mkongwe wa muziki nchini zahir ally zorro akitoa tafuu kwa mwanae banana na bendi yake ya B Band kwenye mnuso mmoja hivi usiku wa kuamkia leo ukumbi wa diamond jubilee hall. baba na mwana hao wanatikisa anga kwa kibao chao cha 'nzera' ambacho kimeshika chati zote kwa sasa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Mkuu wa wilaya ya nanii mbona unatuchanganya na kiswanglish chako "ukumbi wa Diamond jubilee Hall". Lakini kuhusu picha B Band wametulia kinoma.

    ReplyDelete
  2. Mimi nahoji mbona huyu mzee (Zahir)huwa anapenda kuvaa tofauti na wanaband wengine? Hata kwenye Video ya nzela alikuwa tofauti kabisa na wenzake au hataki kujionyesha sawa na mtoto wake? ona hapo kapiga suti nyekundu wengine wote nyeupe. sijamsoma kabisa wadau. ni mtazamo tu.

    ReplyDelete
  3. Jamani kwani si waislamu hawa? hawajafunga?

    ReplyDelete
  4. Anon wa 12:23Pm
    kwani mtu akifunga ndio haruhusiwi kufanya kazi. Basi tungeshuhudia waislamu wote wakikaa nyumbani tu mwezi huu mtukufu wasiende kazini. Sijui na hiyo futari watashushiwa na malaika.

    Hao kazi yao ni muziki kama ilivyo yako inayokuwezesha mkono kwenda kinywani n.k

    ReplyDelete
  5. wewe anony wa tarehe 18 12.23pm hapo juu kwani kufunga nini.ndo usifanye kazi? atakula nini asipofanya kazi? badilika usiwe na mawazo mgando.au wewe mtoto wa kulelewa? kwa taarifa yako hata huyo anayekulea anafanya kazi hata muda huu!

    ReplyDelete
  6. Nauliza swali ikiwa Kaka yako ni daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama ( gynnaecologist) na huu ni mwezi mtukufu anakaa nyumbani eee?

    ReplyDelete
  7. Hebu hawa wanaoendelea kupiga kelele kuwa kuimba hii ni kazi wakae kitako niwafahamishe kidogo. Kidini, yaani dini ya kiisilamu inakataza mtu kufanya kazi ya aina hii, iwe ramadhani au mfungo mosi, muisilamu hatakiwi kufanya kazi hii period.

    kuna kazi nyengine pia zimekatazwa lakini watu waisilamu wanafanya, hilo ni kosa, sasa waisilamu wengine ni wajibu wao kuwakumbusha wenziwao. Tatizo ni kuwa kwa nini hawaasi wenzao miezi mingine?

    kwa ufupi kama wewe ni muisilamu na unaamini allah, mtume na kitabu chake basi hutofanya kazi hizi, hutouliza oh sasa nipate shibe wapi, ila utatafuta kazi nyingine yeyote ile inayokubalika na dini yako ufanye.

    La kama wewe ni muisilamu jina na hujali dini yako basi ni wewe na mola wako, ila ni wajibu waisilamu kukumbushana.

    KUMBUKA:
    UISILAMU SIO MWEZI WA RAMADHANI TU NI MIEZI YOTE 12 YA KILA MWAKA!!! kwa hiyo makumbusho yawe kila siku

    ReplyDelete
  8. Anon wa 6:52 PM

    Asalaam aleykum.

    Unajui uzuri wa uislam ni kwamba kila kitu kimeandika katika kitabu kitukufu cha Qur'an. Sasa naomba unipe ni aya gani inayokataza kufanya kazi ya kuimba na inaelekeza kazi za kufanya.

    Mi naona wewe utakuwa unaendeshwa na hisia tu kwani hata kuandika dini yako unakose eti "UISILAMU" hii ndiyo dini gani?. Umepitia madrassa wewe?. Tusidanganyane hapa.Uislam haujaharamisha muziki hata kidogo, hebu nieleze "DUFU" sio muziki?.

    Matendo yako wewe unayoyafanya kama ni kukatika viuno hadharani yanaweza kuchukuliwa kuwa si utamaduni katika uislamu. lakini hebu jiulize Baba na Mwana wakipiga Music wanamlazimisha akacheze?.

    Mfungo mwema.

