



Tarehe 12/09/2008 Jumuiya ya Wanadiplomasia Vijana ya London (Young Diplomats Association in London – YDL) kwa kushirikaiana na Friends of Commonwealth na Ubalozi wa Tanzania London, waliandaa hafla ya kuchangia mradi wa Pemba Panorama (Pemba Panorama Project), iliyofanyika Marlborough House, Pall Mall, London.
Mradi huo uliombwa na Zanzibar International Film Festival (ZIFF), kwa lengo la kuwasaidia kina mama wenye kipato kidogo Kisiwani Pemba. Zaidi ya watu 250 walihudhuria hafla hiyo iliyoanza saa moja na nusu jioni hadi saa sita usiku.
Katika hafla hiyo jumla ya zawadi 42 zilishindaniwa, baadhi ya zawadi hizo zilitolewa na Ubalozi wa Tanzania London, Zamani Zanzibar Hotel Kempinski , Kilimanjaro Hotel Kempinski, Breeze Beach Club & Spa, New Africa Hotel and Casino pamoja na Shirika la Ndege la Kenya Airways.
yaani badala ya kukatika katika si bora mngeenda kubeba mabox halafu watu tupo kwenye mfungo mnatuonyesha mapaja ohhhh
ReplyDeleteNaomba kuuliza kwani kuuliza sio ujinga. Hii young diplomats association ni jumiya gani? ina malengo gani na na nani anaeweza kujiunga? na unajiunga vipi
ReplyDeleteSindimba ya UK bwana mmmh haya ...
ReplyDelete