JK: Misaada kwa Afrika ni wajibu, siyo hisani

Na Mwandishi Maalum, New York, Marekani

Bara la Afrika limeziambia nchi tajiri duniani kuwa hatua zozote za kuongeza raslimali zake kwa maendeleo ya Bara hilo siyo hisani, bali ni wajibu wa kihistoria na ulazima wa kiroho kwa nchi hizo kufanya hivyo.

Bara hilo pia limesema kuwa ni jambo la kukatisha taama kuwa nchi hizo tajiri zimeshindwa, mpaka sasa, kuheshimu wala kutimiza wajibu wao katika kutoa fedha zinazohitajika kuliwezesha Bara hilo kutekeleza kikamilifu Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s).

Msimamo huo wa Afrika umetolewa leo (Jumatatu, Septemba 22, 2008) na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa Viongozi wa Juu Kuhusu Mahitaji ya Mandeleo ya Afrika unaofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, Marekani.

“Nataka kuchukua nafasi hii kuelezea masikitiko ya Afrika juu ya kushindwa kwa nchi tajiri kuheshimu ahadi zake za kutoa raslimali za kupambana na changamoto za maendeleo za Afrika,” amesema Mwenyekiti huyo wa AU na kuongeza:
“Niruhusu nitumia nafasi hii leo kutoa mwito kwa nchi tajiri kuongeza kasi katika kutimiza malengo yao. Huu ni wajibu wao wa kihistoria, ni ulazima wao wa kiroho kusaidia wahitaji wa misaada katika Afrika. Hii siyo hisani.”

Pamoja na msimamo huo, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Afrika inaelewa na kuheshimu sana hatua kadhaa zilizochukuliwa katika miaka ya karibuni kupambana na changamoto za mahitaji ya maendeleo ya Afrika.

“Hatua hizo zinajionyesha dhahiri katika maamuzi ya 2006 World Summit Outcome, 2005 Paris Daclaration on Aid Effectiveness, na Azimio la 2005 la G-8 Gleneagles Summit Declaration,” amesema Rais na kusisitiza:

“Pia tunazishukuru nchi tajiri na zenye viwanda vingi zaidi duniani za G-8 kwa kuongeza mwelekeo wao na uelewa wao kwa masuala ya maendeleo yanayoathiri Afrika.”

Hata hivyo, Rais Kikwete ameongeza kuwa pamoja na juhudi hizo zote na makubaliano ya Moterrey Concensus ya 2002, bado wasiwasi unaongezeka katika Afrika juu ya kuongezeka kwa pengo kati ya nini kimeahidiwa na kiasi gani hasa kimetolewa kwa ajili ya maendeleo ya Afrika.

Amesema kuwa, kwa pamoja, nchi tajiri ziko mbali kabisa na lengo lao la misaada waliyoahidi kutoa kwa Afrika.

Amesisitiza: “ Kwa pamoja , G-8 ziko mbali kabisa katika utekelezaji wa ahadi zao za kutoa misaada ya maendeleo kwa Afrika. Naambiwa kuwa, kwa jumla, misaada ya G-8 kwa Afrika chini ya Jangwa la Sahara imeongezeka kwa dola bilioni 2.3 tokea mwaka 2004, wakati misaada hiyo ilitakiwa kuongezeka kwa kiasi cha dola bilioni 5.4 kwa
kipindi hicho hicho.”

Rais Kikwete amesema kuwa kama hali hiyo itaendelea, Afrika haitakuwa na uwezo wa kupata raslimali zinazotakiwa kugharimia uwekezaji katika shughuli za umma ambao ni muhimu kuweza kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. missada si wajibu. wajibu ni usawa na haki kwa wote. Ombaomba hufa maskini na mtegemea cha nduguye hufa maskini. Kidumu CCM

    ReplyDelete
  2. matonya nae afundishe practical poverty vyuo vikuu kama prof dr J alivyotabiri. REPOA inabidi mumkabizi hicho kitengo matonya msituhadae hapo mlalakuwa

