Zain yafuturisha wanahabari Mwanza
Na Mwandishi Wetu
ZAIN, kampuni ya simu za mkononi yenye mtandao katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, imeendeleza programu yake ya kufuturisha katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.Safari hii, Zain imewafuturisha wanahabari wa jijini Mwanza, hafla ilizofanyika juzi usiku (Jumatano) kwenye hoteli za La Kairo jijini Mwanza.
Meneja wa Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Singano alisema hatua hiyo ya kufuturisha, ni programu iliyopangwa kufanywa na Zain katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani.
Mbali ya kuwafuturisha wanahabari, pia Zain ilitoa zawadi anuwai ya vyakula ikiwa ni pamoja na unga wa sembe, ngano, mafuta za kula, sabuni kwa watoto zatima wa kituo cha Yatima Islamic Foundation kilichopo Wilaya ya Ilemela, Mwanza.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. James Nsekela na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Salum Ferej, Meneja wa Huduma za Jamii wa Zain Tanzania, Tunu Kavishe alisema Zain itaendelea kuwajali wasiojiweza, na pia kampuni hiyo itaendelea kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
Mbali ya Tunu na Beatrice, pia Zain iliwakilishwa na Meneja Mauzo wa Zain Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya na Ofisa Biashara wa Zain Mwanza, Amani Boma.
Akizungumza katika hafla hizo, Dk. Nsekela aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Samwel Kamote, aliishukuru Zain kwa kujitolea kusaidia shughuli mblimbali ya jamii.
Naye Sheik Ferej alisema amefurahishwa na kitendo cha Zain kuendelea kujitolea kusaidia shughuli mbalimbali ya jamii, na akaiombea dua njema kwa MWenyezi Mungu ili izidi kufanikiwa katika biashara zake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...