    ReplyDelete
  9. Waambieni hao wamezidi,kwa hiyo, Wanamuziki,Wanaofanya kazi kampuni za bia, sigara, baa, majumba ya starehe,wanaouza vinguo vya kina dada vimin,vitopu topu,na wanaofanya maduka yanayouza baadhi ya vitu nyeti,maduka ya vyakula ambako nako kunauza baadhi ya vilevi, au kama alivyosema ndg kazi zingine zenye vikwezo dr,policia,NA KADHARIKA AMBAO NI WAISLAM HUWA INAKUWAJE???!!!! Tafadhali jamani.....

    ReplyDelete
  10. Anony wa September 18,2008. 6:52PM wewe naona hizo ni hisia zako tu, hiyo hao vijana ni kazi kama kazi zingine na hamna sehemu yoyote ile ya kitabu kitukufu cha ki-islam kinachokataza music mbona kuna dufu tena ukienda nchi za uarabuni dufu yao ni ya music babu kubwa pia huko huko uarabuni uislam umetoka kuna bendi za mziki wa kiduni kama hizi za vijana wetu hapo nyumbani Tanzania tena nyingi tu, kuna mabaa ya pombe,kumbi za sinema za ngono, watu wanavuta bangi, cocane, rushwa, wizi, prositution kama kazi na vitu kama sema havifanyika wazi kwama huko kwetu au Ulaya kwa vile wanogopa watu kama nyie ambao mnaweza kuwapiga mawe na kuwauwa kwa kusingizia uislam, tembea uone mambo ukienda nchi za uarabuni na kuwaona utajiuliza huu uislam wetu ulitokea wapi? nenda hapo karibu Misri UTAJIONEA MWENYE NI KAMA EUROPE. mambo mengine yayofuatwa na watu ni utamaduni tu si dini sawa na kuita balakashia na kanzu ni vazi la ki-islam si kweli hayo ni mavazi ya mashariki ya kati ni utamaduni wao awe mkristo au mu-isla au hana dini hilo ni vazi lao, wanavaa nguo nyupe kwa vile kuna jua na joto kalinguo nyeupe uakisi jua na barakashia ni kujikinga kichwa kwa jua kali. afaghanista ni nchi ya ki-islam lakini ni nchi inayoongoza kwa kuuza raw material ya madawa ya kulevya duniani (pope maua mekundo ya kutengenezea heroin), Pakistan ni nchi ya ki-islam inaongoza kwa madawa ya kulevya, watanzania wote wanaokamatwa na madawa ya kulevya hutokea Pakistan, hata serikali ya talaban iliyoangushwa pato laki kubwa la serikali lilikuwa linatokana na heroin na ilikuwa serikali ya ki-islam. huko Uarabuni watu wanaenda kazini kama kawaida, kazi ni kazi tu bwana tuko huko Ulaya tunafanya kazi na waislam safi toka IRAN, MISRI, SAUDI ARABIA, IRAQ, PAKISTAN, DUBAI, KUWAIT QATAR, AFAGHASTAN katika kiwanda cha kuchinja na kuitengeneza nyama ya nguruwe na ukiwauliza kwa nini wanashika nguruwe wanakuambia hii ni kazi anahitaji pesa kuishi.

    ReplyDelete
  11. Kwa mara ya mwisho kabisa naandika kuhusu issue hii na sitendela nayo kwani kuna watu wengine humu vichwa vyao vina maji na ubishi ni hulka yao,. pia kuna ambao hata sio waisilamu na hawajui lolote kuhusu dini hii wanaleta points za kiajabu ajabu.

    kwanza kuna aon wa sept 18 7:53alonikosoa eti hakuna dini uisilamu! duhh hayo ni mambo, lugha ni ngumu na kwa vile mie si mjuzi wa lugha sitosema sana, lakini katika kiswahili mara nyingi watu hutumia "i" na sijui ni kwa nini lakin sioni kuwa hilo ni kosa la kufika kumwita uislamu mwenzio (kama wewe kweli ni muislamu) anaendeshwa na hisia tu mfano wa maneno ya haraka haraka tu ni

    Qur-an Qur-ani
    Injil Injili
    Jibril Jibrili
    Islam Isilamu
    Ahmed Ahmedi
    Salum Salim
    fikra fikira
    bikra bikira

    Ama kuhusu mimi kwenda madrassa, well sijui madrassa ni nini na sijaenda lakini nimeenda chuoni ambapo nimefunzwa Qur-an, sheria na hulka za kiislamu.

    Muziki unasema sio haramu, una point hapo kwa angle fulani,lakini yanayokwenda na performance za hao wana muziki jee? kwanza kuna nyumba wanazofanya show zao kunakuwepo ulevi, na mchanganyiko wa wanaume na wanawake wakicheza kiufuska kabisa. Sasa kama wewe ni muislamu basi unajuwa fika nini dini yako inasema kuhusu kufanya maasi na kumsaidia mtu kufanya maasi, au kumfanyia wepesi mtu kufanya maasi yake. Huwezi kufunguwa bar halafu ukasema siwalazimishi kunywa kwa hivyo sina makosa.

