Hilo ndio gari lililotolewa na Kampuni ya Global Publishers likiwa ni zawadi ya kwanza ya wasomaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa Wikienda, Risasi, Championi, Amani na Ijumaa, kuponi za kushiriki zipo ukurasa wa pili wa magazeti hayo.
Wafanyakazi wa Global Publishers wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri Bendera (hayupo pichani) alipokuwa akiwahutubia Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Joel Nkya Bendera amewataka Watanzania kusoma magazeti yanayozalishwa na kampuni ya Global Publishers ili waweze kujinyakulia zawadi ya gari aina ya benzi na nyingine mbalimbali likiwemo gari la aina ya Mitsubishi Pajero.
Mh. Bendera aliyasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa promosheni kabambe ya Jishindie gari aina ya Benzi iliyofanyika katika ofisi za Kapuni ya Global, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa Risasi, Amani, Ijumaa Wikienda, The Bongo Sun na jarida la School & College.
"Licha ya kuwarudishia wasomaji faida, shindano hili litabadili maisha ya wasomji wenu na kwenda sambamba na maisha bora kwa kila MTANZANIA kama anavyohimiza Rais wetu mheshimiwa Jakaya Kikwete.' alisema Bendera katika promosheni hiyo itakayodumu kwa miezi sita.
habari zaidi na picha bofya hapa


Oll Raiti Studenti mm studentz. Zeriz sambadi gess wat G L O B E L mmm Global Publishers is?????
ReplyDeleteNaona hata jamaa aliegonga hilo bana nae alikua anajaribu kugesi jinsi ya kuandika Global. jamani hili janga haliwakumbi waalimu na wanafunzi tu ila hii lugha ni GLOBAL issue.
Mdau Makini Makini Sana
a.k.a wa kwenye sky.