    ReplyDelete
  3. Ndo maana mnalegeza vichwa vyenu mkisubiri wajibu wa kihistoria uwaleteeni maendeleo, misaada ni hiari yao kutoa kwa Afrika si lazima na wala si wajibu wao, walikuja Afrika kutafuta maendeleo yao, nasi inatubidi tuende kokote kutafuta maendeleo yetu, kama walitafuta kwa sera mbaya hiyo ni kitu ingine kabisa lakini isigeuzwe kuwa ni wajibu wao kuturudishia kwa njia ya misaada, sisi wenyewe tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii, na kuwa na usawa, haki na fusa sawa kwa wote duniani wa watu kwenda wanakotaka kutafuta maendeleo ilimradi wana uwezo wa kufanya hivyo na hawafunji sheria za sehemu husika, kusiwe na ukiritimba wa watu kuzuwiwa kwenda watakako kutafuta maendeleo iwe ndani ya nchi au nje ya nchi, isiwe rahisi kwa watu wa nje kuja kwetu na vigumu sisi kwenda kwao au isiwe rahisi kwa watu wa mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine na wa mkoa mwingine kuwa vigumu kwenda kwingine, freedom of movement should be both ways, na tututmia rasili mali zetu vizuri ambazo wazungu walizijia na kuwapatia mitaji ya maendeleo waliyoyafikia nchini mwao.

    ReplyDelete
  4. Misaada si wajibu ni hiyari ikishakuwa kuwa ni wajibu na ni lazima then hiyo si misaada tena inabidi tutafute msamiati mwingine.

    Me nadhani wajibu ni kulinda ralisilimali zetu na kuhakikisha kuwa zinawanufanisha walio wengi ni si kikundi kidogo cha wachache wateule. Rasilimali tulizo nazo ni nyingi kiasi zikitumika vizuri kwa faida ya wengi hatutahitaji hiyo misaada hata tukihitaji ni kwa kuongezea tu kidogo. Lakini sasa mambo ni kinyume misaada ni number moja kwa ajili ya maendeleo, hayo mengine baadaye matokeo yake tunauza uhuru wetu kama nchi na kama bara. Kinachonimua zaidi ni kwamba kizazi hiki hakitalipa sana gharama ya mentality hiyo bali vizazi vinavyofuata ambavyo tunaviua kabisa kwa kuvifanya tegemezi-Mungu tusaidie jamani.

    ReplyDelete
  5. Kidumu CCM,
    Nafurahi kuona wengi hawaungi mkono suala la 'Misaada ni Wajibu'. Hii ni bishara tosha ya ukomavu wa akili na uzoefu wa watu wetu. Mmarekani au Mwingereza na wengineo watakupa msaada gani wa kukuondoa katika umasikini? Wanachukua vya bure kila uchao ati wakupe msaada? Na msaada upi huo unaotaka? Pesa? Mbona tutauza nchi kwa dola na paundi ndogo tu? Teknolojia na sayansi? Thubutu! Hakupi hiyo Mmarekani au Mwingereza. hakupi ng'o. Elimu? wapi na wapi. Ujue nini anakifanya ili uje umgeuke? Nayo hakupi ya bure. Afya? Madawa au kuwasomesha madaktari? Hizo ni ndoto. Akikuhurumia atasomesha watano kwa mwaka nao ni wengi tena kwa masharti kedekede. Uhandisi? Nani akupe ujuzi wa kujijengea dalaja na barabara na kuunda mitambo yako mwenyewe? Unataka viwanda vyake afunge eti akupe wewe misaada? Fani ni nyingi ukianzia na uandishi, uuguzi hadi uganga wa mifungo na ubwana shamba. Nakwambieni kwa uwazi kabisaaaa tena dhahiri shahiri kuwa misaada ya namna hii hata siku moja Mmarekani na wenzake hawakupi.

    Kubwa hapa ni kuirudia historia na kuwarudia na kuwakumbatia marafiki wetu wa kweli, Warusi na Wachina. Angalia matharani kada ya udaktari na uhandisi, Ni nchi gani ilijitolea kwa kiwango kikubwa kuwafundisha madaktari, wahandisi na waandishi,wachumi na wazee wa propaganda bila kumsahau kamaradi Kingunge kama Urusi? Jibu ni Hakuna. Na mpaka sasa wasomesha watu wengi mamia kwa mamia tena bure. Ukiongea na hao ndio watakusaidia kuleta maendeleo ya kweli na si wamarekani.

    Bila Urusi Msumbiji, Angola, Zimbabwe, Namibia na hata Afrika Kusini zingekuwa bado ni makoloni.

