
  6. Halafu masnduku yenyewe ya zawadi au sijui binafsi zake mawili patamu hapo!!!

    ReplyDelete
  7. Begi lake nimelipenda!

    ReplyDelete
  8. He he he he he..jamani mbavu zangu dah! Michu leo umenifurahisha! Eti akahutubia uwanjani, sasa aliwahutubia ndugu zake, shangazi zake, mama wadogo, mama na wapwa zake, maana ndo nnao waona kwenye picha! Dah ukoo mzima ulifka kumpokea! Hapo mbinde sijui alinunuwa chocolate ngapi?! Yarabi tobaaaaa! Sasa huo mkutano si angeufanyia sebuleni nyumbani?!
    ooooh nimesahau kumbe nyumba ya kupanga chumba kimoja! Ok basi vizuri kutumia nafasi ulioipata hapo uwanja wa ndege!

    ReplyDelete
  9. Hskuna chochote hapo, hakuna cha kushika hatamu wala nini, watu wanadhani wana weza mtumia JK kupata cheo ndio maana wana jifanya kujiunga na chama ili wapate kula, wengini wajanja janja tuu , wanaume wanajua wakijipendekeza wata kamata madaraka na wanawake wana dhani wakijiunga hawakosi ubunge na uwaziri,wengie wanjua watawatamanisha viongozi , Mtakula wa chuya JK sio mjinga kihivyo na wajua wote vizuri.

    ReplyDelete
  10. Hakuna jambo lolote baya kupokelewa na ukoo zaidi inaonyesha ni jinsi gani walivyo na upendo katika familia yao . Mimi nina swali moja tuu mbona sijasikia hata siku moja tawi la CCM likifunguliwa Marekani ?

    ReplyDelete
  11. Yule mtoto aliyekuwa anatafuta hifadhi ya mda wakati wa matibabu london kapata? Hilo ndio swali la kumuuliza huyo katibu

    ReplyDelete
  12. NAONA NILIKUWA NA TYPO KIBAO KWA HIYO MESSAGE HAKUKUFIKIA MLENGWA DADA NANIHII.....KAMA NARUHUSIWA KURUDIA MANENO YANGU NIKUWA NASEMA HIVI....., UNA VERY ELEGANT PERSONALITY AND U HAV THAT KIND OF TOUGH POLITICAL LOOK. KAMA ZA KINA MAMA KATE KAMBA,GETRUDE MONGELA, MARY NAGU, MAMA TIBAIJUKA,NK. KAZA KAMBA DONT WORRY ABOUT WACHUKIZI (MAHATER) KAMA UNAENDEKEZA POLITICS SI THE PATH ULIOCHAGUA? WAO INAWAUMA NINI.KIKWETE ALIENDA KUWA MKUU WA CCM LINDI WHEN HE WAS ALREADY A GRADUATE WA ECONOMICS, DONT U THINK IT HELPED HIM TO LEARN THE GRASS ROOTS LEVEL.

    AGAIN MIE NIKO WA WEWE MPAKA MUMEO ANIFUKUZE, KAMA UNATAFUTA CAMPAIGN MANAGER MIE NIKO HAPA I CAN BE
    DAVID AXELROD WAKO NA WEWE UWE OBAMA MWAMANKE AU SIO!!!!!!!"yes we can"

    SHABIKI WAKO # 1 USA!!!michuzi mjumbe hauwawi.

    ReplyDelete
  13. Kulikua na umati wa watu wa kawaida zaidi ya ndugu zake waliokua wanamsubiri nini?Baadhi ya watu bado washamba sana,eti katoa hotuba?Kweli mnachekesha jamani wandugu

    ReplyDelete
  14. kabla hajaolewa alikuwa anaitwa susan mushi alikuwa anakaa regent estate mitaa hiyo hiyo aliyokuwa anakaa kikwete kwa hiyo kwa kifupi huyu line ya uongozi tayari yupo katika channel hilo halipingiki na kwa taarifa yenu huyu kashaingia katika system ma hater mezeni chupa ila ukiwa fasta katika maisha hulali njaa kwa hiyo apokelewe na ukoo,kijiji,mkoa ahutubie asihutubie hiyo ni kitu ndogo sana compared to foundation aliyoweka period!

    ReplyDelete
  15. Mimi pia CCM damu tena niko hapahapa london!Ila co member kwenye tawi hilo.kwasababu naamini tukianza siasa nje ya nchi yatatokea yale ya CCM na CUF nyumbani.
    Kwa kifupi hilo tawi ni la wauza sura eti mnadhani mtapewa ubunge!Lofa kama wewe katibu Susan Mzee tena unatutia aibu wa2 wa ulaya!unarudi home na sanduku linalouzwa na wamachinga mitaani!!Mgauni kama mama mpika vitumbua bana!!
    Sasa hapo airport ulihutubia kina nani?coz tunaona ndugu zako tu!
    Ila kaka Michuzi wewe Hongera sana na Mungu akuzidishie uhai!Maana unajua kumpamba kila raia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...