baada ya kuwakilisha jimbo la nanihii niko mapumzikoni na wah. iddi azan (ilala), zainabu vullu (viti maalumu) na mdau saidi yakubu ambaye baada ya kupiga libeneke kule BBC sasa yupo dodoma akiwa kama afisa mratibu wa bunge la jumuiya ya madola.
leo kazi ilikuwa ni moja tu. snepu kwa wingi na suti ya kuazima. hapo juu toka shoto ni juma dihule (mtanania) selemani mpochi (guardian) athumani hamisi (habari leo) na deus mushi (dodoma studio)
hapo kaongezeka pedejee kanini (kaunda suti) na mdau wa dar
niko na japhet sanga nje ya ofisi za daily news na habari leo hapa dodoma
mhariri wa habari wa daily news japhet sanga akiwa amezungukwa na wadau wa ral internet cafe ambayo ni maarufu sana hapa dom kwa spidi ya mtandao wake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Michuzi, msalamie sana Japhet! - Chemi

    ReplyDelete
  2. kweli suti za kuazima haziongopi kwani watu kama majokeli

    ReplyDelete
  3. Mkuu Wa Nanilii Naomba Nikuulize...MBONA PICHA ZOTE MKONO UPO MFUKONI Au UnaTune Hirizi???

    ReplyDelete
  4. ukijua kuwa umefanya jambo sivyo-ndivyo na unajua dhahiri waosha vinywe hawatalala bila ya kusema neno, basi unachostahili kufanya ni kwenda kule woasha wanapokwenda kabla ya wao hawajafika.
    ndio trick ambayo michuzi ameamua kuitumia ktk huu mtundiko wa suti ya kuazima...

    tukiachana na hayo ya suti,mimi naomba msaada mmoja wadau tusaidiane;
    hawa wabunge wetu huitwa waheshimiwa na sometimes hata wao wenyewe hujiita Waheshimiwa..
    hivi inamaana kwamba sie tuliobakia ni wadharauliwa? naomba msaada wadau

    ReplyDelete
  5. Hapo suti ya Athumani bwn!!! imemkubali kishenzi!

    ReplyDelete
  6. Huyo asiye na suti, si ni Peter huyu!! Amenenepa haswa!

    ReplyDelete
  7. Ndugu, Hiyo tabia ya kusema watu kijanja siyo nzuri, yaani wewe umeguandua kuwa wenzako wameazima suti waje nazo Dodoma halafu unatoa siri zao, hakika wewe siyo rafiki mwema, Nimekuogopa kaka, Anyway umeeleweka kwa kutaka watu wajue kuwa uliopiga nao picha na suti zao hizo wameazima.

    ReplyDelete
  8. Sir ISSA NAONA MKONO UKO MFUKONI "YAHE" DAWA YAKE NI "ANT ITCHING"

    ReplyDelete
  9. Michuzi leo umemsahau Peter Twite wa Majira? unamwita mdau wa dar?

    ReplyDelete
  10. HEEEEE KWELI HAKUNA WEMBAMBA NAMKUMBUKA ATHUMANI ENZI ZA ZE GADIAN MH ALIKUWA KAMA FAGIO LA CHELEWA ALKINI ALIKUWA ANALIPA KULIKO SASA MWAMBIE JK AMPUNGUZIE TIRIPU.

    KAKA JAFET NAE KAPENDEZA SANA NAONA AMEPUNGUZA ULABUU MANAKE ALIKUWA HALI ILA NGANO DU ILIKUWA KWA KWENDA MBELE MPAKA MIDOMO IKAUNGUA . KAZI KWELI KWELI ( USIBANE ACHA TUFURAHI)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...