    Hivi mbona mnasahau haraka historia? Mambo hayajabadilika. Mchezo mchafu uko pale pale akudanganye mtu na biashara huria. Utauza nini marekani bwana? Konyagi? Na sisi tunapiga makofi. Hiki mbona ni kichekesho. Utajenga uchumi gani kwa Konyagi? Wamarekani na wenzao bado sera zao ni kunyonya tu. Ni kuendeleza ukoloni tu. Ni Kuidumaza Afrika tu na tukumbuke kuwa Afrika dumavu ndiyo faraja ya hawa wakubwa. Wanaishi kirahisi kwa kuidumaza na kuibia Afrika. Huo ndio ukweli na huo ndio ubeberu haswaaa. Wataiba kirahisi. Watatupa mikataba mibovu mfano ile ya madini asilimia tatu. Watatupa sera mbovu za uchumi mfano Structural Adjustment Programme (SAP). Hivi kweli haya yote mmeyasahu kweli? Hivi kweli hamuoni? Au...

    Njia mbadala za kuleta maendeleo yetu ni nyingi. Hadi mara nyingine.
    Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

    ReplyDelete
  6. Hivi hotuba ya mheshimiwa ilikuwa kwenye kiswahili ama mwandishi ameitafsiri kutoka kiingereza kwenda kiswahili. Maana nashindwa kabisa kushawishika na maneno haya.

    Mtambalizi.

    ReplyDelete
  7. misaada haiwezi kua wajibu
    huwezimlazimisha mtu akusaidie etı kwakua weye maskını ni hıyari yake kufanya hivyo

    na hata hıyo mısaada hua inaishia mikononi mwa viongozi si kwa manufaa ya umma.

    kama kweli kikwete ana uchungu na umma si ombaomba bali tuna rasilimali tele zikipata usimamizi mzuri basi tutajiinua wenyewe.

    kuombaomba ni kudumisha ukolonı mambo leo(neocolonialism) tumeachiwa huru lkn bado tunataka tawaliwa.
    so what is independent means?

    ReplyDelete
  8. Anon, 9:15am, uko wapi ndugu yangu? kama ungekuwa una position ofisi ya raisi au foreign affairs ndugu yangu si ingekuwa vizuri? kama uko nje rudi basi nyumbani ndugu yangu ili sera kama zako zipate action.

    ReplyDelete
  9. Hii kali maana hata hao 'watoa misaada' walikuwa wanasinzia kusikiliza hotuba iliyokosa vina vya hoja ya umasikini wetu.

    Nchi za Afrika zinahitaji kuwa na access za kuuza bidhaa zao huko Marekani, Ulaya bila vikwazo vya so-called international standards.

    Bidhaa zetu za kilimo ni organic kweli kweli na hazina madhara kwa walaji kama maziwa ya China au Nestle au NIDO.

    Tupiganie kwa ari, kasi na nguvu mpya ili 'Turuhusiwe' na mataifa haya manyoyanji watoa 'misaada' kusindika bidhaa zetu kama kahawa,matunda,tumbaku, pamba, dhahabu, tanzanite, hapa hapa Tanzania au afrika, na kuziuza bidhaa zilizosindikwa huko Ulaya kama kahawa ya kopo,Juice za kopo, Sigara,nguo na bangili/mikufu/vito vya dhahabu na tanzanite, badala ya kuwauzia malighafi kwa bei ya chini mno.

    Kama tuliweza kuchongana kungarisha almasi hapo TANCUT Iringa sioni tunashindwaje kutengeneza vito kamili vya tanzanite na vya dhahabu Bongo na kuviuza kama kinamama huko ulaya badala ya walanguzi wa De Beers London na Brussels.

    Hotuba, hoja na mikakati ya namna hiyo ndiyo itatukwamua toka katika umasikini wa kufa mtu.

