KUNRADHI WADAU,
HUWA SINA KAWAIDA YA KUSEMA SEMA SANA ILA NATAKA NIWEKE JAMBO MOJA SAWA.
KUNA HILI LIBENEKE LA WATU KUTUMA PICHA NA SALAMU KWA WADAU WENZAO AMBALO LILIWAHI KUSITISHWA KWA MUDA BAADA YA JAMAA KUCHAFUA HALI YA HEWA, NA BAADAYE LIKAFUNGULIWA TENA NA HADI LEO PICHA NA SALAMU VINAPOKEWA NA KUTUNDIKWA KAMA KAWAIDA.
KUNA BAADHI YA WADAU WANA TABIA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA NA KUKATISHA TAMAA WENZAO KWA KUOSHA VINYWA, HATA SIJUI NI KUTAKA SIFA AMA KUPUNGUZA STRESI ZAO ZA MAISHA, MRADI TU WAMJERUHI MDAU MWENZAO.
UJUMBE HUU NI KUWATOA HOFU WADAU WOTE WANAOTAKA KUTUMA SALAMU NA PICHA HASA KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU YA IDD EL FITR, KWANI HAKUNA HATA MDAU MMOJA ATAYEJERUHIWA KWANI NAHAKIKISHA HALI YA HEWA INABAKI SAFI KWA KILA PICHA NA SALAMU.
HAO WADAU WACHACHE WAOSHA VINYWA NAWAOMBA WASIJISUMBUE KUTAKA KUCHAFUA HALI YA HEWA KWENYE GLOBU HII YA JAMII KWANI MAONI YAO HAYATOONA MWANGA WA JUA.
WAKATABAHU
-MICHUZI
NB: KAMA ILIVYOA ADA TAYARI HAPO CHINI KUNA WAPENDWA WADAU KIBAO AMBAO BAADHI WANATAKA KUPOTOSHA UKWELI NA KUNIWEKA MANENO MDOMONI KWAMBA NINA NIA YA KUZUIA UHURU WA HABARI. NAOMBA NISEME SINA NIA HIYO NA WALA MIE SIJASEMA NAZUIA KILA KITU, BALI MAONI YANAYOCHAFUA HALI YA HEWA KAMA VILE MATUSI YA NGUONI NA CHUMBANI NDIYO TATIZO. NA HAYO NI MENGI KULIKO MTAVYOWEZA KUFIKIRIA.
PIA ENDAPO KAMA UHURU WA HABARI NI KUMJERUHI MDAU MWENZETU KWA KUMSUTA NA KUMVUA NGUO HADHARINI, BASI LIWALO NA LIWE LAKINI KATU SINTORUHUSU HALI IWE HIVYO KATIKA GLOBU HII YA JAMII.
IELEWEKE PIA KWAMBA KUNA UTANI AMBAO KAMA ANAVYOSEMA MDAU HAPO CHINI NDIO CHACHANDU ZA GLOBU, HAYO MATANI SINA NENO NAYO. NONGWA YANGU NI MATUSI YA NGUONI NA KUJERUHI WADAU WENZETU
LIBENEKE OYE!


mmh Michuzi acha kubana!!
ReplyDeletewee huoni hali ya hewa siku hizi mbaya kila kona!! kuna matsunami sijui nk.
Endeleza libeneke mzee, natakia lakini kweli
Mdau
oky, nimeeleweka kaka Mchuzi.
ReplyDeleteNa mimi sitaona MWANGA WA JUA??? nimulike basi......Nahaidi kuanzia leo naacha kazi ya KUOSHA KINYWA.... kwanza hailipi meno yanaendela kuoza tuuu na mdomo unanuka bado.
AM BORN AGAIN...
Mambo Michuzi?
ReplyDeleteMi nina swali moja ndugu yangu hivi blog zenu huko nyumbani kwa nini zote zinakuwa na karibu kila kitu sawa yaani inakuwa kama mtu mwingine anakuwa na blog na kazi yake ni kuchukua habari zilizo kwenye blog za wengine kiasi kwamba hata wewe kama vile umeiga hako katabia?
Sidhani kama maoni yangu nayo yanachafua hali ya hewa naomba unijibu ndugu yangu kwani naona kama ubunifu unakuwa zero.
