Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mh. Omar Yussuf Mzee, akipokea misahafu kwa ajili ya vyuo vya Kuran vya Wilaya ya Mjini kutoka kwa Mkuu wa Taasisi ya Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba, kwa ajili ya watoto wa vyuo hivyo wakati wa futari iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Jamatini Kidutani, Unguja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani inakuwaje Mambo ya serikali na DINI vinachanganywa namna hii?? Kama ni mambo ya futari na madrassa ni lazima awe waziri? si hayo mambo yafanywe na viongozi wa dini? au ndo serikali imekuwa ya kidini siku hizi?? maana hata juzi mh. balozi wa uk alifanya hayo hayo. Nadhani hata kama mkuu wa nchi ni wa dini hiyo ni vema kujaribu kutenganisha mambo ya siasa na dini. Otherwise?? watu wanaanza kujiuliza kunani??

    ReplyDelete
  2. mwinyi naona ubena comment yangu ya kuhusu kutmia dini kutangazia biashara.mie nashukuru kuona umeibana kwani inamaanisha hilo tendo si sawa.na nilikwambia kwamba yale ni maoni yangu binafsi ndio maana nilitaka kujua kutoka kwa wadau kwamba ni sawa au sio.kwa vile ubenania inaonekana si sawa.
    Mdau mzawa libeneke oyeeeeeeeeeee, bwawa la maini ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  3. Mboni hamuulizi kunani wakati whaeshimiwa wanapokwenda kuchangisha harambee makanisani au kwenda kuhudhuria sherehe za kusimikwa maaskofu? Mbona hamuulizi kunani wakati maaskofu na makadinali wanapotoa matamko ya kwa wanasiasa, au hiyo siyo dini au dini hiyo ina mamlaka juu ya dini nyingine? Au hiyo dini inaruhusiwa mbona kuna balozi wa Vatican hapo Dar na hamuhoji kunani? Ila linapokuja suala la kuona mabaibui, vibaragashia na misahafu ndio mnakuwa sensitive na suala la dini na serikali? Niendelee nisiendelee? Ngoja niachie wengine waendelee lakini ningendelea kuchambua zaidi hapo ningeonyesha jinsi huyo anony anayeuliza kuhusu dini na viongozi waserakali alivyo na aina fulani ya upofu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...