Zain yakusanya dola za Marekani 4.49 bilioni kugharamia kutanuka zaidi
Zain Group, kampuni inayoongoza ya mawasiliano Afrika na Mashariki ya Kati imetangaza kwamba imekusanya dola za Marekani 4.49 billioni na kuongeza mtaji baada ya asilimia 99 ya wenye hisa kulipia hisa zao za nyongeza. Pesa zilizokusanywa zitatumika kugharamia programu yake kabambe ya kujitanua zaidi.
Kiasi cha fedha kilichopatikana kimevunja rekodi ya mauzo ya hisa katika historia ya Kuwait na kimevuka malengo, licha ya mwelekeo wa kusuasua wa hivi karibuni katika masoko ya kimataifa ambawo ulisababisha kushuka kwa bei ya mafuta pamoja na kuporomoka kwa masoko ya mitaji duniani kote.

"Kukamilika kwa mafanikio makubwa zoezi la kuongeza mtaji wa biashara wa Zain, ongezeko ambalo limevunja rekodi ya historia ya Kuwait ni ishara dhahiri kwamba wenye hisa wana imani na timu ya menejimenti ya Zain, utendaji wetu kufikia sasa na mkakati wetu wa kupanuka zaidi kufikia lengo la kuwa moja kati ya makampuni 10 yanayoongoza duniani ifikapo 2011,’’ alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dr Saad Al Barrak, na kuongeza kwamba “Pesa zilizopatikana zitatumika kugharamia mipango ya Zain ya kujitanua zaidi na kufikia malengo ya kifedha,”.
Zain imeweza kufikia hatua ya maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano katika kipindi cha miaka mitano na kuweza kunua huduma zake katika nchi 22 katika mabara mawili; Afrika na Mashariki ya Kati, ikihudumia zaidi ya wateja hai milioni 50.
Kila mwenye hisa wa Zain aliyesajiliwa hadi March 10, 2008, siku kampuni ilipokuwa na Mkutano Mkuu wa dharura alikuwa na haki ya kununua hisa za nyongeza zinazolingana na ongezeko la asilimia 75 ya idadi ya hisa walizokuwa nazo katika tarehe hiyo.
Bei ya hisa kwa ajili ya kuongeza mtaji ilikuwa dola za marekani US$3.20 kwa kila hisa moja na siku ya kulipia hisa ilianza Agosti 17 na mwisho ilikuwa Septemba 18, 2008.
“Vigezo vyote vya kifedha vya Zain sasa vinaonyesha ongezeko la kasi la kupanuka kwa Zain kutokana na miradi iliyopangwa ya kupanuka zaidi katika masoko ya Africa na Mashariki ya Kati. Tunatarajia uwekezaji huu utachangia kuongezeka kwa mapato na faida ya kampuni,’’ alisema Dk. Al Barrak.
Benki ya Taifa ya Kuwait (NBK) kupitia matawi yake ya ndani na nje ya nchi ndio benki iliyokuwa ikiuza hisa hizo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...