kikosi cha timu y pan african ambayo inasemekana ilikuwa ni kikosi bora kuliko vyote nchini kutokana na ukweli kwamba kiliundwa na wachezaji chipukizi waliopikwa na kupikika chini ya kocha victor stancelaus ambaye alianza kuwafundisha wakiwa chini ya umri wa miaka 12. na walipochanganyika n wakongwe kama kina abdulrahman juma, omar kapera na kitwana manara, mambo yalikuwa balaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kitwana .Abdulrahmani Juma na Omar Kapera hawajawahi kuchezea Pan wacha uzushi au hujui historia ya Pan Africa.

    ReplyDelete
  2. Michu, Hapa umekosea! Hapa bado walikuwa Yanga na hii ilikuwa ni mechi ya kirafiki iliyokuwa imejumlisha wazee na watoto wa Yanga. Ndio maana kuna kina Zito Kiaratu, Omar Kapera, Muhidin Fadhil, Abdulrahman Juma 'Linkman' ambaye hakupata kuchezea Pan hata mechi moja, Adolf Rishard, Mohamed Mkweche, Mohamed Yahya 'Tostao' na kadhalika. Nawakilisha.

    ReplyDelete
  3. Nakumbuka kulikuwa na mgogoro Yanga African na baadhi ya wachezaji walihamia PAN AFRICAN, na wengine walienda kucheza kwenye timu ya MOROGORO, nimesahau kidogo ni kama MSETO au MORO UNITED, na kama sikosei PAN AFRICAN ilianzishwa baada ya mgogoro huo, lakini picha hii ni YANGA si PAN

    ReplyDelete
  4. kitwana, sunday, na kassim, wote waliwahi kuchezea Pan African.

    ReplyDelete
  5. Michu hii sio Yanga wala sio Pan hii ni NYOTA AFRICAN ya Morogoro baada ya yanga kugawanyika 1977 kabla haijaundwa Pan mwaka 1978 waliotoka Yanga wote walienda Nyota ya morogoro na picha hii ni ya fainali ya kombe la Ofuma ambalo Nyota ifungwa bao 2-1 na simba mdau James Holland

    ReplyDelete
  6. HII NI YANGA..... NA SIO NYOTA AFRICA WALA PANYA AFRICAN.
    MDAU UK

    ReplyDelete
  7. Toka kushoto.Boi wickens,Juma pondamali(mensah),zito,adolph,adam juma(rip)kapera(rwambo),jaffar,mkweche,muhidin.Mstari wambele.Godian,moshi(dayan)Tostao,Kitwana Manara(bapo)Leonald Chitete,Kassim Manara,Abrahman Juma(Capt)Na Muhaji muki.Ilikua Yanga,Sio Pan.

    ReplyDelete
  8. challaboy kapatia majina ya wote, pia hii ilikuwa yanga takribani 1974 baada ya kushinda nyamagana,utaona waliokuwa wanapoteza nafasi zao wamevaa zile jezi za yanga za nyamagana,hii ilikuwa mechi ya kirafiki ndio maana humuoni sunday manara au gibson sembuli, ukiona vijana adolp,pondamali,kassim tostao,mkweche,gordian walikuwa wanaonekana chipukizi bado, wajina wangu zitto kiaratu inaonekana amenenepa vibaya ndio maana alinyang'anywa namba na leodgar tenga, anyway challaboy hongera una kumbukumbu nzuri.

    ReplyDelete
  9. blah blah blah!!!
    sasa which is which??talk something tuelewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...