RAIS Jakaya Mrisho Kikwete anaondoka nchini jana (Jumamosi, Septemba 20, 2008) kwenda New York, Marekani, ambako atahudhuria na kuhutubia kikao cha mwaka huu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN).

Rais amepangiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne ijayo, Septemba 23, 2008 katika nafasi yake pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Mbali na kuhutubia Baraza Kuu, Rais Kikwete amepangiwa kuhudhuria mikutano mingine muhimu kuanzia ule ambao utaangalia Mahitaji ya Maendeleo ya Afrika. Mkutano huo, utajadili ahadi za nchi tajiri kwa Afrika na Maendeleo ya Bara hilo, na kuona ahadi hizo zinatekelezwa namna gani.
Rais pia atahutubia kikao cha ufunguzi cha viongozi ambao watajadili maendeleo ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s). Baada ya kuwa amehutubia kikao hicho, Rais atashiriki katika mijadala kuhusu afya ya Mama na Mtoto, na pia mjadala kuhusu ugonjwa wa Malaria, masuala yote mawili yakiwa sehemu muhimu ya MDG’s.

Ijumaa, Septemba 26, Rais atakwenda mjini Washington, ambako atatoa hotuba muhimu ya ufunguzi kwenye Kikao cha Mwaka cha Wabunge Wenye Asili ya Afrika katika Bunge la Marekani, na pia kuhutubia mkutano wa viongozi wa shughuli za biashara katika Marekani.

Mbali na mikutano ambayo amepangiwa kuhutubia ama kushiriki, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wengi wa shughuli za kisiasa, kibiashara na kiuchumi duniani na katika Marekani.

Miongoni mwa viongozi ambao Rais Kikwete atakutana nao na kufanya mazungumzo nao ni pamoja na Rais wa Iran, Mheshimiwa Ahmedinajad; Katibu Mkuu wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Mheshimiwa Javier Solana; na mfanyabiashara maarufu duniani wa shughuli za kompyuta na teknolojia ya mawasiliano, Bill Gates.

Rais Kikwete pia atakutana na Waziri Mkuu wa Denmark, Mheshimiwa Anders Fogh Rasmussen; na Katibu Mkuu wa Shirika la Kazi Dunia (ILO), Juan Somavia.

Rais Kikwete pia atafanya kikao cha pamoja kati yake, Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki Moon na Makamu wa Rais wa Sudan, Ustaz. Ali Osman kuzungumzia mgogoro wa eneo la Darfur nchini Sudan.

Wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili katika Sudan mwanzoni mwa mwezi huu, Mwenyekiti huyo wa AU, alimwahidi Rais Omar El Bashir wa Sudan kuwa angefanya kikao kati yake, Katibu Mkuu wa UN, na mwakilishi wa Sudan kuhusu hali ya Darfur wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu.

Kikao hicho kitaangalia jinsi gani ya kuharakisha zoezi la kupeleka askari wa kulinda amani wa UN na AU katika Darfur, na pia jinsi ya kuahirisha, kwa angalau mwaka mmoja, hati ya kukamatwa kwa Rais Bashir iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uharifu (ICC).
Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Duh...kusema kweli rais wetu ana millage nyingi. Hasa kwa rais wa nchi masikini jamani...hii ni hatari sasa. Si alikuwa Marekani juzi...Sudan...leo tena karudi Marekani. Alafu hapo hasafiri mwenyewe. Wote wasafirio naye ni first class na bado accommodation costs. Kudadeki...
    Wananchi tungepewa makadirio ya fedha zinazotumika kwa safiri za rais.
    Wadau mnaonaje?
    Michuzi usinibanie hii...maana najua na wewe katika hizi safari unapata kuangaza angaza macho kama mwandishi wa gazeti la serikali.

    mtoto

    ReplyDelete
  2. MWEMWE RAIS ANARUKA STATE TENA

    ReplyDelete
  3. Sasa nyinyi mmnaojifanya kulalamika muonekane mna uchungu, kwani JK kule anaenda likizo au kikazi kama Rais na Mwenyekiti wa AU?--Nyinyi mlitakaje? Kama hamna cha kusema sio lazima m-comment!

    ReplyDelete
  4. It's high time now viongozi wa Africa wajifunze kutulia nyumbani na kusukuma gurudumu la maendeleo internally.Wa-SA walianza kumchukia Mbeki kwa style hii hii ya kitalii...Nadhani hii ni impact ya kuzoea kuwa waziri wa mambo ya nje.

    ReplyDelete
  5. Mimi mpaka leo sijamuelewa huyu raisi wetu ana agenda gani na marekani na husasan raisi Bush? Wametokea kuwa maswahiba sana tangu raisi wetu aingie madarakani, kulikoni!

    ReplyDelete
  6. acheni zengwe wabongo,huyu jamaa ana kofia nyingine kama mwenyekiti wa Afrika,msiangalie bongo tu..fungueni macho..

