
Habari za leo tena ndugu wanajumuiya,
Yafuatayo ni maendeleo ya tulikofikia katika maandalizi ya kuusafirisha mwili wa marehemu mama yetu pichani.
Umepatikana ukumbi wa kufanyia harambee hapo kesho 09/08/08 kuanzia saa kumi jioni (tunaombwa kuwahi).
Ukumbi unaitwa SAFARI HALL uliopo BISSONNET.
Anwani ni : 9651 Bissonnet ste 105,
Houston
TX 77036.
Gharama ya ukumbi, muziki na vipaza sauti ni dola elfu moja na mia tatu ($1,300.00) .
Tunaomba kukumbusha akina kaka/baba walete vinywaji na akina dada/mama walete vyakula Familia ya marehemu ilituomba nafasi mbili za wasindikizaji wa mwili.
Mpaka sasa tuna jina la mtoto wa marehemu ANDREW WELLA, tutatoa jina lingine mara wakifikia uamuzi. Kiasi kilichopo mkononi ni dola mia nane ($800.00), rambirambi zinaendelea kupokelewa nyumbani kwa Bw. Jonas Mbuya. Anwani ni:
2751 Wallingford Dr.
#2912Houston,
TX 77042….
Gate code *2369
Wanajumuiya watatu wamejitolea kuendesha shughuli ya harambee (MCs) hapo kesho, nao ni Bw. Sam mkumbo, Dada Nuru Mazola, na kaka Andrew Njau Karatasi (documents) zote zinazohu usafirishaji wa mwili wa marehemu kutoka ubalozini tayari zinaendelea kushughulikiwa kwa wakati huu.
Mahali pa kuhifadhi mwili wa marehemu mama yetu (Funeral Home) pamepatikana. Gharama yake ni dola elfu tisa ($9,000.00). Hii ni pamoja na kuandaa makaratasi ya ubalozini, kutayarisha, kuhifadhi na kuusafirisha mwili hadi Dar es Salaam, Tanzania.
Jina na anwani ni:
FOREST LANE FUNERAL HOME
8706 ALMEDA GENOA RD,
HOUSTON
TX 77075.
Namba ya simu ni
713-991-9000.
Fulana (T-Shirts) kwa ajili ya mnada zinaandaliwa.
Tunatarajia kuwa na fulana hamsini (50) zenye picha ya marehemu. Kama mahitaji (demand) yatakuwa makubwa zaidi ya haya tutauza karatasi (VOCHA) maalumu ili kuweza kuwatengenezea wanaohitaji hapo baadae.
Taarifa zaidi zitatolewa kwa kadri tutakavyozipata. Kwa niaba ya familia tunawashukuruni nyote kwa kuendelea kutufariji.
EPHRAIM MPENDAAMANIM
semaji wa msiba(kwa niaba)
Poleni wafiwa, Mungu wa Imani,ampumzishe Mama yetu mahala mema peponi,Pia napenda kuwapongeza wenzentu wa Htown kwa moyo wao wa ushirikiano wakati wa matatizo na kufanikisha kile wanachotakiwa kutekeleza kila wanapopatwa na matatizo .Kwa kweli kusahau tofauti zenu na kuwa kitu kimoja inapowabidi kuwa hivyo ni mfano wa kuigwa, nimeishi miji kadhaa hapa Marekani lakini HOuston ni KIBOKO, HONGERENI SANA. Nimekuja hapa kutembea lakini nimefurahishwa na mnavyoshirikiana na Munu Awajali msibadili mioyo yenu katika hilo na mzidishiwe, Mdau Usa.
ReplyDelete