
mnenguaji mahiri wa tangwa pepeta aisha mohamed (pichani) maarufu kama aisha madinda usiku huu amekanusha habari zinazopasha kwamba ameamua kustaafu kunengua na kuanza kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali. mahojiano yetu kwa njia ya simu yalikuwa kama ifuatavyo:
mie: habari za leo da'aisha
yeye: nzuri tu kaka, sh'kamoo...
mie: marhaba, ushafuturu?
yeye: eeee. tayari. ndo najipumzisha kidogo kisha nipige msala
mie: enhe, lete habari, nasikia unastaafu muziki...
yeye: ai jamani, mie huyo? nani kasema?
mie: nimesikia sasa hivi redio clouds fm wakisema hivyo. wanasema umeamua kuwa mjasiriamali na kuachana na mambo ya kunengua jukwaani..
yeye: si, kweli
mie: unasemaaa.... (hapa sauti inakatika-katika)
yeye: nasema hivi, sio kweli. hayo maneno si ya kweli.
mie: enhe, ukweli ni upi?
yeye: ukweli ni kwamba mie sijaacha kazi. na wala sijastaafu. mbona naendelea tu....
mie: sasa huu uvumi unatokana na nini....
yeye: nashangaa. unajue eee.... juzi kuna mtangazji mmoja wa eatv anaitwa maimatha nasikia alitangaza kuwa nastaafu muziki na kwamba nataka kuanza biashara
mie: enhee...
yeye: mie kwanza sijawahi kuongea na maimatha. halafu baada ya kutangazwa huko, kuna mwandishi mwingine nakanipigia kutaka kujua ukweli kama ulivyofanya wewe saa hizi
mie: enheee, halafu
yeye: huyo mwandishi hakunipata, na wala sijaongea naye. kesho yake nasikia naandikwa gazetini kwamba nastaafu. nikashangaa...
mie: sasa mbona wenzio wako nairobi, na wewe bado uko dar?
yeye: ni kweli wenzangu wako nairobi kwenye ziara. mie nimepewa ruhusa kupumzika na pia kufunga ramadhani. wakirejea nitajiunga nao na mtaniona stejini kama kawa...
mie: asante da'aisha. samahani kwa usumbufu
yeye: ah, bila samahani kaka yangu. ndiyo kazi...
DU? SIKU IZ FULL KUZUSHIANA IK KIZAZ CHA EPA NA RICHMOND KIMEINGIA KWA WANANCH MARA UYU KAZUSHIWA IV MWINGINE VILE YAN FULL MAJUNGU.
ReplyDeleteTANZANIA TULIPOFIKIA SIYO KUNA AJA YA WAANDISH KABLA YA KUANDIKA HABARI LAZIMA WAULIZE KWA MUHUSIKA.HONGERA MKUU WA WILAYA YA NANII KWA KUAMUA KUMUULIZA MUHUSIKA KABLA YA KUANDIKA HABARI
walianza na MwanaFA ohh kafariki leo tena Aisha kastaafu jamani hata aibu hamna kwa nini mnafanya kazi bila uangarifu na kuchapisha kitu bila kuwa na uhakika alafu majiita eti profesionals hakuna uproffessional hapo hata kidoago sio siri waandishi wahabari manaboa sana. msiwe manafikiria tu kuwa mtauza habari hebu fikirieni ni wangapi mnawaumiza na kuwasababishia matatizo na hizo habari zenu za uzushi.
ReplyDeleteIii somooo! ntoto Aisha kaumbika wajameni. Nakutakia kazi njema Aisha Madindda. kweli moja ya watu wanaonivutia kuipenda Twanga hata huku ughaibuni ni pamoja na mnenguaji aisha jinsi anavyojituma na kulimudu jukwaa. Big up sana dada.
ReplyDeletekwani kuna nini cha ajabu kama mtu akistahafu? mnategemea huyo dada ataendelea kuwakatia viuno mpaka siku atakapo ingia kaburini?.
ReplyDeleteMbega
At a risk of becoming totally irrelevant. what attracted me to this story is the picture of the DOOR,was this lady in prison when the picture was taken. I know she was not and that is what really scares me
ReplyDeleteWakatabahu