Safari ya tiba ya mpiganaji Athumani Hamis imekwiva.
Kutokana na umbali mrefu wa safari ya kwenda India katika mazingira aliyonayo mpiganaji huyo, serikali imefanya mabadiliko ya safari yake na sasa ataenda kutibiwa Afrika Kusini na huenda safari ikawa Alhamisi.

Kampuni yake anayofanyia kazi,TSN, imeanza pilikapilika za kufanikisha safari hiyo kwa kuchukua nyaraka muhimu na kuomba nafasi ya usafiri maalum kwa mgonjwa wa aina yake.

Viti sita vinatakiwa kuondolewa katika ndege ili kupisha kitanda maalum ambacho itamwezesha kuendelea kuwa katika utulivu katika safari hiyo.

Wizara ya Afya imeeleza kuwa tayari imeshaanza kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania kufanikisha zoezi zima la kumfikisha Athumani kwa tiba.

Habari nyingine zinasema kwamba watu kadhaa ambao walionyesha kutaka kutimiza ahadi zakufanikisha safari hiyo wameshaanza kuwasiliana na TSN kutekeleza ahadi hizo. Tayari kampuni ya Vodacom imeshakata tiketi mbili kwa ajili ya wasindikizaji wa ziada wa mgonjwa safari itapowadia, pamoja na bakshishi za kujikimu wakiwa huko sauzi.

Athumani Hamisi alipata majeraha katika maeneo ya shingo na mgongo akielekea Kilwakikazi ambako Vodacom walikuwa wanafuturisha.

Wenzake wawili,mpiganaji mmojakutoka habari Corporatin na Channel ten walipona katika ajali hiyo ambayo gari walilokuwa wakisafiria limeharibika vibaya na huenda lisitumike tena.
Hali ya mgonjwa kwa sasa ni ya kuridhisha, anakula na kuongea na hata kutaniana na marafiki zake, japo amepooza mauongo yote tokea kifuani kwenda chini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. pamoja na kuua watanzania wengi bado mnapeleka wagonjwa? mbona India matibabu ni rahisi.

    ReplyDelete
  2. BRO UKIPONA INABIDI UFUNGE NDOA KABISA NA HUYU BINTI, MAANA YUKO VERY FRONT LINE

    ReplyDelete
  3. wewe hapo juu kwani ujaelewa maelezo india safari ndefu masikini mungu mpe nguvu apone kaka wa watu inauma sana

    ReplyDelete
  4. angalia mshikaji hao wasoza si watu tena. wasije wakakumalizia

    ReplyDelete
  5. kwa kweli kupeleka watu huko sauzi ni hatari unajuaje hao manesi au hata hao madaktari kama nao wana akili mbaya mtafutieni mgonjwa mahala papofaa sio huko sauzi wendawazimu watupu wako huko

    ReplyDelete
  6. Pole zake mdau.
    Kwa bahati mbaya nimewahi kupata kuwa na jamaa waliopatab matatizo kama ya kwake kama mara tatu hivi. Na nimeshiriki katika kuwasindikiza. Tatizo kubwa ambalo ningeomba niwashtue waasindikizaji ni kwamba Vile vitanda (Hasa vya MOI) huwa havitoshi kuingia kwenye mlango wa ndege. Ni vikubwa kidogo( nimeshuhudia hivi Kwenye SWISSAIR, KQ na Pia SAA nadhani). Na kwa kuwa mgonjwa hatakiwi kutingishwa au kusumbuliwa huwa inakua kazi kubwa katika kumuingiza. Iliwahi kutubidi safari moja kumuingiza mgonjwa kwa kutumia shuka(kwa kweli ni mauimivu makubwa saana alipata). nashauri waliangalia hili (yeyote muhusika) kabla ya kwenda kupaata simanzi airport.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...