wachezaji wa simba wakiwa kambini, wakiwa wamekula fasheni za enzi hizo. wadau wenyekompyuta kichwani tufaeni majina wenzenu basi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mwenye nywele nyingi na mawani ya jua ni MAREHEMU MARTIN KIKWA, kutoka kulia ni OMARY HUSSEIN, huyu alichezea Yanga na Simba,wa pili toka kulia ni MACHELE- KAJOLE, ni marehemu alikufa kwa ajali ya gari. wengine sura nazifahamu majina yamenitoka.

    ReplyDelete
  2. Ndugu wadau sura sio ngeni ila ni longtime sasa najaribu kuzikumbuka,Wapili toka kulia ni Mohamed Kajole,watatu wake ni mohamedi Bakari Tall,toka upande huohuo wa kulia ni Adam Sabu kama sikosei,Wapili toka ni nadhani ni Martin Kikwa, Ezikiel Juju"Man"Jumanne Hassan Masimenti. michuzi babu wewe mchokoz sana mimi ni Yanga kandambili lakini hao jammaa nawakumbuka sana enzi hizo tulikuwa hatunywi mma, mpaka Hussein Juma mmakonde alipotung`atua kwa mara ya kwanza kuwa teja la simba wanja la Karume gaol la kusawazisha ikawa 1-1 tulikimbiza Mchaka mchaka mpaka Kaunda Stadium,tangia hapo ikawa rashid Handhuri akawa muaji wao na miaka kadhaa baadae ikaja Homa ya Jiji "Bonga Bonga" natumai hio October hawatoki,Mdau Mbegu

    ReplyDelete
  3. HAYO MASURUALI YALIKUWA YANAZIMA VIBATARI KWELI USWAHILINI.

    ReplyDelete
  4. wa pili kutoka kushoto Martin kikwa,wa mwisho pili kutoka kulia kwa omary Hussein kulia kabisa ni Mohamed kajole

    ReplyDelete
  5. Wa kwanza kulia ni Abdallah Hussein kaka yake na Omary Hussein,
    Mohamed Kajole,Athuman Juma,Mohamed Tall,Ismail Mwarabu,Aluu Ally,Martim Kikwa na huyo wa mwisho simkumbuki. Hapo yanga alikuwa akifungwa mbili anashangilia.

    ReplyDelete
  6. Nimegundua kuwa Maisha kila yakizidi ukali na nywele zinakimbia, tazama picha za vijana wa zamani wengi wana manywele lakini vijana wa leo wengi wanashindana kwa uwanja wa ndege eyapoti tupu kichwani kwenda mbele!

    ReplyDelete
  7. Michuzi kwanza thanks kwa picha kama hizo za long time. nikianzia kushoto 1 Yussuf Kaungu 2 Martin Kikwa 3 Aluu Ally 4 Ismael Mwarabu 5 Mohamed Tall 6 Athuman Juma 7Hamis Askari 8 Mohamed Kajole na wa 9 ni Abdallah hussein . nawakilisha mdau Dege Leicester Uk.

    ReplyDelete
  8. Wa pili kulia ni Martin Kikwa (late?) na wa tano toka kushoto ni Mohamed "Tall" Bakari - sentahafu ambayo mfano wake sijahawi kuona hata Rio haoni ndani...

    ReplyDelete
  9. ALIYEWAPATIA WOTE HAPO NI MDAU DEGE WA LEICESTER.Omari Hussein hajacheza Simba enzi hizo za Kikwa na Kajole.Amechezea Simba baada ya mpira kuisha kabisa na kukosa namba YANGA.

    ReplyDelete
  10. Nawashukuru wadau Mbegu, Dege nawengine, kwa haraka niliweza kumtambua TALL tu, kwa umri wangu niliwajua kikwa, Kajole na bin Juma wakiwa wakubwa zaidi, hapa kajole alikuwa kijana mno. Sasa wadau tukumbusheni zaidi, hii ilikuwa mitaa ya MWAKA GANI?

