Uhamasishaji wa RAFDA Mwanza na Arusha uliofanyika wiki hii uliendelea vizuri.
Mwanza imeonyesha mwamko zaidi kwani wabunifu walijitokeza kwa wingi zaidi wengi wao wakiwa wana ujuzi wa fani hii kwani tayari wana majina makubwa kwenye ulimwengu wa fashion mjini hapo.
Fomu zilinunuliwa kwa wingi na wabunifu wa Mwanza wameonyesha kwamba wanataka taji la RAFDA mwaka huu liende jijini hapo.
Kwa upande wa Arusha, jiji hilo limeonyesha kwamba ubunifu wa mavazi hauna msisimko sana hivyo ilibidi timu ya uhamasishaji ya REDDS ifanye kazi ya ziada kuhamasisha kwenye maredio, na kuzunguka kenye vyuo mbali mbali jijini hapo.
Wakazi wa Arusha wanaombwa wajitokeze kwa wingi kununua fomu hizo na kujiunga kwenye shaindano hili lenye kunyanyua vipaji vya ubunifu wa mavazi ili waweze kushindana na kufikia viwango vya miji kama Dar es Salaam na Mwanza.
Mwanza fomu zinapatikana Flora Saloon na Lakairo hotel,
Arusha zinapatikana Tripple A, Angel Saloon na IMPALA HOTEL.
Ziara za uhamasishaji zinaendelea jijini Moshi (25th August)- leopald Hotel saa 4 asubuhi,
Tanga (26th August) - Mkonge Hotel saa nane mchana,
Zanzibar (28th August) African House saa 8 mchana
na Morogoro - Morogoro Hotel (30th August) saa 4 asubuhi.
hivyo wapenda ubunifu wa mavazi wanaaswa wajitokeze kwa wingi kuhudhuria semiza hizi za uhamasishaji.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 11 September 2008.
Mshindi wa shindano hili atajinyakulia dolla 5000 za kimarekani na safari ya kutembelea juma la mitindo Africa ya Kusini pamoja na mafunzo ya wiki moja ya ubunifu chini ya mbunifu maarufu Sonwabile Ndewale.
KIWIA, Irene E.
Director
Beautiful Tanzanie Agency
Cell:+255 754 611 213
Mdogo wangu Sophia, nimefurahi umekuwa mkubwa tena binti mrembo. Mara ya mwisho nilikuona Tanga miaka ya 90 wakati mzee wako akiwa meneja mkuu wa kiwanda cha mbolea. Mimi ni rafiki wa dada yako Nurieth
ReplyDeleteSophia good work, but REDDS na Irene Kiwia hebu tuambieni ina maana kuwa huyu Redds ambassador alipojitoa ndio hakuna kati ya wale 25 waliobaki? Mlipoenda Mwanza hamkuchagua wa pili na wa3 duh ninyi ni kiboko. Sasa Sophia ameshiriki mwaka gani? Mlitakiwa basi angalau mtoe statement kuwa mwaka huu hakuna wa Redds fashion ambassador... duh poleni, na hao Vodacom mbona huyo wao nae kimya? au ndio ameenda kujiandaa na Miss world? alisema namba moja inamuandama so atakuwa namba moja pia huko.. haya lets wait and see.
ReplyDeleteHey!!
ReplyDeleteMichuzi nisaidie nipate number ya huyo mwenye suluali nyeupe.
Roho yangu imemdondokea....nipo mbali na Tanzania la sivyo ningemtafuta.
Nitafutie hata e-mail yake.
jibu nitaliangalia kwenye comment za picha hii hii.
Mdau