Home
Unlabelled
dar tambarare
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kaka Mithupu, tunafahamu maana "halisi" ya tambarare. Ila, kwa barabara kama hii, tena "toleo jipya" ingelipendeza kama tungekiona kijani hapo kati badala ya.... Also, at least kwenye ardhi za wenzetu, hayo majani yanapandwa sambamba na ujenzi, so shime wana-project hizi mkisisitiza hilo kwenye contact zenu. Otherwise, kama alivyosema Mreno (aka Portuguese) Aluta Continua!!
ReplyDeletesalaam kaka ,nice work naona bongo hapo but wana ask wats the gap between the two lane for???i have been many places in this world but neva seen sucha a thing!!!wadauu hii sawa au kila kitu cha utawala huu ni bomba ata kama wamechapia???
ReplyDeleteEee bwana eh, njia ya home ndio inameremeta hivi sasa? Nimeacha ndio kwanza walikuwa wanaanza upanuzi. Imetulia hii!!
ReplyDeleteHiyo barabara ni nzurisana lakini ina tatizo moja,inakosa U-Turn.Niliona magari mengi yanakatiza kwenye kivuko cha pundamilia kurudi upande wa pili wa barabara kwa kuogopa kuendesha umbali mrefu kurudi kwenye barabara ya pili.Michuzi ulikuwa unatoka wapi?Kimanzichana nyumbani?Manake nyuma kidogo hapo ndipo kuna zile nyumba mpya za polisi.
ReplyDeletekaka umefanya jambo la maana sana kunionyesha barabara y kuelekea kwetu mbagala majmatitu ipo mkeka safi sana,nakuomba utuonyeshe ilipoishia pia na hali ya usafiri kutoka mbagala kwenda kkoo ipoje asubui twaomba photo plz.nipo uk reading
ReplyDeleteNINAVYOJUA BARABARA YA KILWA BADO INAENDELEA KUJENGWA, UJENZI BADO HAUJAISHA SIJUI WEWE TAARIFA YA UJENZI KUISHA UMEIPATA WAPI.
ReplyDeleteuzuri wa barabara ni pamoja na kutukumbuka sisi waenda kwa miguu,sijaona vivuko vya watembea kwa miguu,kwani hiyo barabara ni pana sana,inabidi wajenge flyover au sabuway ili kupunguza ajali.pia ikiwekewa uzio ili kuzuia watu kukatisha ovyo barabara.sio baada ya barabara kwisha watu wanaanza kudai matuta.
ReplyDeletewalio-plan na kujenga hii barabara, hawakuzingatia future.naamini kabisa, kwamba ni wazo la busara lisilohitaji utitiri wa degree kulitekeleza.
ReplyDeletetunahitaji barabara zenye lane zisizopungua tatu kila upande kama kweli tumedhanmiria kukomesha msongamano wa magari Dar Es Salaam.
waste of money kung'ang'ania lane mbili wakati ni wazi kuwa hazitoshi.
kwa mdau wa 7:20, hiyo nafasi hapo kati ni pana sana ili kuruhusu ujenzi wa njia maalumk ya kupita mabasi siku za usoni. Kama hujasikia bado, Dar ina mpango wa kuanzisha mfumo wa mabasi yaendayo kwa kasi (Rapid Transit System) na mabasi hayo yatakuwa na njia yake maalum ambapo magari mengine hayapiti (bus lane). Hivyo basi, barabara kuu zote zinazojengwa/kukarabatiwa sasa lazima ziweke nafasi hiyo kati. Hata Sam Nujoma ambayo ujenzi wake unaelekea ukingoni pia ina tuta kubwa katikati ambalo litakuja kuwa barabara baadae.
ReplyDeleteNalitolela naona unashangilia njia ya kwenda kwenu Ntwala (Mtwara)!!
ReplyDeleteMdau
Bongo tambarare????kata kulia au kushoto hapo uone mahandaki...mpaka viongozi wa kikoloni wakiondoka bongo ndio walipa kodi watafaidi matunda yao...
ReplyDeleteMdau Nalitolela,
ReplyDeleteKuhusu hiyo nafasi pana ya hapo katikati ni ujanja mpya wa kulinda hifadhi ya barabara. Zamani eneo la hifadhi lilikuwa linaachwa kando ya barabara kushoto na kulia ila baada ya kuona Wabongo tulivyo wepesi kuvamia maeneo hayo na baadae kuanza kulalamika bomoa bomoa ikija sasa hivi serikali ndio imekuja na ujanja mpya wa kuweka eneo la hifadhi ya barabara katikati. Hivyo kama ni kwa upanuzi kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi, au uanuzi mwingine wowote wa kawaida hapo baadae inakuwa rahisi zaidi.
