Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza na Jamhuri ya Ireland, Mheshimiwa Mwanaidi S. Maajar, akiwa na maofisa wa Ubalozi na wahusika wengine waliohudhuria hafla hiyo
Balozi Maajar akipokea mojawapo ya michango iliyotolewa Balozi Maajar akiwa na baadhi ya wageni
wageni walipata burudani nzito ya ngoma ya sindimba

Tarehe 12/09/2008 Jumuiya ya Wanadiplomasia Vijana ya London (Young Diplomats Association in London – YDL) kwa kushirikaiana na Friends of Commonwealth na Ubalozi wa Tanzania London, waliandaa hafla ya kuchangia mradi wa Pemba Panorama (Pemba Panorama Project), iliyofanyika Marlborough House, Pall Mall, London.
Mradi huo uliombwa na Zanzibar International Film Festival (ZIFF), kwa lengo la kuwasaidia kina mama wenye kipato kidogo Kisiwani Pemba. Zaidi ya watu 250 walihudhuria hafla hiyo iliyoanza saa moja na nusu jioni hadi saa sita usiku.

Katika hafla hiyo jumla ya zawadi 42 zilishindaniwa, baadhi ya zawadi hizo zilitolewa na Ubalozi wa Tanzania London, Zamani Zanzibar Hotel Kempinski , Kilimanjaro Hotel Kempinski, Breeze Beach Club & Spa, New Africa Hotel and Casino pamoja na Shirika la Ndege la Kenya Airways.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. yaani badala ya kukatika katika si bora mngeenda kubeba mabox halafu watu tupo kwenye mfungo mnatuonyesha mapaja ohhhh

    ReplyDelete
  2. Naomba kuuliza kwani kuuliza sio ujinga. Hii young diplomats association ni jumiya gani? ina malengo gani na na nani anaeweza kujiunga? na unajiunga vipi

    ReplyDelete
  3. Sindimba ya UK bwana mmmh haya ...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...