mkurugenzi wa mauzo wa zain herbert louis akisoma jina la mshindi wa Rav4 wa mwezi huu leo


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain inayotoa huduma katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, leo imemchagua, Edwin Alkech mwenye umri wa miaka 33, aliyebahatika kuibuka mshindi wa saba wa zawadi ya gari jipya aina ya RAV 4 jijini Dar es Salaam.
Edwin, mkazi wa Tabora ambaye ni askari wanyamapori, aliibuka mshindi katika bahati nasibu iliyoendeshwa Dar es Salaam leo kwenye ofisi za makao makuu ya Zain.
Gari hilo ni moja kati ya magari 11 yanayotolewa na kampuni namba moja nchini ya simu za mkononi ya Zain Tanzania katika promosheni yake kubwa kuliko zote ya Endesha Ndoto 2.
“Kama mnavyofahamu Zain Tanzania bado inaendeleza jitihada zake za kubadilisha maisha ya wateja wake kwa kuwazawadia magari mapya kutoka Toyota Tanzania yakiwa yamesajiliwa kwa jina la mshindi na kulipiwa ushuru na bima zote husika.
“Zain, kampuni namba moja ya simu za mkononi nchini inaendesha promosheni ya Endesha Ndoto 2, tutakabidhi jumla ya magari 11 mapya kwa Watanzania wenye bahati likiwemo jipya la kifahari aina ya Toyota Land Cruizer.

Leo tumemchagua mshindi wa saba aliyenyakua gari aina ya Toyota RAV 4,” alisema Margaret Kositany, Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania.

Promosheni ya Endesha Ndoto ni sehemu ya programu endelevu ya Zain Tanzania. “Lengo letu ni kuboresha maisha ya wateja wetu na kuwafanya waishi kwa raha zaidi kwa kuzingatia kauli mbiu yetu ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa),” alisema Margaret.

Katika mahojiano na Meneja Uhusiano huyo wa Zain Tanzania, badaa ya kuibuka mshindi, Edwin alisema amefurahi kuibuka mshindi na ataendelea kutumia huduma za Zain kama kawaida.

Mpaka sasa droo ya Endesha Ndoto Yako 2 ya Zain imekwishawawezesha watu sita kuibuka washindi wa magari aina ya RAV 4. Mshindi wa kwanza alitoka Dar es Salaam, wa pili alitoka mkoani Mbeya, wa tatu Iringa, wa nne Pwani, wa tano Tanga na wa sita Dar es Salaam.

Ili kushiriki katika promosheni ya Endesha Ndaoto 2, mteja anapaswa kutuma sms ya neno ndoto kwenda nambari 100 na atakuwa ameingia rasmi kwenye promosheni hiyo.

Mbali ya zawadi ya magari, Zain pia inatoa zawadi nyingine anuwai kupitia Ndoto Pointi. Kila mara mteja wa Zain anapozungumza anajisogeza karibu na Ndoto Pointi. Kwa kila Tsh 500 anayozungumza anajipatia ndoto pointi moja.
“Mteja akifika kati ya Ndoto Pointi 1,000 hadi 3,000 anajishindia kufurishi cha zawadi kutoka Zain, akifika Ndoto Pointi 3,001 hadi 5,000, anajishindia simu mpya aina ya Nokia 1110i. Mteja akifika pointi 5,001 hadi 7,001 anajishindia simu aina ya Nokia 1650 wakati pointi 7,001 hadi 9,000 anajinyakulia Nokia 5310 au Ipod. Pointi 9,001 na kuendelea mteja anajishindia simu ya kisasa ya Blackberry bure,” alisema Margaret.

Margaret aliwatahadharisha Watanzania kuwa makini na jinsi taarifa za matapeli wanaowalaghai watoe pesa, na akabainisha kwamba pale mshindi anapopatikana, Zain Tanzania haitumi sms, bali hupiga simu na mshindi hahitaji kulipia gharama zozote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...