kikosi cha yanga ambacho wadua wengi wanahisi ndicho kilichokuwa bora katik historia ya wana wa jangwani ambao kwa sasa wanafanya vyema kwenye ligi kuu ambapo hawajapoteza hata gemu moja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. ngoja nijaribu kuwatambua
    Waliosimama to shoto:-mkwasa,buruhani hemedi,hamisi kinye,joseph fungo,ahmad amasha,selemani jongo,isihaka hassan"chukwu"na saleh hijja saleh huyu nakumbuka alikua mtaalamu kutoka znz.
    Waliochuchumaa toka shoto:-mkambi"jenerali",chama(kiboko ya mogella),simkumbuki,omar hussein,simkumbuki,allan shomari na wawili waliobaki nimeshindwa kuwakumbuka.
    Enzi hizo beki anamfukuza mtu ardhi unaisikia inavyocheza.

    ReplyDelete
  2. Naweza kumtambua Charles Boniface Mkwasa wa kwanza kushoto waliosimama na Amasha (wa tano toka kwa Mkwasa). Haya wadau nani atawajua wote. Zawadi tiketi ya Yanga na Simba (2010).

    ReplyDelete
  3. Nilikuwa Na umri Wa Miaka 12 Na Nilikuwa taifa Na Hii ilikuwa Ndio Mechi ilioamua Nani Atakuwa Bingwa Wa Super League 1981 Kati Ya Wanandugu Wawili Dar Young african Na pan Africa Nakumbuka Mpaka Leo Ngoma mpaka Mwisho 0-0 Katika Picha nawakumbuka wote kutoka kulia Kwenda Kushoto Waliosimama Charles Boniface"Mkwasa",juma Shabban,Hamisi Kinye,Joseph Fungo,Ahmed Amasha,Suleiman Jongo,Isihaka Hassain"Chukwu" Na Saleh Hija
    Waliochutama Kushoto Kwenda Kulia ni nahodha Juma Mkambi"General"Athuman Juma "Chama"Charles Kilinda(sasa hivi kocha Wa JKT Ruvu,Omar Hussein "Keggan"Issa Mohammed "Killer"Alan Shomari, Charles Alberto(Marehemu),Na Rashid Hanzuruni Kwa Maoni yangu Kaka michuzi Nadhani kikosi kilichokuwa Bora zaidi ni Kile Cha mwaka 1983 ambacho Hakikupoteza Hata Mechi moja katika iliokuwa Ligi Daraja La kwanza Tanzania bara Ambacho Kilikuwa na kina Marehemu Yusuph Bana,makumbi Juma,Abeid Mziba,Hussein idi,Moshi Majungu Juma kampala Na Ali Mchumila
    Mdau Wa Soka La Bongo
    Shebbe Jeizan.

    ReplyDelete
  4. Mdau Shebbe nimekukubali..Duh kumbukumbu yako nzuri sana. Hongera

    ReplyDelete
  5. Yusuf Athman Ismail Bana- RIP.sikujua kama huyu ni marehemu.

    ReplyDelete
  6. juma shabani alikuwa beki kiboko from moro, omar hussein pia alikuwa mshambuliaji wa mairi, alikuwa na ndugu yake abdallah hussein enzi za mseto. nashukuru kumuona juma shabani kwenye hii group

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...