kikosi cha simba abacho inasemekana kilikuwa bora katika historia ya wana msimbazi. kwa sasa simba wanasuasua kwenye ligi kuu, wakiwa wamekosa ushindi katika mechi tatu mfululizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Bwana michuzi nikimuona huyo gabacholi aliyesimama mstari wa nyuma nasikia hasira za kufa mtu!!! huyo jamaa ndie alipeperusha kombe la CAF kwa kula dili na Mohamed Mwameja.Ilikuwa awape wachezeji wote magari.akaomba kibali apate exempetion serikali kuingiza magari hayo akanyimwa.akaona isiwe nongwa akapanga dili na mshenzi huyo tukabamizwa na Stella!!!!!! Na suala la magari achilia mbali ubingwa tukawa tumekosa!!! Mshezi mwameja yeye alikatiwa.
    MWENYEZI MUNGU AMUWASHIE MOTO WA MAWE SIKU ZA KIAMA CHAKE.

    Mangi wa K'koo

    ReplyDelete
  2. we michuzi wacha fiksi, hiyo siotimu ya simba ni timu ya taifa ya miaka ya 1990.Waliochuchumaa wa kwanza kulia ni Joseph Lazaro, wa kwanza kulia waliosimama ni kocha wa stars sunday kayuni, David Mwakalebela wa nne kulia waliosimama na wa kwanza kushoto waliochuchumaa ni Sanif Lazaro Tingisha.

    ITS ME MZEE WA LIVERPOOL, KIBOKO YA WACHOVU MAN

    ReplyDelete
  3. Kaka Umeshachemka na Swaum Hii Ni tanzania Bara katika michuoano ya chalenge Cup Unguja Hapo uwanja Wa Amani Mwaka 1991 Kutoka Kushoto kwenda Kulia Azim Dewji(Meneja Wa Timu) Idi Pazi "father"Edward Chumila(Marehemu)David Rodger, Kingsley malwiro,David Mwakalebela,Twaha Hamidu"Noriega" Mohammed Mwameja na Sunday Kayuni (Kocha)Waliochuchama Kutoka Kushoto kwenda Kulia Sanifu Lazaro Tingisha,Hamza Mponda,Hamza maneno,Juma Burhani,zamoyoni mogella,george Masatu,Method Mogella(mareheumu)Na Joseph Lazaro Hapa walicheza na Uganda Na kufungwa Ni Hamisi gaga(Marehemu)Na Athumani China Ndio Hawakuwepo katika Picha
    Mdau Wa soka la bongo
    Shebbe Jeizan

    ReplyDelete
  4. namuona mzee zamoyoni magoli!

    ReplyDelete
  5. SHEBBE JEIZEN WE KIBOKO KWELI HUJAFANYA KOSA HATA MOJA KUTAJA MAJINA YA WACHEZAJI SI UTANI UMEBOBEA KATIKA SOKA MAANA HATA MIMI NI MTAALAMU WA SOKA KWA HII ORODHA WEWE NI KIKOMO KATIKA MEDALI ZA SOKA BONGO,NIKIJA BONGO INABIDI NIKUTAFUTE,SHKRANI KWA KUTUPA RAHA WADAU WA NJE YA NCHI

    ReplyDelete
  6. Asante Sana SHEBBE JEIZEN- yaani umenipa raha sana kunitajia hichi kikosi mim ni mpenzi wa Simba hasa kipindi hicho cha 1990s, lakini nilikwama kidogo katika kukumbuka majina. umenifurahisha sana best yangu. mdau wa New Zealand

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...