mwina kaduguda, maarufu kama 'simba wa yuda' , katibu mkuu wa simba aliyesimamishwa uongozi miezi kadhaa iliyopita, amerejeshwa kwenye kiti chake katika mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika leo hapa dar. simba huyu wa yuda amerejea ulingoni wakati simba ikiwa inafanya vibaya katika ligi kuu ya bara kwa kufungwa mara mbili mfululizo na jana kutoka sare

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. jamaa na mzimia sana kama tulivyo waafika tumelaaniwa kuharibiana ndio maana umasikini wetu ni wamilele

    ReplyDelete
  2. Ni aibu kubwa kwa klabu kubwa kama simba wamekutana na kuongelea suala la kaduguda badala ya kuongelea maendeleo ya timu ambayo yanatia mashaka ktk ligi inayoendelea. Hapakuwa na tuhuma yoyote ila viongozi waliamua kumsimamisha kwa kutowaunga mkono ktk masuala mbali mbali na hii inatokana na tofauti ya elimu kati yake na viongozi waliobaki. Wana simba baada ya jana kutotatua tatizo la ligi mtegemee hali mbaya zaidi ktk ligi inayoendelea.

    ReplyDelete
  3. Huo mkutano ulichemka sana badala ya kukaa kuzungumzia mustakabali wa ushiriki mbovu wa Simba kwenye ligi kuu, wanaongeza matatizo.... sasa ushindi wa Simba kwenye mechi zilizobaki utakuwa ni droo

    ReplyDelete
  4. Nyie simba mimi siyo mpenzi wa klabu yenu ila nawashauri mkae meza moja mmalize matatizo yenu.Mambo ya kiongozi mmoja kujiona anafaa au anafahamu kuliko mwenzake acheni.Kati ya tabia lukuki za kiongozi mzuri ni yule anayesema "sisi" badala ya "mimi".Hapo simba nadhani kuna baadhi ya viongozi wanajiona bora kuliko wenzao.Wachezaji mnao wazuri,benchi la ufundi zuri.Simba ikilegalega,soka letu kwa ujumla litalegalega.

    ReplyDelete
  5. HATA KAMA SIMBA TUTAMLETA SKOLARI KUJA INOA TIMU YETU, BADO HATUTAFANIKIWA HATA KIDOGO. TATIZO NI KUWA KOCHA HAPEWI NAFASI YA KUONESHA UJUZI WAKE, LA MAANA MIMI NAONA NI VEMA KAMA KUNA KOCHA MGENI, BASI WASIWEPO HAO AKINA JULIO KWENYE BENCHI, SINA MAANA YA KUMPONDA JULIO ILA MAJUNGU YA MAKOCHA WETU WA KIZALENDO NDG ZANGUNI NDO YANAKWAMISHA SOKA LETU. HAWATAPENDA KOCHA WA KIGENI AONEKANE AMEFANYA VIZURI ZAIDI YAO. NAAPA KABISA, KAMA MAXIMO ANGELETWA NA TFF LEO ANGESHAONDOKA, ILA KWA KUWA KALETWA NA MKUU MAKOCHA WAZAWA WANASHINDWA JINSI YA KUMPIGA VITA. LAZIMA TUELEWE YA KUWA HAKUNA ULIMI USOPENDA KITAMU KWA HIYO MAKOCHA WAZAWA WASINGEPENDA KITUMBUA CHAO KIINGIE MCHANGA.KUMRADHI KAMA NIMEGUSA HISIA MBAYA KWA YEYOTE YULE.

    MDAU UGHAIBUNI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...