Hayati Castory Mpogole

Kwa dhati kabisa kwa niaba ya Familia ya Mpogole, ndugu na jamaa wote tunatoa shukrani zetu kwenu nyote mlioshiriki kwa njia moja au nyingine katika kufanikisha kusafirisha mwili wa Marehemu ndugu yetu Castory Mpogole.
Msaada wenu kwetu umekuwa wa umuhimu usio na kifani. Hivyo basi hatuna budi kuwashukuru kwa fadhila kubwa mliotutendea.
Aidha tunawashukuru sana kuweza kuchangia gharama zote za kusafirisha mwili wa marehemu hadi nyumbani Tanzania. Huu ni msaada usio kifani kwetu tunasema tena

ASANTENI SANA.
Marehemu Castory Mpogole alizikwa tarehe 20/08/2008 katika makaburi ya familia kwenye kijiji cha Nzivi, tarafa ya Nyololo, Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Kwa yote hayo mliyoyafanya ili kufanikisha utaratibu mzima wa mazishi ya marehemu ndugu yetu, sisi kama ndugu tunakuombeeni Baraka nyingi zenye fanaka na mafanikio mema katika shughuli zenu za kila siku.
Sisi tulimpenda Castory lakini Mungu alimpenda zaidi.

CHRISTOPHER J. MASASI
KAKA WA MAREHEMU
NA KWA NIABA YA WAFIWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. R.I.P Castory

    ReplyDelete
  2. Poleni sana, mimi nilisoma tosamaganga miaka ya 1980, huyu alikuwa na undungu wowote na aliyekuwa headmaster wetu wakati huu, hayati Mzee Mpogole? baada ya hapo bw. christoper masasi unaweza nisaidi kama unayo contact ya bwana mmoja alisoma pale tosamaganga anaitwa Chesco Mfikwa, mi naitwa Mazengo Kasilati, email: mazengo@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. jamani ndugu yangu
    hazina ya pekee hii kwa sie wanyalu imetutoka.
    Bwana ametoa,,,ametwaa jina lake lihimidiwe
    wa-kuboma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...