    ReplyDelete
  11. siwajui hao walio kwenye picha(ukweli) nataka kuwakosoa hawa wanaosema kwamba OMARY HUSSEIN alikuwepo kwenye picha hii.Ninavyokumbuka OMARY HUSSEIN alianza kuichezea YANGA miaka ya '80 kisha yeye na ABEID MZIBA(kama sikosei)walikimbilia UARABUNI aliporudi mwanzoni mwa miaka ya '90 akajiunga na SIMBA.Sasa ukiangalia hii picha si ya Miaka ya '90 ni kati ya miaka ya 1970-85.Mimi ni dogo wa miaka ya '80-90 sijawahi kuziona maishani zaidi ya kwenye picha(albamu) za dingi na hapa tu.

    ReplyDelete
  12. kuijua squad hiyo lazima uwe underline original.pamoja na kuwa siku zimesonga lkn kutoka kushoto,ni ezekiel greyson "jujuman."martin kikwa,abdallah mwinyimkuu"pele."ismail mwarabu,mohamed bakari "tall.'athuman juma willington mwaijibe,mohamed kajole"machela." na mwisho kulia ni filbert lubibira.hizo enzi kuala lumpar alipigwa 6-O U/TAIFA.habari ndio hiyo.

    ReplyDelete
  13. Wa pili kutoka kushoto ni Martin Kikwa, anafuata George Kulagwa, wa tano ni Mohamed Bakari Tall akifuatiwa na Adam Sabu na wa pili kutoka kulia ni Mohamed Kajole Machela.

    ReplyDelete
  14. Toka shoto.yussuph Kaungu(bruno)Martin kikwa(rip)Aluu Ally(spoiller)Simkumbuki,Mohd Bakari(tall),Athman juma,Filbert Lubibira,mohamed kajole(machela)Na Abdallah Hussein.Challa boy,Amstd

    ReplyDelete
  15. Wadau mi Dau mbegu tena, namuunga mkono mkono mdau hapo juu huyo ni Abdallah Hussein ilikuwa taabu sana kupata namba enzi hizo kwake kwani miaka hiyo Adam Saab alikuwa tishio,na kama sikosei hiyo ni miaka ya 77 na 79 nilikuwa nipo darasa la pili mechi yao nayoikumbuka wa walilala Doulla Younde ya Cameroon mabao 4 kwa Mawili, nyingine ambayo walicheza na Laka Rovers ya Nigeria mechi ambayo kijana mdogo ali-Break toka timu Marehemu Hussein Tindwa Alizimia uwanjani na hatimae kufariki kabla ya kufika Muhimbili Hospital, mdau wa Leicester upo? Data hizo isipokuwa mi Yanga Chinja, hamtoki hiyo october 25 mdau wa leicester, ha ha ha take care mchizi waaangu, habari ndo hiyo, bado nipo nipo kwanza.Mbegu Reading,UK

    ReplyDelete
  16. l to right
    Kaungu, Kikwa, Alluu Ally, pass, Tall, Athumani Juma pass ,Kajole, pass
    Hizo redio kaseti ndio zilikua bab kubwa enzi hizo watu wanacheza kavacha

    ReplyDelete
  17. Wanapendeza sana,
    Japo hayo mashati yamerudi, bado hawa wa siku hizi hawajaweza kubana 'slimfit' kama wale. Nakumbuka sana picha hizo ilikuwa hatari tupu, wakati huo hakuna vijana wanene wenye vitambi kama sasa, wote walikuwa hivyo.
    Hicho kiatu kikikukanyaga unalazwa hosp.
    Suruale ilikwa fundi anaambia pima kiuno, chini malizia kitambaa.

    ReplyDelete
  18. haloo peaple,

    mimi ni stella martin kikwa huyo mwenye nyele nyingi ni marehemu baba yangu martin kikwa nawengine wote siwajui kwaajili wakati baba yangu anacheza mpira mimi nilikua mdogo sana. lakini baba yangu alikua mchezaji mzuri sana rest in peace.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 30, 2011

    Martin Kiwka ni uncle wangu, maskini ali kufa :(

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...