Habari yako,
Ninapenda kukukaribisha UtuExchange (
http://www.utuexchange.com/static/sw/Home.htm ).

UtuExchange ni tovuti inayoendeshwa kwa mfumo wa masoko ya mistaji, lakini badala ya kifanyia biashara makampuni, tunafanyia biashara kuagua matukio ya huko baadaye.

Ni rahisi. Unawekeza kwenye matukio ambayo unadhani yanauwezekano mkubwa wa kutokea. Unafanya hivyo kwa kununua vipande (shares) za matukio hayo. Kama matukio hayo yakitokea, unatengeneza faida. Yasipotokea, unapoteza mataji wako.

Kwa hiyo, jinsi ambavyo wewe unaagua matukio ya baadaye vizuri, ndivyo faida yako inaongezeka.

Unaweza kutumia faida uliyotengeneza kuchukulia Tuzo mbali mbali. Tuzo kubwa kubwa tu zitakuwa zinpigwa mnada mara kwa mara. Na zawadi hizo zinaenda kwa wanaoweka zabuni za juu. Kwa hiyo, tena, jinsi ambavyo unatengeneza faida kubwa ukilinganisha na wengine, ndiyo inakuwa rahisi kwako kujinyakulia zawadi hizo.

Najua unachofikiria. Ni bure kabisa. Kwa hiyo haupotezi kitu. Unashinda tu, iwapo unaweza kuagua mtukio ya baadaye sawa-sawa.

Bofya kwenye kiungo hiki hapa chini na ujiunge
na
UtuExchange SASA HIVI!
http:/www.utuexchange.com/

Tunatumaini tutakuona hapo UtuExchange.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mh. Balozi na Mkuu wa wilaya ya nanihii, mie sijaelewa hawa wadau wa 'utuexchange' wanaongelea nini hasa.

    Maana kuagua manake inaweza kuwa ni kusafisha nyota yako ya matukio ya baadaye, mimi ndivyo nilivyoelewa.

    Na pia hiyo faida ni faida gani unayoipata?! Hebu wadau wa Utuexchange mtufahamishe mnaongelea kitu gani hasa????

    kama mmefanya tafsiri ya neno kwa neno toka lugha nyingine, basi bora mtoe tangazo ktk lugha hiyo, kama ni kiingereza muandike hivyo.

    ReplyDelete
  2. Neno lingine lenye maana ya kuagua ni kubashiri.

    Naomba nisahihishwe, lakini nadhani neno "agua" halihusiani na kusafisha nyota mwanawane. Ni kwamba tu imetokea wasafisha nyota "wanaweza" kubashiri mambo yako yatakayo tokea baadaye.

    Kitu tunachoongelea hapa ni kwamba UtuExchange inakupa fursa ya kutoa maoni yako lakini kwa mtindo tofauti kidogo; Kwa mtindo wa masoko ya mitaji.

    Kwenye masoko ya mitaji biashara ni kuuza na kununua vipande vya makampuni. Unanunua vipande ambavyo unadhani bei yake ya sasa ni ndogo kuliko thamani yake halisi, na hivyo unadhani kwamba bei ya vipande itaenda juu baadaye na hivyo utakuwa umetengeneza faida. Ikitokea bei yake ikaenda kweli juu, basi unakuwa umepata faida. Ikitokea imeenda chini, tofauti na ulivyo fikiria, basi wenyewe wanasema inakuwa imekula kwako. Kwa hiyo, ukiifikiria vizuri, bei ya vipande vya makampuni katika masoko ya mitaji huwa inaendana na maoni ya washikadau kuhusu ufanisi wa kampuni husika.

    UtuExchange inafanya kazi kwa mfumo huo huo. Ila badala ya kufanyia biashara vipande vya makampuni, tunafanyia biashara mtukio ya baadaye.

    Chukulia kila tukio au dai linalowekwa pale kama kampuni ambayo inakuwa na vipande (wangereza wanaita shares ama securities nadhani).

    Kwa mfano mtu anaweza akadai kwamba:
    Zombe atahukumiwa kwenda jela kesi yake itakapofikia tamati.

    Kabla kesi haijaisha, wadau wanaruhusiwa kuuza na kununua vipande vya dai hili.

    Mwisho wa kesi, ikitokea dai hilo likawa kweli, kila kipande kitakuwa na thamani ya 100U. (U ndio fedha yetu mule ndani, sio fedha halisi).

    Kwa hiyi kama ulinunua kipande kwa 20U, basi unakuwa umetengeneza faida ya 80U (100 toa 20).

    Hiyo ndiyo jinsi moja ya kutengeneza faida.

    Ikitokea Zombe akaachiwa huru, basi thamani ya vipande vya dai hilo inakuwa ni sifuri. Maana yake kama ulinunua kipande kwa 20U, unakuwa umepata hasara ya 20U.

    Hatimaye, ni wazi kwamba watakaoweza kutengeneza faida zaidi ni wale wanaoweza kubashiri mambo sawasawa kwa kununua vipande vya matukio ambayo yanakuja kutokea.

