
Asalaam Aleikum!
Kwa heshima na uadilifu, kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya waislam waishio jimbo la Massachusetts napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaalika watu wote katika hafla kabambe tunayoiandaa ya kusherehekea kumalika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan!
Sherehe hii ya Eid El Fitr itafanyika Jumamosi tarehe 4 Oktoba, 2008 katika ukumbi wa
Kabab & Curry 903 Main Street,
West Springfield,
Mass 01089-3941
simu yao namba (413) 750-3444
toka saa mbili usiku mpaka liamba.
Shughuli hii ya kifamilia (watu wazima kwa watoto) nyote mwakaribishwa na ni shughuli ya bure. Kwa niaba ya wanakamati napenda kuwakilisha!
Isaac A. Kibodya


Massage Delivered ndugu but naomba niwaulize wadau wenzangu; Hivi kusema "Kwa niaba yangu binafsi" hii imetulia kweli? Japokuwa mie Masai niliyesoma kwetu Longido naona hii ni makosa. Naomba tumsaidie huyu ndugu yetu kwa kumpa neno sahihi!! - Nasyeku!!!!
ReplyDeleteMjomba inabidi ukuwe...................................................Nasikia mkeo anakuja utakuwa hivyo mpaka lini?
ReplyDeleteHivi ndugu zangu watanzania tutaelimika lini alichokisema Mzee Kibodya hakiusiani na ujio wa mkewe wewe kama una uhasama naye tumia jukwaa lingine kutoka dukuduku lako lakini sio kutuchafulia hewa ,Nasema hivi sio kuwa nimetumwa na mzee kibodya ila ni kuchoshwa kwangu na vijitabia vya baadhi yetu ambavyo haviwakilishi desturi za utanzania wetu , upunguani na ugumu wa maisha ya mtu usiwe ndo jukwaa la kutusi wenzio kisa tuu unakwazwa na maisha magumu hapa marekani rejea kwa mola wako na kujipinda kwenye swala hakika utaonyeshwa njia iliyo nyoofu na kuepukana na vishawishi vyako vya kutusi na kejeli zisizo na msingi.
ReplyDeleteMdau wa lynn (Kiwalani)
Naunga mkono kabisa mdau wa Lynn Kiwalani, kwani habari alioituma mjomba ilikuwa nyepesi na yenye kueleweka.Wee Anonymous wa kwanza na wa pili, kwani kila liandikwalo humu lazima mlitolee comments? Nilivyoelewa mimi ni ujumbe mfupi wa shughuli ya kidini na watu wote wanakaribishwa, sasa iweje hili likahusishwa na mengine sijui kukua, mke, n.k.? Mjomba, wewe usiwajibu, haina maana. Sisi tutakuja kusherehekea sikukuu ya Idd na watoto wetu, wapuuzi wachache wasituvurugie shughuli.
ReplyDeleteMwanao mwenyewe, Mass!