wachezaji wa yanga wakila pozi na kombe lao la ubingwa wa soka bongo na afrika mashariki na ya kati. anayesoma gazeti ni mh. saidi el maamry wakati huo akiwa mwenyekiti wa fat alienda kuwapa pongezi vijana. wadau wenye kompyuta kichwani mnakumbuka mwaka gani huu na je hao wengine ni kina nani?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. MICHUZI MIE NAOMBA KUULIZA KUNA MCHEZAJI MMOJA WA KIKAPU ALICHEZEA JESHINI MIKA YA 70 ALIKUWA MREFU SANA TANZANIA NZIMA ALIKUWA ANAITW A BILLY URAASA ALICHEZA MPIRA WA KIKAPU JESHINI YUKO WAPI?UNAWEZAA KUTUWEKEA PICHA YAKE HEWANI??ALIKUWA NI MTU MREFU SANA TANZANIA NZIMA ENZI ZA MIAKA YA SABINI NA ALICHEZA SANA MPIRA WA KIKAPU...NASIKIA YUKO KIGAMBONIO KARIBIA NA JESHI..TUWEEKEE STORY ZAKE BWANA ALIKUWA JAMAA MMOJA SAFI SANA ENZI HIZO ZA KABLA HATA MIPIRA YA KIKAPU HAIJAVUMA TANZANIA...ASANTE SANA

    ReplyDelete
  2. Aliyelala ni GIBSON SEMBULI- NI MAREHEMU SASA. MWENYE NGUO NYEUPE SHATI NA SURUALI NI SUNDAY MANARA, HUYO MWEMBAMBA MREFU NI ABDLEHEMAN WENGINE NAWAKUMBUKA KWA SURU MAJINA YAMENITOKA.

    ReplyDelete
  3. Naowafahamu hapo kulia Gibson Sembuli(RIP) kulia,Sunday Manara karibu na kombe na Abdulrahman Jumah katikati.wengine siwajui nilikuwa lactogen kipindi hicho but YANGA damu damu.
    Cha chandu - UK

    ReplyDelete
  4. nadhani ilikuwa mwaka 1975 kwani mwaka wa nyuma yake Simba ndio ilikuwa mabingwa na yanga waliwachapa watani hao wa jadi. Aliyeinama anaeonekana kichwa na mkono ni Omari Kapera alikuwa ndio Center Half wa yanga enzi hizo mwengine hapo ni Abdurahman Juma kama sikosei, Sembuli(RIP) Sunday Manara Computer,Dilunga

    ReplyDelete
  5. Nimegundua kitu kimoja watu wa zxamani hawakuwa na VIPARA siku hizi mtoto miaka 16 ana upara kichwani.

    ReplyDelete
  6. Hiyo ni mwaka 1975 Yanga walipochukua ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kule Zanzibar baada ya kuifunga Simba kwa mabao 2-1 yaliyofungwa na Sunday na Sembuli. Mwenye mawani ni kocha Tambwe Leya (RIP), aliyemshika Abdulrahman Juma 'Linkman' ni golikipa Muhidin Fadhili na alkiye karibu na Sunday ni Adam Juma kama sikosei....

    ReplyDelete
  7. Mwenye afro nyuma ya marehemu Sembuli ni Muhudini Fadhili alikuwa golikipa wa Yanga

    ReplyDelete
  8. Januari 1975 magoli mawili yaliyofungwa na Sunday Manara na marehemu Sembuli (RIP). Hii ilikuwa miezi kadhaa baada ya kuwaliza Simba Nyamagana (kwa haki au Manyoto anajua Mungu). Nilikuwa darasa la sita na nakumbuka kuusikiliza mpira huu katika redio ya kaka yetu marehemu Ibrahim (RIP) aliyekuwa mwanachama wa Yanga akiwa na kadi ya njano. Alikuwepo pia Hamisi Issa Kwezi, marehemu Ali Kombo (RIP), Juma athumani (Mazig-zag Kibandiko Jomba Jackson 5 mtu wa ... (jaza hapa nakupa zawadi) tajiri wa saba katika dunia ya tatu).

    Thank you for Michuzi for always bringing good old memories flooding back.

    ReplyDelete
  9. Chesi,
    nakurekebisha kidogo mwenye miwani anayesoma gazeti bro Michuzi yuko right ni Said Hamad El-maamry but pia huyo mwenye miwani nyuma ya Sunday Manara ndie kocha Tambwe Leya(RIP).hata nilikuwa sijui keshafariki.
    Cha chandu- Uk

    ReplyDelete
  10. saaaaaaaaaaaaaaaaaaafi sana wadau,,naskia buldiko la roho apa
    aisee MICHU siku NIKIKUONA SURA KWA SURA LZM NIKU-HUG NA MWAA LA NGUVU,,unanruhusu???kumbuka hili na tar ya leo kbs,,,
    nimekupenda sana kwa izi newzzzz,,home swit home

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...