    Rocky
    London

    ReplyDelete
  10. Mimi nafikiri haina maana kuwalazimsha watu weupe watupatie misaada wakati makapu ya kuhifadhia misaada yote tunayopewa yametoboka. Nchi hazitaendelea kwa misaada bali ni kwa matumizi sahihi ya kile walichonacho, hata kama ni kodogo. Kwa hiyo basi Misaada si lazima bali kuwapokonywa mafisadi utajiri wa nchi ndiyo lazima kama kweli tunataka maendeleo

    ReplyDelete
  11. Hii ni kali ya kufunga mwaka 2008. Ati misaada kwa Afrika au Tanzania ni lazima na si hisani. Rais wetu alisoma uchumi chuo kikuu na hakuna hata lecture moja, na hakika, alipofundishwa kuwa uchumi wa nchi hujengwa kwa misaada! Kama kuna washauri wake napendekeza wasome kitabu cha Kishpre Mahbubani kiitwacho " The new Asian Hemisphere". Kwa kifupi maendeleo ya ustaarabu wa kizungu si exportable kwani kila sehemu walikokwenda kama wakoloni au walowezi hakuna hata sehemu moja ambapo wakazi asilia waliendelea kama wao. Misaada ni dumavu. Tuige Japani baada ya vita ya pili au China sasa ambapo wanapeleka vijana wao wengi kusoma nje bila vikwazo kwa matumaini ya kati yao watarejea kuijenga nchi yao. Hili limelipa licha ya wachache walioamua kutorejea!
    Misaada ingelipa Tanzania tungekuwa mbali toka enzi za Nyerere, kwa sas tumekuwa kama bottomless pit, ambapo kila pesa iingiayo hupotea bila kuleta faida kwetu zaidi ya watoaji.
    Misaada kama ilivyo sasa ni biashara kwa mtoaji kwani huleta ajira kwa wananchi wao na kuongeza uzalishaji kwenye viwanda vyao. Kwa kila dola 1 itolewayo kuna direct and indirect return ya up to 30cts yaani faida ya 30%. Ikipunguahapo misaada hukatwa. Kma ni misaada nini tutakacho? Umati visima vya maji zungumza kuhusu kujenga njia za uchumi halafu ona nani atakupa 'msaada'. Wengi wetu tunakumbuka ilivyokuwa taabu kupata mkopo kujenga reli ya Tazara, kuboresha reli ya kati miaka ya sabini/themanini. Mtizamo wa Wazungu bado uko palepale " the war of cultures with only one axis"!
    Rais wetu na wapambe wake mnatuangusha, kama bado hatujafa, watanzania na waafrika kwa jumla kwa mitizamo isiyojenga bali kudumaza.

    ReplyDelete
  12. Hata siku moja misaada inayotoka kwa hizi nchi zilizo endelea huwa haiji kwa nia njema. Misaada hii inaimaliza na itaendelea kuimaliza Africa. Hawa watu (i.e. Developed Countries) hawatupendi sisi watu weusi na haitakuja kutokea wakatupenda hata siku moja..... hata historia inajionyesha.

    Leo nitatoa mfano mmoja tu wa msaada uliopitia sector ya afya ambao umetumaliza na unaendelea kutumaliza wa-Africa..... achilia mbali misaada inayopitia sector ya uchumi (labda nitakuja kutoa mifano na madhara yake siku nikichokozwa kama nilivyochokozwa na hii mada).

    United States iliunda programme maalumu kwa ajili ya kutengeneza AIDS virus. Lengo lao kuu ilikuwa ni kuua watu weusi na walipata support kutoka kwenye mataifa makubwa kama Russia, German, Britain, France, Canada na Japan. Plot hiyo ilifanikiwa na US waliweza ku-attach AIDS kama compliment kwenye misaada ya kinga za Small Pox iliyotumwa kuja Africa mnamo miaka ya 1970s..... mwenye akili pekee ndio ataye elewa nilicho andika hapo juu.

    Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kupitia Website ya mpiganaji Dr. Boyd Ed Graves (www.boydgraves.com) ambaye ameifikisha serikali ya US mahakamani akiitaka ibatilishe maamuzi yake ili kuokoa maisha ya weusi walio wengi, asilimia kubwa ikiwa kutoka Africa.