//Mdau
ebwanaeeeeeeee bomba mbaya ila tunaomba hao wajenzi wasikisahau kile kipande cha barabara ya kuingia dampo la zamani pale kwa Azizi Ali .serikali pigieni chapuao kipande hicho kiunganishwe kwenye tenda hiyo kinatusumbua sana
ReplyDeleteMdau (from 4:40pm). Tunaongea kitu kimoja in a way; sababu hiyo unayoita hifadhi ya barabara ni kwa kusudio la upanuzi siku za usoni. However, in this case specifically; pamoja na ile ya Sam Nujoma... upanuzi huo pindi utakapkojua utakuwa maalumu kwa ajili ya DART (Dar Rapit Transit). ie, lane ya kati itajengwa kwa ajili ya mabasi. I can say that with 100% certainity.
ReplyDeleteHuyo mdau anayetetea hio nafasi kubwa iliokuwa wasted kati kati kwamba itakuwa ya mabasi ya kwenda kasi in future ni umbumbu mkubwa sana.sijawahi kuna lane ya mabasi peke yake inawekwa katikati ya barabara kwani ni hatari kubwa kwa abiria wakati wakushuka.lane nyingi za mabasi tu kutosababisha msongamano wa magari zinakuwa ni outside lane.hio hapo wamechemsha ni kutofikiria future nafasi kubwa sana hio imepotezwa,hata wakisema wanampango wakupanda miti ni ziro bado tunahitaji kufanya njia za kusafiri rahisi sio kujijengea tu barabara bila kutumia akili tuko 2008 sasa sio mambo ya kubomoa tena baadae
ReplyDeleteSasa hio lane ya kati itatumika kwa mabasi kwenda tu au manake haitoshi kwa yanayorudi ndio maana mmeambiwa wamechemsha.na kwanini wasingemaliza kujenga wanavyotaka sasa hivi wakati wanajua watu wanapata tabu? Kwanini wapoteza hela baadae kufanya wanachotaka? Barabara za huo usafiri mpya ziwe za pembeni sio kati kuweka pembeni itasaidia abiria kushuka na kupanda kwa usalama zaidi.
ReplyDeleteanony wa 7:19 ulichosema kuhusu lane kuwepo kati badala ya pembeni is a good point, I was suprised myself, as in the little tarvelling I have done, I always see buses on the outermost lane. Ila they had people do feasibility studies and all before they came up with plans.. maybe that was the optimal design.
ReplyDeleteKuhusu upana mdogo wa barabara it's true na mi mwenyewe nishajiuliza sana hilo swali pindi Sam Nujoma inajengwa. Well let's wait and and see how it all plays out kabla hatujaanza kuwalaumu.
PS: mdau wa 6:09 na 7:19, I was merely conveying what I know, specifically kujibu swali la mdau wa 7:20 na sijatetea. By the wau, hiv wadau huwa hatuwezi kuchangia na kukosoa bila kuitana mbumbumbu/wajinga/etc?
Mbona mambo mengine marahisi jamani.
ReplyDeleteKama wataweka lane kati kati, tatizo likowapi, si mabasi yatapita kushoto kabisa na hizo lane mbili za kati zitatumiwa na magari ya kawaida?
Au?
Na kwa kulingana na picha, hapo kati panatosha lane mbili, na panabaki kinafasi.
Road reserve yaweza kuwa popote pale aidha kati kati au pembeni. Suala la road reserve pembeni ya barabara limefeli na ni gharama kubwa kumantain kwa sababu ya kutopenda kufuata sheria. Yule anayesema kuwa wangejenga sasa, kwa kutumia nini? Ninamaanisha kwa bajeti au pesa zipi, huwa hawaamki asubuhi na kusema leo tunajenga barabara hii au ile. Mipango ya ujenzi wa barabara huchukua muda mrefu, kuna feasibility studies, kutafuta pesa za ujenzi, na kufanya makadirio ya ujenzi, hiyo ni project iliyokamili. Sasa mpaka kufikia kujenga inawezekana hata hiyo pesa iliyobajetiwa mwanzo isitoshe na mara nyingi huhusisha wafadhili pia katika kugharamia ujenzi wake ingawa siku hizi hakuna ufadhili wa 100%. Na kwa kuwa hatujazoea kufanya mipango ya siku za usoni tukiona mipango kama hiyo imepangwa huwa tunashangaa na kusema kwanini hawafanyi sasa hivi. Kila kitu kinakwenda na uwezo tulio nao sasa, mipango ya baadae na michakato itakayofanyika baadae kutafuta pesa zaidi kwa ajili ya ujenzi, sio wakati umepata pesa ya kutekeleza mipango yako unakwazwa na tatizo la kukosa eneo la kufanyia kazi kwa sababu ya uvamizi.
ReplyDelete