    ReplyDelete
  7. PS
    Mpe salam zetu Barrak Obama mwambie twamtakia kila la kheri na twamuombea mafanikio kwenye uchuguzi ujao. Pia mwambie kuwa vurugu hilo likiisha twamkaribisha bongo aje kula nasi ubwabwa na uduvi na samaki wa kupaka
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  8. vijana wa it mvidioconferensing mzee safari sio nzuri kwa afya

    ReplyDelete
  9. mimi nataka nikupe ukweli wewe unaejiita mtoto kama akili zako zilivyo hivi kama wewe una uchungu na nchi yako kwa nini usirudi kijijini kwenu kutumikia huko... kazi yako ni ku cretisize kila wakati kuhusu nchi yako huna lolote hebu elewa mambo kwanza inaelekea hujui kama trip nyingine za rais JK zinagharamiwa na AU Organization rais Kikwete ni mwenyekiti wa AU so trip zingine zinakuwa ni one of his responsibility as a chairman of AU.Na hiyo trip alioenda USA mwanzoni mwa mwezi huu ni mualiko rasmi kutoka kwa bush kwa hiyo nafikiri unaelewa kama mtu akikualika kwake kawaida huwa yeye ndie gharama itamuangukia ni si mualikwa keep that in mind.

    ReplyDelete
  10. if he is going to USA...TO MEET BILL GATES,AHMADINEJAN AND ALL THOSE STUPID PEOPLES LIKE HIM...SO WHATT?WHAT DOES IT HAS TO DO WITH US??

    ReplyDelete
  11. JK bado anafikiri yeye ndiye waziri wa mambo ya nchi za nje, kazi ambayo ninafikiri anaimudu vizuri sana kuliko urais. Membe yuko wapi? enzi za mwalimu jkn hivi vijisafari na vimialiko vingine alikuwa akimtuma Malicela, na hakuna lililoharibika. sana sana utaratibu huo unasaidia kumjenga waziri kidiplomasia, kisiasa, kijina, na kuwa na moyo wa kujiamini kama tulivyomuona jk mwenyewe na malicela!!!!

    ReplyDelete
  12. hehehe...mimi napenda watu wenye hasira sana. Anon wa September 21, 2008 5:01 PM, nani kakwambia kuwa sipo kijijini nalima? Au una-make conclusion tu kabla ya kuuliza?
    Mimi nimeuliza mnaonaje? Sasa wewe umejibu fresh kusema kuwa safari nyingine zina gharamiwa na AU au mwaliko. Lakini unakumbuka mambo ya ubalozi wa South Africa na issue za nyumba za nanii, kulipwa mshahara na bunge la AU, nk. Sihitaji kutaja mengi hapo uelewe...nadhani kama unafuatilia habari utakuwa unafahamu.
    Swali ni sisi wananchi tuna unauhakika gani hakuna double charging ya hivi vi-trip? Mimi napenda ukweli na uwazi. Mkinitukana sawa...mkichangia sawa.
    Hela ni zetu walipa kodi. Sio haki yetu kujua matumizi ya Rais?


    mtoto

    ReplyDelete
  13. Baba yetu anatusahau. Huyu ndio kama wale wababa wanaotelekeza watoto wao nyumbani na kusafiri kila siku kikazi. Before they know watoto wamekua wakubwa na matabia yao hayafai.

    Kwani kuwa AU ndio kila kukicha ni safari tu????? Kwani ni yeye wa kwanza kuipata hiyo post?

    Tuongee ukweli too much is too much. Ameshavunja record huyu kijana kwa kusafiri nje ya nchi.

    ReplyDelete
  14. TULIMPIGIA KURA WENYEWE. TUKAE KIMYA.

    WENGINE WANACHOTA KWAKUFANYA BIASHARA NA WENGINE WANACHOTA KWA KUTANUA TU.

    MIMI NILIONDOKA TZ BAADA YA KUPIGA KURA SIJARUDI TENA LAKINI JE MLIOKO HUKO TUPENI FEEDBACK BASI? NATAKIWA KURUDI NYUMBANI JUNE JE NIRUDI AU NITAFUTE KIBIBI HUKU?

    ReplyDelete
  15. Mwacheni rais afanye kazi zake.

    ReplyDelete
  16. Hata akikaa hapa nyumbani atafanya kazi gani?Mwacheni asafiri.Ningependa kumkumbusha kwamba bado hajaenda Australia,Alaska,Mongolia,Bolivia,Iceland na kama 2010 itakuwa bado basi akumbuke kwenda na Antarctica tukafungue Ubalozi kule!Jamani Urais wa Afrika ni kuzurura dunia nzima!Ukirudi unaanza kupiga stori aisee nimekuta maghorofa huko siyo mchezo manaake,jumba linapotelea hewani kupita mawingu kabisa sijui wanajengaje majumba yale jamani!Halafu unasema tutakuja wapita maendeleo,subutu!Sisi tubakie kuomba tu yalla maskini basi!Labda vitukuu wetu,inshallah!Siku mie nikifika New Zealand,nitawaalika timu yao ya Rugby nasikia wazuri kweeeeli! Kipanya Upo?

    ReplyDelete
  17. kwikwikwiii,,tehteh
    ila annon wa 5.01 MUONGO MKUBWA USIZUGE WATU,,double-payments za trip zipo kijana,,waweza jilipa uku na kule walipwa teh teh teeeh tunaijua sana hii wee acha tu

    ReplyDelete
  18. wadau wa New Zealand tupo bwana tunafuatilia blogu. Waziri mkubwa alikuja huku 2007 kabla ya kujinyatua kutoka kwenye post. Timi ya rugby ni noma...wakifungwa ni kilio nchi nzima. Ni sawa na brazil kwenye soka...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...