Mtoto Samuel Nkya na chini ni kamati ya kuandaa safari yake ya matiabu India. Toka shoto ni Athumani Hamisi, Baba yake Mzee Nkya, Mwenyekiti wa kamati David Sawe na Balozi wa Zain
Nakuandikia kukujulisha kuwa safari ya mtoto Samuel uliyemwangaikia sana ni leo saa 8:10 kwa kutumia ndege ya Qatar toka DSM kupitia Doha hadi Mumbai.

Vyombo vya habari vya ITV,Guardian,TSN na Blog ya Michuzi vitakuwepo Airport saa 6:00 ili kupokea neno la shukurani na kuagana na mwanetu.


Aidha pamoja na salaam hiyo, ninaungana nanyi kumwobea mwenzetu Athumani Hamisi aendelee kupona na kupata afya njema.

Narejea kuwashukuru sana kwa kazi kubwa mliyoifanya.Nawiwa kuwaomba radhi kwa usumbufu au vikwazo vyovyote katika harakati zote za kukusanya misaada ya mtoto huyu. Mimi kama mwanadamu mwingine yeyote sikamiliki.

Nitaendelea kuwasiliana nanyi moja kwa moja kutoka hospitali ya Workhardt Mumbai kuwapa taarifa za muhimu
Nawatakia afya njema na kila la heri siku zote..
Emanuel Nkya
Safarini Mumbai

Habari kamili ya mtoto Samuel inapatikana kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nilifikiri wa kwanza kushoto ni Rashid - au labda kabadili jina na kuitwa Athumani Khamis...

    ReplyDelete
  2. KWAKO KAKA MICHUZI, HABARI YA MTOTO SAMUEL NILIIONAGS HUMU, INASIKITISHA ILA SIKUIFUATILIA ZAIDI..LEO KUKUTA HABARI YA SAFARI YA MUMBAI,KWAKWELI IMENIGUSA SANA,SINA LA KUSEMA ILA KWA UFUPI NASEMA..
    MUHIDIN ISSA MICHUZI, MWENYEZI MUNGU AKULIPIE SAWASAWA NA MATENDO YAKO,UBINADAMU MLIOMFANYIA HUYU MTOTO, MWENYEWE MUNGU NDO ATAKULIPA/ATAKULIPENI.
    MUNGU MBARIKI MTOTO SAMUEL, MATIBABU YAENDE SALAMA NA ARUDI TUMUONE TENA KWENYE HII BLOG.
    Mdau,
    Scandinavia.

    ReplyDelete
  3. Inshallah Mungu amwongeze katika katibabu yake kwa uwezo wa Allah yeye ndio mweza wa kila kitu tuzidi kumwombea.

    Katochi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...