
Rais wa zambia Levy Mwanawasa, 59, amekufa mjini Paris kutokana na ugonjwa wa moyo, taarifa ya BBC imesema.
Kiongozi huyo alipatwa na shinikizo la Moyo Juni mwaka huu.Makamu wa Rais Rupiah Banda, ambaye anatarajiwa kukaimu nafasi yake,alitangaza kifo cha rais huyo kwa njia ya televisheni.
Alisema Rais Mwanawasa amefariki leo saa nne unusu asubuhi, na kwamba
Serikali (ya ZAmbia) imetangaza siku saba za maomboleozo kuanzia leo.
Mwanawasa ameacha mjane na watoto sita.
Bro. Unaonaje badala ya kutumia neno amekufa, ukaandika kuwa amefariki au ameaga dunia ili kupunguza ukali wa maneno?
ReplyDeleteManake kwa utamaduni wetu kusema kuwa mtu amekufa inakuwa haijakaa njema.
Ni hayo tu. ingawa maoni yangu kuhusu word verification umeyatupa kapuni.
Ubarikiwe Bro.
Alikuwa Raisi safi sana huyu kuliko karibu maraisi wote wa Afrika kwa kupenda wawekezaji wadogo waafrika ngozi nyeusi..
ReplyDeleteKama kuna mtu alipenda wawekezaji waafrika ni huyu.aliwaheshimu hadi wawekezaji wadogo kabisa wa kiwango cha machinga..
Zambia ndiyo nchi pekee Afrika mashariki, kati na kusini ambako kumejaa wawekezaji wadogo wa Afrika weusi kutoka nchi nyingi za Afrika .Ukienda utawakuta Watanzania kibao kuanzia karibu kila kabila la Tanzania liko kule,Warundi,wanyarwanda,wakongo,wazimbabwe,waafrika ya kusini,wanamibia,waswazi n.k wanaendesha biashara zao kihalali bila bughudha kabisa kutoka serikali ya Mwanawasa..
Mwanawasa alitambua kuwa wawekezaji wadogo waafrika weusi kutoka mataifa mengine ni muhimu kwa uchumi jikimu hasa wa Afrika na Zambia.Wafanyabiashara wadogo waafrika toka nchi za Afrika wamejaa sana Zambia.Wana maduka,viwanda,n.k na wanapewa leseni na hawabughudhiwi tofauti na nchi kama Tanzania,Kenya na Uganda ambako watu wanajifanya wazawa sana na wana utaifa sana wakati utaifa wenyewe ni wa kuwakataa waafrika wenzao na kuwakumbatia wahindi na waarabu,wazungu au watu wenye mitaji mikubwa toka nje ya bara la Afrika.
Kama kuna Raisi mfano wa wengine kuiga kuwainua waafrika wengine kwenye eneo la uwekezaji wa watu wadogo wenye mitaji midogo kutoka mataifa mengine ya kiafrika na kuwatambua na kuwaheshimu Mwanawasa ni mfano mzuri tofauti na nchi nyingine ambako wazungu,wahindi na waarabu ndio hasa wanaonekana ndio wawekezaji na wanasiasa wanashindana kujikomba kwao na kuwatambua kama ndio wenyewe kwa uwezekezaji na kuwakimbiza mitaani kwa viboko machinga wao wa kiafrika na kuwatoa vijijini wawekezaji wadogo waafrika ngozi nyeusi wanaochimba dhahabu kwa majembe ya mikono ili wawapishe watu wa nje waje wachimbe na magreda!!!.Hata mchimba dhahabu kwa jembe la mkono ni mwekezaji wa kiwango chake cha mtaji huo wa jembe alichojaliwa na mola wake hicho ndicho nilichojifunza kwa Mwanawasa na siasa zake za kujali waaafrika wawekezaji wadogo.
Hata kama Afrika au dunia haitakukumbuka mimi binafsi nitakukumbuka kama shujaa wa Afrika na mheshimu waafrika na mitaji yao midogo.
Na mazishi yako lazima nitahudhuria.
I salute you Mwanawasa.Rest in PEACE
Koloboi@yahoo.com
jamani mbona nimemuona jumapili china anaangalia Olympic tena alikuwa anapiga picha na mabondia wa Zambia loh, maisha matamu lakini mafupi.Maskini Michuzi mungu awarehemu. mwana wa saa! I can believe my eyes
ReplyDeleteKoloboi thanks a lot kwa kuliona hilo mzee na Mungu akubariki, Im sure wengi walikuwa hawajui hayo uliyosema.
ReplyDeleteKwa kuongezea, Mwanawasa alikuwa sumu ya ufisadi, last time nimeenda Zambia June this year nimekuta kesi kibao za former Generals, IGP, ministers na wengine kibao ambao walitumia vibaya madaraka yao kujipatia fedha chafu. Ingekuwa hapa kwetu ina maana akina nanii hii wetu wote wamgekuwa ndani.
Kingine ni uchungu na nchi yake. Kupitia yeye Zambia iliintroduce windfall tax ambayo ni kodi isiyofungwa na bei ya mkataba bali bei ya soko ya madini ndio inayodetermine base ya tax. Hili limetushinda sisi maskini Mungu atusaidie. Mfano bei ya ounce moja ya gold ni kama dola 350 wakati bei halisi ya soko ni kama dola 1000 kwa sasa, pesa tunayopoteza hapo Mungu anajuwa. Zambia mwaka jana peke yake waliokoa dola mil 400 kupitia windfall tax ambazo zingepotea kama hapa kwetu.
Mwanawasa, mimi, koloboia na wengineo wote wenye uchungu na bara hili tutakukumbuka daima. Amen.
Bobby