wadau kunradhi,
mwenzenu kila ninapokwenda neshno huwa siishi kujiuliza endapo kama ni sawa kwa magari kuegeshwa juu ya majani badala ya juu ya sementi. sasa hii staili sijui ni ya kichina-china ama kibongo-bongo. naomba kuondolewa tongotongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi, ukiona hivyo ndo ujue jinsi wabongo tulivyo. Na hizo ni ishara kwamba mambo madogo-madogo ya kistaarabu tu hatuyawezi. Sasa itakuwaje kudhibiti RUSHWA,UKIMWI na UFISADI?

    ReplyDelete
  2. Hiyo picha haielezi ukweli na wala sijafika huo uwanja

    Hebu weka basi atleast lane mbili?

    Inawezekana walivyojenga ndio hivyo kuwa watu wapaki kwenye majani lakini hivyo pavement ni njia tu

    Kama hiyo sehemu ni ndogo watu wakipaki magari yao je wanaotaka kuingia na kutoka itakuaje? watumie majani kama njia.

    Naona wachina ndio waliokua wanabania hela. Wangeweka cement sehemu yote halafu wachore tu alama za sehemu za kupaki magari ni wapi na wapi pa kuingilia

    ReplyDelete
  3. tatizo ni elimu tu, bado hatujui umuhimu ya hayo majani ndio maana inavyoonekana kupaki kwenye majani ndio sawa kutokana na picha

    ReplyDelete
  4. kwanza hayo si majani ni nyasi.Jifunze kiswahili kabla ya kukosoa.
    Btw hapa ni sawa na kuvua kandambili na kuingia ndani ya choo cha makuti pekupeku

    ReplyDelete
  5. Hata mimi najiuliza maswali kama Anon nambari one, kama akili yetu haiwezi kufanya kazi kiasi ya kujua kwamba majani ni mojawapo ya pambo zuri na badala yake tunaliteketeza wenyewe basi Ufisadi na rushwa haviwezekani.
    Ni sababu zile zile zinafanya miji yetu inakuwa michaafu kupindukia kwasababu tumeshindwa kufungua akili zetu na kujua mambo kama hayo ndo yanazidi kutudidimiza

    ReplyDelete
  6. jamani sijui nyasi au garden bongo???????/ hiyo ni kibongo bongo sio kichina, yaani mpaka roho inauma jinsi walivyozikandamiza na hizo prado zao na mabenzi. mweee ustaraabu sifuri kabisa.

    ReplyDelete
  7. Mkiambiwa kuwa ngozi nyeusi hamjaweza kujitawala mnaona mnatukanwa, halafu mnakaa mnalala mika mbona mamtoni kuzuri huku kwetu vumbi. mtoni kuna ustaarabu sehumu ya kupaki magari mmewekewa sasa unapopaki kwenye hayo majani inamaana waliyo yapanda hayo majani wanaomokwa au inakuwaje?au ndiyo hayo magari yenu ya mtumba ambayo ndani plastiki tupu ndiyo yanadhamani zaidi? au ndiyo maendeleo yanaharakishwa wakati waswahili hawako tayari? nyie kimbizeni mwenge tu na kucheza mkole halafu mnadai eti mmelaaniwa,wana watoka pabaya nyie

    Mbega

    ReplyDelete
  8. GO "GREEN"...GO.."GREEN" NI VIZURI SANA WATANZANIA MFANO WA KUIGWA

    ReplyDelete
  9. Bahati nzuri mimi nimeziona wakati wanapanda hizi nyasi ni sehemu maalum ya maegesho,kuna jamaa mmoja amesema wachina walikuwa wanabania cement, hapana pale pole pamesakafiwa halafu wakaacha vishimo vingi vingi ambavyo ndo vimepandwa nyasi kama ukiangalia vizuri utaona nyasi zimeota mafungufungu ndo dizaini ya parking walivyo tengeneza, na sio watu wamepaki kimakosa kama wengi mnavyofikiri, ule ni uwanja wa kisasa, wahusika wasingekubali watu waegeshe kimakosa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...