    Unaweza ukajiuliza kwamba baaada ya kutengeneza faida kibao na kuongoza, halafu nini sasa?

    Kuatakuwa na zawadi za kumwaga. Zitakuwa zinanadiwa. Na unaweza kutumia U's zako kuweka zabuni. Anayeweka zabuni ya juu ndio anajichukulia zawadi.

    Samahani kwa kuweka maelezo marefu mno, lakini natumaini hiyo imekupa mwanga angalau kidogo muheshimiwa [anonymous].

    ReplyDelete
  3. Kwa nini unawaeleza watu kwa kuzunguka hivyo hawataelewa, wewe sema ni BETTING, KAMA VILE WANAVYOFANYA BOOKMAKERS, NI aina fulani ya KAMALI ni mchezo wa kubahatisha, kwa mfano unaweza kutabili Match ya Manchester United na Liverpool ikichezwa Liverpool watafunga magoli 3 kwa 2 na goli la kwanza la Manchester United litafungwa na ROONEY kama itatokea hivyo basi mtabiri sahihi atapewa shilling 5000 kwa mfano lakini unapotabiri unanunua tiketi sema kwa shs 1000. and mind you huu utabiri unakuwa umwpangwa na bookmaker mwenyewe wewe unachagua tu utabiri gani unahisi unaweza kutokea ndo unalipa hiyo shs 1000 na kusubiri matokeo yakitokea kama ulvyochagua utapata hizo shs5000. na utakuwa umetengeza shs 4000. hivyo vitu vinafanyika sana huku Ulaya

    ReplyDelete
  4. Sadakta [Anonymous]!

    Ndio kabisa ni kama kamari hivi.

    Ila hapa kuna tofauti kadhaa kidogo.

    Moja, hakuna bookmarker. Bei ya kipande inategemea na demand na supply. Yaani wewe mwenye kipande ndio unaamua unauza kwa kiasi gani, na anayetaka kununua anasema yuko tayari kununua kiasi gani. Biashara inafanyika automatically pale anayeuza na anayenunu bei wanazotaja zinaendana.

    Pili, kamari kama uliyotaja mara nyingi zinafanyika kwenye matukio ambayo kweli kabisa ni ya kubahatisha. UtuExchange itakuwa na matukio kama hayo, lakini lengo nikuwa na matukio ambayo mwenye information zaidi ndiye anakuwa ana advantage. Kwa hiyo lengo letu ni kwamba skill na ujuzi wa mtu ndio umfaidishe na sio pata-potea.

    Tatu, hatutumii fedha halisi. Kwahiyo huna cha kupoteza. Ila ukiwa mzuri sana kuna kutakuwa kuna tuzo kwako.

    Mfumo kama huu huwa unaitwa "Prediction Markets" ( http://en.wikipedia.org/wiki/Prediction_Markets ). Na lengo sio kwamba watu wacheze kamari tu. La hasha. Lengo nikukusanya maoni kwa kutumia busara ya makundi ( http://en.wikipedia.org/wiki/The_Wisdom_of_Crowds ).

    Asenti.

    ReplyDelete
  5. Hey, BETTING is illegal in Tanzanian.

    Hairuhusiwi kisheria, je unataka kufungwa weye?

    Na unataka sisi washiriki tufungwe pia?

    Hebu nenda kwa Tarimba Abbas pale Harbour View Towers ukaombe kibali kwanza, kisha weka tamko rasmi kwamba una leseni ya kufanya betting.

    ReplyDelete
  6. Afadhali umeuliza muheshimiwa. Inaonekani wewe ni mfuatiliaji wa mambo.

    The Gaming Act, 2003 (Hii ni sheria ya michezo ya bahati-nasibu), ina-define "gaming activities" vizuri na inasema it does not include games in which, naomba ninukuhu, "no person makes money
    for operating the game", mwisho wa kunukuhu.

    UtuExchange does not make money out of the game. Tunachotaka ni kuruhusu watu kutoa maoni kwa njia tofauti kidogo, ambapo mtu anaweza kuzawadiwa kama maoni aliyotoa ni sahihi, na anaweza kuwajibishwa kiaina flani kama maoni aliyotoa kama haya.

    Kwa hiyo karibu, na usisite kujichukulia zawadi kwa kuogopa kuvunja sheria.

    UtuExchange hutumii fedha. Wala hutoi hata shilingi. Ni njia yako tu ya kutoa maoni yako. Currency ya U tunayotumia pale ni kama points tu unapocheza michezo mingine.

    Ila tu hatimaye unaweza kuzitumia kujinyakulia zawadi. Kwamfano sasa hivi kuna zawadi ya 100,000TZS nzima imekaa tu inasubiri mjuaji mmoja ajichukulia.

    Karibu sana UtuExchange.

    PS: Hatujakushukuru mzee misoup. Asante kwa kuwajulisha wadau hii kitu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...