    Sentensi yako ya mwisho inaonyesha kiasi gani upeo wako ni mdogo, sasa labda nigeuze suali lako na kukuuliza hivi; kweli hawawalazimishi watu kucheza lakini je si wanacheza kwa sababu kuna anaepiga huo muziki hapo? usipopigwa muziki watacheza? jawabu ni hapana. Ndio maana muislamu hatakiwi kupiga muziki waachieni wasio waisilamu. Unaposema nikupe aya inayosema muziki ni haramu jawabu ni sina, ila nitakushauri usome vitabu vya sheria na ufahamu undani sio kusoma kama hadithi za elfu layla ulayla.

    ama anon wa sept 18 11:55 point yako ni mbovu sana, wewe ni kama watu wengi tu wanadhani kuwa waarabu ndio waislamu kweli kweli na kila wafanyalo ni according to islamu! WRONG!!! dini ya kiislamu si ya waarabu kama ilivyo ukristo sio ya mzungu, uislamu ni dini ya umma wote, mwarabu nae pia hufanya makosa tena makosa mengi. hata ndani ya qur-an imesemwa "al arab ashadu minal kufra" waarabu ni wafanyaji wakubwa wa kufuru.

    ReplyDelete
  12. Dini ya Ki-islam ni ya WA-ARABU ndio walioineza dunia nzima na dini ya Ki-kkristo ni ya WA-YAHUDI hii haina ubishi kabisa, sisi wengine tumeletewa tu kwa namna moja au nyingine, EBU FIKIRIA KAMA WASINGEKUJA SISI TUSINGEKUWA WA-KRISTO AU WA-ISLAM. KWANI KUNA SEHEMU HAPA DUNIANI HAWA WATU HAWAKWENDA NA HAKUNA DINI HIZI, NI KAMA ZA UMMA NA ZA MUNGU KWA NINI SEHEMU HIZI HAZINA DINI HIZI, ACHA MAWAZO YA UKALE. utaniuliza wapi? nenda katika misitu ya AMAZON Brazil kuna watu hawa dini hizi wanadini zao za jadi tu.

    ReplyDelete
  13. anon wa sept 20 2008 1:07 point mbovu kabisa, umeshindwa hata kufahmu kilichosemwa, sasa labda nikupe mfano mdogo uweze kukusaidia na akili yako finyu. ikiwa unafanya kazi zain na moja ya wajibu wako ni kuitangaza zain jee utasema zain ni ya kwako? sijui uyahudi ila uislamu ulifikishwa kwa hao waarabu na kutakiwa kuitangaza na kuisambaza dunia nzima, hawakuambiwa kama hii ni yao kwa mantiki kuwa "it belongs to them" ila ni dini ya walimwengu wote! bisha, kataa au usikubaliane nami lakini huo ndio ukweli.

    ReplyDelete
  14. Acha kupokea mambo ki-ukale nani kakuambia dini zilifikishwa kwa wao ili wazisambaze, zilitokea wapi? dini ni ubunifu tu wa-waanzilishi hamna ushahidi wowote unaoweza kuonyesha zilitoka wapi! na kama walitumwa kuzisambaza, which I don't believe in it, kwa nini bado hawajasambaza sehemu zingine za dunia, na kama dini inatoka kwa huyo unayemhisi aliwatuma wasambaze sasa kwa nini alete dini nyingi na asilete dini moja tu kwa wanadunia wote? dini ni ubunifu wa-waanzilishi na si vinginevyo, pia mfano wako wa ZAIN na dini ni ufinyu wa mawazo yako wala haufanani, and even though I could argue as on the other side I can say it is true that all the employees of a certain firm (including ZAIN) are the owners of that firm as they have a stake on it, ni wadau, stakeholders, wanafanya kazi kwa niaba ya mwenye firm, hivyo ni yao, kama umesoma economics na business utakubaliana nami, ni kwamba biashara inaanzishwa na mtu mmoja na pale inapokuwa anatafuta watu wamsaidie, (as he can't do it alone anymore), kwa niaba yake, nadhani wewe ukiwa meneja utaua shirika kwa vile unadhani si lako na hilo ndo lilotokea kwa mashirika ya umma ya Tanzania yalikufa kwa vile wafanyakazi hawakuyaona kama ni yao na wakakalia kuiba tu na yakafa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...