Habari za leo ndugu wanajumuiya,
Alfajiri ya leo tumepokea taarifa ya msiba wa mama yetu mpendwa Ethro Yohane Gadau. Mama Ethro amefariki dunia asubuhi ya leo tarehe 7 August 2008 katika hospitali ya West Houston Medical Center iliyopo hapa Houston kutokana na "shinikizo la damu" lililompata tarehe 5 August 2008.


Marehemu Ethro alizaliwa tarehe 12 Decemba mwaka 1956. Marehemu, alikuja Houston miezi miwili iliyopita kumtunza mwanae, Jane Wella, na mjukuu wake mchanga, Naomi Mbuyah.. Ameacha mume (Eleutherius J. Wella), watoto wanne (Pamella, Andrew, Jane, na Clara), na wajukuu wawili – Labron Wella, na Naomi Mbuyah.


Kikao cha awali cha maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu mama yetu kwenda Dar-es-Salaam, Tanzania kimefanyika leo jioni 7 August 2008 nyumbani kwa Jonas Mbuya. Kikao hiki kilichoongozwa na Mzee Leonard Tenende kimechagua viongozi wa msiba huu kama ifuatavyo:
M/Kiti: Mathew Mohono 281 804 6478
M/Hazina: Jonas Mbuya 832 428 5621
Wasemaji wa msiba huu: Ephraim Mpendaamani na Domino
Wanakamati: Nuru Mazola,Lilian Maliti,Toni Makinda, Margareth Jenga, Mami Kasomi na Mariam Janguo.

Pia kikao hiki kwa pamoja kimeamua kuwa na harambee siku ya Jumamosi tarehe 9 August 2008 kuanzia saa kumi kamili jioni (4pm) (ukumbi bado unashughulikiwa na tutawajulisha mara tu tukipata taarifa). Mipango ya sehemu ya kuhifadhia mwili wa marehemu bado inashughulikiwa na Bw. Juma Maswanya. Juhudi zinafanyika ili hiyo sehemu tuweze kuitumia kuaga mwili wa marehemu siku ya Jumapili(August 10).


Makadirio ya usafirishaji wa mwili ni dola elfu kumi na nane ($18,000.00). Makadirio haya yanahusisha gharama zote za kuufikisha mwili wa mama yetu mpendwa nyumbani Tanzania. Kwasababu hiyo basi, kwa niaba ya familia ya Mzee Wella wanajumuiya tunaombwa tujitolee kwa kadri ya uwezo wetu ili tuweze kufanikisha lengo letu la $18000.


Wanajumuiya tunaombwa tuwe na kiwango cha chini cha dola mia($100) kama rambirambi. Pia kama una chochote ambacho ungependa kutoa kwa ajili ya mnada tafadhali wasiliana na yeyote hapo juu.


Pia kwa kurahisisha shughuli hii akaunti imefunguliwa kwa ajili ya wale walio nje ya jiji la Houston.

Benki ni WACHOVIA.

Routing Number: 111015159

Akaunti namba ni: 1010199794410.

Waliopo kwenye akaunti hii ni

JONAS MBUYA na ANDREW WELLA
Tumfariji Jane – mwanajumuia mwenzetu – pamoja na familia yake katika kipindi hiki kigumu sana cha kumpoteza mama yetu mpenzi. Anwani ya nyumbani kwake ni:
2751 Wallingford Dr. #2912
Houston, TX 77042….. Gate code 2369
Tunaomba akina mama/dada walete vyakula na akina kaka/baba walete vinywaji wanapokuja msibani na siku ya harambee.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina
EPHRAIM MPENDAAMANI
Msemaji wa Msiba (kwa niaba)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bwana hutoa na huchukua! Mungu amlaze mahali pema peponi MAMA yetu! Pole Jane na Jonna pamoja na ndugu wote !
    Victor(houston).

    ReplyDelete
  2. Mchango ni mchango jamani.Mambo ya kusema kiwango kwenye kitu kama msiba si vizuri kabisa.

    Tubadili hiyo tabia.Kama ilitakiwa 18,000 dollars si kweli kwamba kila mwanajumuiya anatakiwa kutoa 100$.Houston kuna watanzania wengi sana.Kwa kufikisha 18,000dollars kila mtanzania angechanga hata 30-50dollars.

    Maisha magumu jamani.Tuchangishwe kiwango kutokana na mahitaji.

    ReplyDelete
  3. Anonymous August 09, 2008 6:38 AM

    Kumbuka wahenga walisema 'kutoa ni moyo na wala si utajiri'

    Spirit waliyonayo wa-TZ wa Houston ni ya mfano na wa kuigwa. Walikutana Jumamosi na wakatekeleza yale waliyoombwa na wengine wametoa zaidi ya $100.

    Tusikimbilie kwenye kulalamika, tujaribu kwanza na kuona uwezo wetu ni upi.

    Ninawapongeza kwa dhati kabisa wale wote waliojitoa katika kufanikisha na kuhakikisha mwili wa mama wa mwenzetu unasafirishwa kwenda nyumbani Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...