Mbunge wa Mchinga Mh. Mudhihir Mudhihir akichangia bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, bungeni mjini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mzee Mudhihr ile hoja yako bungeni wiki mbili zilopita , ya kukataa jina la machinga kutumika kwa wachuuzi wa vitu vya mikononi mtaani, kwa kweli itakubidi ufanye kazi ya ziada kutetea au kuwaelimisha wananchi, kwani limeshaenea mno na limeota mizizi midomoni mwa watu wengi, kama unavyolalamika ndugu zako wanadhalilishwa likitumiwa kuita wachuuzi hao machinga.
    Wazo lako la pili la kuwapatia wachuuzi hao eneo zuri la kufanyia biashara zao badala ya kubeba duka mabegani na kuzunguka ni zuri mmo na linahitaji kutiliwa mkazo zaidi ili lifanikiwe.

    ReplyDelete
  2. aisee babaangu meno ya mbunge yanahitaji whitening or something like that, mbunge hana access ya dentist woooa!!!!

    ReplyDelete
  3. Wewe anoni wa 12:00AM acha ushamba wa kimawazo, changia vitu vya kimaendeleo. Sina shaka, wewe ni mmoja wa waliokimbia baiolojia. Pole lakini.

    Wadau, Mh. Mudhihir wakati akichangia hotuba ya Ofisi ya Makamu wa Rais alionge pointi moja muhimu sana juu ya kudumisha muungano wetu, ambayo ilinikuna. Alisema dawa chungu mara nyingi ni tiba nzuri. Dawa ya muungano ni kuvumilia kunywa dawa ya 'kuondoa habari za SMZ vikiwemo bendera yao n.k' na kuelekea kwenye serikali moja!

    Kwa maneno mengine, Zanzibar iwe sio tu sehemu ya Jamhuri ya Muungano, bali 'mkoa.' Mimi naungana na Mh.Mudhihir, nikiwa kama mzanzibar mpenda Tanzania, huwa nachukizwa sana na maneo "Tanganyika" na "Zanzibar" enzi hii.

    Mudhihir alitaadharisha kuwa wazanzibar tusilaumiwe kwa kupenda jina Zanzibar, kinyume nanyi wenzetu wa Bara amba hamjazoe jina Tanganyika (kama nilivyo nami pia). Tatizo ni kuwa sisi Tumekulia Zanzibar na ninyi mmekulia Tanzania.

    TAFAKARI
    Wao wamekulia Tanzania, na sisi tumekulia Zanzibar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...