stelingi maarufu wa kihindi sunjay dutt akimpongeza mkuu wa wilaya ya nanihii kwa kuwa ambasadaa wa zain, na chini anakula pozi na maulidi baraka wa kitenge. hii ni leo hoteli ya kempinski alikofikia stelingi huyu ambaye aliiambia globu hii ya jamii kuwa baada ya kumaliza shughuli na balozi wa zain anaelekea serengeti kwa vekesheni. amesema hii si mara yake ya kwanza kuja bongo na anasema anaizimia sana nchi hii, ila basi tu
mambo ya sunjay dutt bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Michu!

    Mbona jamaa anarembua macho? au swaumu? pia imekuwaje wanajeshi wetu wamemuacha na hicho kivazi? nakumbuka Joti wa Ze Comedy alirukishwa vichura.

    ReplyDelete
  2. Astaghafulilahi we kijana!! shughuli gani hiyo anayoifanya na balozi wa zain ndani kempisky???? tafwadhali

    ReplyDelete
  3. Ukisoma wasifu wa Sanjay utaona kuwa hapa Tanzania masuala ya sheria za utoaji viza yapo yapo.

    Sidhani kama mtanzania ukiwa na 'tuhuma' hizo za Sanjay utafanikiwa kupata viza kuingia nchi za ulaya (EU) na Marekani. Na hasa hasa ukizingatia vita dhini ya 'ugaidi'.

    Labda hapa 'sheria''haki za binadamu' na 'pesa' ndo inafanya wageni kuingia kirahisi Tanzania,

    ReplyDelete
  4. Nimefurahi sana kuona picha hii ya nanihii na huyu jamaa Sunjay Dutt.Watu wengi watamkumbuka hayati mama yake NARGIS ambaye alikuwa apendwa sana huko Bongo wakati wake Na jee mwaikumbuka film ya bollywood iliyokuwa kali sana =Mother India.
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  5. KARIBU SANA MUNA BAI TUMEFURAHI KUKUONA.

    ReplyDelete
  6. Kaka umenikumbusha longtime sana kuna movies zake kadhaa nilikuwa nazi mind sana miaka hiyo kama "Kanoon Apna Apna" ebwna bongo naona panatisha siku hizi kwa mastaa.

    ReplyDelete
  7. BIG UP SUNJAY DUTT NAIKUMBUKA SANA MOVE YAKO YA JEET HAIN SHAANSE.KARIBU SANA TANZANIA

    ReplyDelete
  8. Jamani hicho kivazi cha juu inadaiwa kuwa tukivaa wanajeshi watatukamata sasa inakuwaje huyu bwana kapita kote huko tangu airport hadi hotelini bila bugudha na sehemu zote hizo askari wapo. Anaejua kuhusu sheria hii naomba anifahamishe tafadhali nisije nikapata misukosuko mwenzenu.
    Mdau wa TOKYO.

    ReplyDelete
  9. Mi hilo jicho lake huniacha hoi

    ReplyDelete
  10. Kaka Michuzi

    Pamoja na sifa nyiiingi ulizomwaga kwa Huyu Ponjoro, mbona wasifu wake waonyesha kuwa ni Criminal kaka. Akina Manumba wanafanya nini, anaweza kuwa na connection na magaidi huyu. Kwanini asiwekwe ndani huyu. I am pissed off my country immigration procedure to allow such a criminal top step on our land

    ReplyDelete
  11. Kaka Michu,

    Huyo mtu uliyopiga naye picha siye kabisa Sunjay Dutt mwenyewe. Lakini sikulaumu kwa kutapeliwa maana wamefanana kidogo. Kama uliwahi kumpa cho chote ili na wewe upate ''role'' ndogo katika moja ya filamu zake basi pole sana kaka.
    teh..teh..teh

    ReplyDelete
  12. Huyu bwana hayo macho amepata kilimanjaro baridi nini?? kama jajapata basi akipata sipati picha kama ataweza hata kuyafungua...
    by the way movie za jamaa zimetulia sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...