kwa kile kinachoonekana kushindwa gemu inasemekana kuna baadhi ya mahasimu wa kampuni ya kilaji nchini TBL wamekuwa wakiihujumu kwa kufuta matangazo ya biashara kwenye sehemu kadhaa nchini, hasa mjini moshi na a-taun kama inavyoonekana kwenye picha hizi zilizoletwa na mdau wa huko. kitendo hiki haramu na cha aibu kimelaaniwa sio tu na TBL bali pia walaji wa bidhaa zake ambao kwa hasira wamesema wataendeleza libeneke na TBL hadi kieleweke. wamedai kuwa mtu ukishindwa gemu hii tafuta mbinu ingine na sio hujuma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nawapongeza hao waliofuta matangazo wa TBL maana idadi ya walevi imezidi kuongezeka. Takwimu zinasema kuwa 75% ya Watanzania ni alcoholic.

    Ni nchi ya pili inayoongoza kwa ongezeko kubwa la walevi duniani ikiifuatia Urusi.

    Uchumi wetu unazidi kudidimia na productivity haiongezeki.

    Watu wanashinda vilabuni 24 hrs matokeo yake wamekuwa watumwa wa pombe.

    ReplyDelete
  2. hiyo issue mi naona ni mchezo mchafu "gorrila marketing" unachezwa.wanaofanya ni hao hao TBL .wao ndio wameshindwa game na hii ni baada ya wapinzani kuwa katika mchakato wa kufungua kiwanda hapo.wanajua watapigwa bao muda si mrefu kama ilivyo dar,mwanza na kwingineko.TBl waliwahi kuwa wananunua bia za wapinzani kwa maroli na kwenda kuzivunja..wakashindwa wakaanza kuchukua chupa sababu zinafanana ili jamaa wakose chupa sasa kuna chupa ndefu zaidi ya zao.wachukue na hizo basi.sasa naona wanataka kuonyesha watu kuwa wapinzani wameshindwa.hiyo ni janja yao..wapinzani lazima tuwafunike hao kenge

    ReplyDelete
  3. Jino kwa Jino maana wao nao walihujumu kiwanda cha bia ya Kibo hapo Moshi.

    ReplyDelete
  4. Wewe ulietoa takwimu hapo ni kivyako na kwa taarifa yako haitasaidia kushusha hiyo pasenti hata mabango yote yatolewa lager zitauzika kama kawa tulishazijua. kili na products zingine zooote.hao wanaofanya ivo wang'oe kabisa.

    ReplyDelete
  5. mbege imekosa wanywaji,hahahahahaha

    ReplyDelete
  6. annon wa kwanza sawa sawa,,,
    hawa watu ni wauaji tuu,basi mnywe na mchape kazi mzalishe na pato la m Tz liongezeke,,,bt mwakalia kilevi weeee no kazi no uzalishaji,,lo umaskini ndo tunao na bado mwaendekeza ulevi

    ReplyDelete
  7. Yawezekana kuwa waliofuta hayo matangazo ni walevi wenyewe, yaani wateja wa TBL.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...