Wabongo London kuwavaa wabongo Slough J'mosi
Timu ya wabongo Edmonton, London Jumamosi ijayo itajitupa uwanjani kuikaribisha timu ya wabongo ya Slough,Katika mchezo mkali utakaochezwa katika uwanja wa wazi uliopo Tottenham.
kwa mujibu wa mratibu wa mchezo huo, Said John alisema maandalizi yote kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika na iliyobaki ni kusubiri siku hiyo ifike.
Said alisema mchezo huo utakuwa mahususi kwa ajili ya kuvunja jungu kabla ya kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani, utakuwa wa vuta nikuvuta kwa jinsi timu zote mbilizilivyoweza kupania mchezo huo.
Mratibu huyo alisema kila upande wake umejiandaa vyaha kuibuka na ushindi katika mchezo huo, japokuwa Slough kupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo kutokana na kuwa na wachezaji wengi wazoefu kama kina Athumani China, Eddy Abdallah,Muddy Chella na wengine wengi.
Kwa upande wa London, timu hiyo itakuwa chini ya mwenyewe Said John, Mzee, John, Pinto na wengine wengi.Lakini London itamkosa kipa wake tegemeo Abdallah Ziebi "London one" ambae amekwenda kwa majaribio katika moja ya klabu kubwa Tanzania.
Baada ya mchezo huo, kutakuwa na tafrija ndogo ya vinywaji na nyama choma.
Saidi John amewataka wabongo wote wakazi wa London kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ili kuweka rikodi yao ya mwaka huu ambayo hawajapoteza hata mchezo mmoja tangu kuanza kwa michezo ya kirafiki katika kipindi hicki cha majira ya joto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...