Hello Bro Michuzi,
Pole na kazi kaka yangu ya kuzunguka huku na kuko, Mimi ni madada na ni mkereketwa sana wa mpira hasa Taifa Stars, hata kama tuna fungwa lakini siku zote unaambiwaa mtoto aanzii kukimbia, anza kukaa ana hata akianza kukaa basi jua mpaka akaze atakuwa kasha dondoka mara kibao.
Sasa basi nilio kuwa nataka kuwasilisha kwako ni hili. kwanini TFF wametuwekea Mpira siku ya J5 na wanajua kabisa watu wengi tuna kuwa makazini, halafu wamewka muda mbaya saa 10 unategemea tutoke mabonde poromoka mpaka huko si itakuwa mpira umeisha jamani, hawaja tutendeaa haki.
Michuzi naomba uwasilishee hii kwa wenzangu katika blogu yetu ya jamii labda wana weza kunipa mawazo mengine zaidi, au labda mie nimekosea kufikiria.
Sina mengi ni mimi wako,
Mkereketwaa wa Mpira
Mdau MGM
JIBU KWA UFUPI NI KWAMBA MECHI ZA KIMATAIFA KAMA ZA KIRAFIKI AU MASHINDANO YANAYOTAMBULIKA NA FIFA YANA RATIBA ZAKE,SASA HIYO MECHI YA JUMATANO NA GHANA NI YA KIRAFIKI AMBAYO INATAMBULIWA NA FIFA HIVYO IKO KWENYE KARENDA YAO AMBAO INARUHUSU MECHI ZICHEZWE JNNE AU JTANO YA WIKI YA 3 YA MWEZI WA 8.KUHUSU SAA MNAJICHAGULIA WENYEWE KUTOKANA NA BIASHARA AU HALI YA HEWA,N.K.KUMBUKA TIMU YA TAIFA INAUNDWA NA WACHEZAJI KUTOKA VILABU HIVYO LAZIMA KUWE NA KARENDA KUEPUKA MIGONGANO NA VILABU.
ReplyDeleteOCD