stelingi maarufu wa kihindi sunjay dutt akimpongeza mkuu wa wilaya ya nanihii kwa kuwa ambasadaa wa zain, na chini anakula pozi na maulidi baraka wa kitenge. hii ni leo hoteli ya kempinski alikofikia stelingi huyu ambaye aliiambia globu hii ya jamii kuwa baada ya kumaliza shughuli na balozi wa zain anaelekea serengeti kwa vekesheni. amesema hii si mara yake ya kwanza kuja bongo na anasema anaizimia sana nchi hii, ila basi tu
mambo ya sunjay dutt bofya hapa
mambo ya sunjay dutt bofya hapa
Michu!
ReplyDeleteMbona jamaa anarembua macho? au swaumu? pia imekuwaje wanajeshi wetu wamemuacha na hicho kivazi? nakumbuka Joti wa Ze Comedy alirukishwa vichura.
Astaghafulilahi we kijana!! shughuli gani hiyo anayoifanya na balozi wa zain ndani kempisky???? tafwadhali
ReplyDeleteUkisoma wasifu wa Sanjay utaona kuwa hapa Tanzania masuala ya sheria za utoaji viza yapo yapo.
ReplyDeleteSidhani kama mtanzania ukiwa na 'tuhuma' hizo za Sanjay utafanikiwa kupata viza kuingia nchi za ulaya (EU) na Marekani. Na hasa hasa ukizingatia vita dhini ya 'ugaidi'.
Labda hapa 'sheria''haki za binadamu' na 'pesa' ndo inafanya wageni kuingia kirahisi Tanzania,
Nimefurahi sana kuona picha hii ya nanihii na huyu jamaa Sunjay Dutt.Watu wengi watamkumbuka hayati mama yake NARGIS ambaye alikuwa apendwa sana huko Bongo wakati wake Na jee mwaikumbuka film ya bollywood iliyokuwa kali sana =Mother India.
ReplyDeleteWakatabahu
KARIBU SANA MUNA BAI TUMEFURAHI KUKUONA.
ReplyDeleteKaka umenikumbusha longtime sana kuna movies zake kadhaa nilikuwa nazi mind sana miaka hiyo kama "Kanoon Apna Apna" ebwna bongo naona panatisha siku hizi kwa mastaa.
ReplyDeleteBIG UP SUNJAY DUTT NAIKUMBUKA SANA MOVE YAKO YA JEET HAIN SHAANSE.KARIBU SANA TANZANIA
ReplyDeleteJamani hicho kivazi cha juu inadaiwa kuwa tukivaa wanajeshi watatukamata sasa inakuwaje huyu bwana kapita kote huko tangu airport hadi hotelini bila bugudha na sehemu zote hizo askari wapo. Anaejua kuhusu sheria hii naomba anifahamishe tafadhali nisije nikapata misukosuko mwenzenu.
ReplyDeleteMdau wa TOKYO.
Mi hilo jicho lake huniacha hoi
ReplyDeleteKaka Michuzi
ReplyDeletePamoja na sifa nyiiingi ulizomwaga kwa Huyu Ponjoro, mbona wasifu wake waonyesha kuwa ni Criminal kaka. Akina Manumba wanafanya nini, anaweza kuwa na connection na magaidi huyu. Kwanini asiwekwe ndani huyu. I am pissed off my country immigration procedure to allow such a criminal top step on our land
Kaka Michu,
ReplyDeleteHuyo mtu uliyopiga naye picha siye kabisa Sunjay Dutt mwenyewe. Lakini sikulaumu kwa kutapeliwa maana wamefanana kidogo. Kama uliwahi kumpa cho chote ili na wewe upate ''role'' ndogo katika moja ya filamu zake basi pole sana kaka.
teh..teh..teh
Huyu bwana hayo macho amepata kilimanjaro baridi nini?? kama jajapata basi akipata sipati picha kama ataweza hata kuyafungua...
ReplyDeleteby the way movie za jamaa zimetulia sana.