    Haya ni baadhi tu ya mambo yaliyopo kwenye Website...... ‘‘Dr. Boyd Ed Graves simply brought a government document (1971 AIDS Flow Chart) to court…... and demanded an investigation. The government knows well what is in that document and that it was not meant for public consumption….. His accusations are not made lightly or out of bitterness….. He is a patriotic American….. everything he has told me is verifiable in government document libraries.’’ Dr. Vincent Gammil, Chemist, 08th August 1999
    In 1971, Progress Report #8 is issued. The flowchart (pg. 61) will forever resolve the true laboratory birth origin of AIDS. Eventually the Special Virus program will issue 15 reports and over 20,000 scientific papers. The flowchart links every scientific paper, medical experiment and U.S. contract. The flowchart would remain “missing” until 1999. World scientists were stunned. The flowchart will gain in significance throughout the 21st Century. It is also clear the experiments conducted under Phase IV-A of the flowcharts is our best route to better therapy and treatment for people living with HIV/AIDS. The first sixty pages of progress report #8 of the Special Virus program proved conclusively the specific goal of the program. By June 1977, the Special Virus program had produced 15, 000 gallons of AIDS. The AIDS virus was attached as complement to vaccines sent to Africa and Manhattan. However, because of the thoroughness of authors, like Dr. Robert E. Lee, we also learn the Stanford Mycoplasma Laboratory issues one of the first papers with AIDS in the title. “Viral Infections in Man Associated with Acquired Immunological Deficiency States.” The primary scientist, Dr. Thomas Merigan, was a “consultant” to the Special Virus program.

    In 1976, the United States issues Progress Report #13 of the Special Virus program. The report proves the United States had various international agreements with the Russians, Germans, British, French, Canadians and Japanese. The plot to kill Black people has wide international support. In March, the Special Virus began production of the AIDS virus, by June 1977; the program will have produced 15,000 gallons of AIDS. President Jimmy Carter allows for the continuation of the secret plan to cull the Black Population.

    In 1977, Dr. Robert Gallo and the top Soviet Scientists meet to discuss the proliferation of the 15,000 gallons of AIDS. They attach AIDS as complement to the Small pox vaccine for Africa, and the “experimental” hepatitis B vaccine for Manhattan. According to authors June Goodfield and Alan Cantwell, it is Batch #751 that was administered in New York to thousands of innocent people. This government will never be able to repay the people for the social rape, humiliation and out right prejudice people with HIV/AIDS face on a daily basis. The men in the shadows of the AIDS curtain accurately calculated that you would not care if only Blacks and gays are dying. In fact you don’t care that nearly a half million Gulf War veterans are encumbered with something contagious. Soon there will be no more Black people and a confused military, older White people will start suddenly dying and you still won’t get it. Be here now for us, give us a chance to be there for you.

    HIVYO NARUDIA TENA..... MISAADA YA HAWA WENZETU SI MIZURI MAANA INA LENGO LA KUTUMALIZA SISI WA-AFRICA. HAWA WATU HAWATUPENDI, NA MTU KAMA HAKUPENDI TOKA LINI AKAKUPA MSAADA KWA NIA NJEMA?

    HABARI NDO' HIYO

    ReplyDelete
  13. Huu ni UMATONYA katika kiwango cha juu kabisa kulazimisha misaada. Na nchi kamwe haitaendelea kutegemea misaada kwani kama wengine walivyosema misaaada huwa haitolewi kwa nia ya kukuendeleza. Kwa kuanzia nchi yetu ina historia kuuubwa ya corruption ambapo mafisadi kwa kiasi kikubwa wameturudisha nyuma. Badala ya kupiga mbita yafuatayo yanatakiwa.
    1. Kitangazwe kifo cha mafisadi, zero tolerance inapokuja rushwa na corruption in the system. Fweza zirejeshwe na watu waende jela
    2. Kodi ikusanywe kama inavyotakiwa kwani ndio source kubwa ya government revenue, no excuse.
    3. Export more than we import. Kuvitia nguvu viwanda vya nyumbani. Omo, blueband, colgate, nguo za kuvaa etc. encourage small business kwa mikopo ya bei nafuu.
    4. Kuboresha huduma za jamii. Kuanzia barabara mpaka hospitali. Serekali inakimbilia kutibu watu India and South, Nairobi why not improve Muhimbili, KCMC etc?
    5. Encorage kilimo cha kisasa, umwagiliaji, mbolea, matractor, with mazao ya chakula na biashara yanayoeleweka. Mkonge na pareto haviuziki tena. Pia ufugaji na uvuvi
    6. Kutumia vizuri rasilimali kuongeza kipato cha serekali including natural resources kama madini na utalii.
    Haya ni machache na hii kitu inawezekana sema inahitaji discpline, Angalia mfano Uchina. Mheshimiwa raisi alianza vizuri ma kama angefanya kweli na mafisadi we could start seeing a light at the end of the tunnel.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...