Sawa Mkuu wa Wilaya, Balozi wa Zain na Mzee wa Libenekezzz.
ReplyDeleteHata hivyo utaua FREEDOM OF SPEECH. Bila shaka wadau wanaotuma hizo salamu ni WATU WAZIMA (18 years and above) kwa hiyo hawahitaji uwakingie kifua.
Kama yule mdau wa "We meet at Leicester Square" si unaona alivyojibu mapigo bwana? Hiyo ndio flavor ya Globu.
Ila kama utaweka salamu za kina Haki Elimu (ie, under 18) basi hao ndio inafaa uwakingie kifua.
Ni mtazamo tu Mkuu wa Wilaya. Usiminye comment.
//Mdau
Tatizo kubwa lilikuwa sio kuchafua hali ya hewa muheshimiwa michuzi,tatizo lilikuwa watu wanatuma picha ambazo sio zao.
ReplyDeleteJe una njia gani ambayo unaweza kuhakikisha kwamba huyo mtu anayekutumia picha ni yake?
Hili swala ndio linaendelea kwenye hile blog ya UTAMU, watu wanatuma picha za watu hili watukanwe na kadhalika.
Ushauri wangu kwako michuzi ni kwamba blog inaendelea vizuri tu bila ya hizo salamu kwahio wala haina haja ya hizo salam kwa njia picha hili kujiweka kando na swala zima liloletwa na mtu kama Utamu.
Kwa ufupi ni kwamba hakuna njia ya kuweza kujua kama mtu aliyetuma picha ni yake au sio.
Mdau mzawa ,
Wanaochafua hali ya hewa wanafanya hivyo kwa baraka zako, kwani kama hutaki wachafue hali ya hewa, usingetundika mabandiko yao.
ReplyDeleteWee Michuzi kutembea kote huko duniani bado hujaelimika! Ama kweli mjinga ni mjinga tu hata akienda shule...! Wewe umelelewa na CCM ndo maana ubongo wako hautakati,unamawazo mgando kama ya babu yako Kingunge! How comes mpaka karne hii ya 21 umebaki na siasa zako za kuwanyima watu uhuru wa kueleza mawazo yao! Kama hutaki mawazo "gongano" basi hii blog usiite blog ya jamii! Sababu haiwi jamii bila kuwa na watu wenye maoni, mitazamo na hulka tofauti!
ReplyDeleteHata anaetoa tafsiri tofauti na ile ulonayo wewe juu ya picha uloweka pia ni mtu muhimu katika jamii (wewe unamuita mchafuzi wa hali ya hewa)!
Ukiweka picha yako kwenye jamii lazima uwe na "sense of humour" Kama huwezi mpelekee mkeo akusifie, ila kwenye jamii usitegemee majibu chanya pekee lazima kuwe na watu wenye mitazamo hasi!
HABARI NDO HIYO.....
Safi sana Mhe. Ambasada.wenye vinywa vichafu waweke kwapani.tena ktk kwapa la mwendawazimu ili nextyme wasijisumbue kufumbua vinywa vyao no more.
ReplyDeleteNAKUSHURURU SANA KAKA MICHUZI KWA KULIWEKA HILI JAMBO HADHARANI,MIMI NI MDAU WAKO MZURI SANA KWA SASA NAISHI CALGARY-CANADA HUWA HAIPITI SIKU BILA KUPITIA HII GLOB YAKO,KWELI INAKERA SANA KUSOMA COMMENTS ZA WADAU WENGINE KWANZA WAKATI MWINGINE LUGHA WANAYOITUMIA SIO NZURI,UNAKUTA MTU KAANDIKA COMMENT YAKE NZURI TU MWINGINE ANAYIBU VIBAYA HAIPENZEZI TUHESHIMIANE JAMANI KAMA HUJAELEWA ULIZA KWANZA.TUWE WAASTARAABU JAMANI,HII NI GLOB YA JAMII.NAKUTAKIA KILA LA KHERI NA HONGERA SANA KWA KUIELIMISHA JAMII YETU.
ReplyDeleteHii poem nimeipokea leo kwenye email na imenitouch sana na inawafaa sana hawa waosha vinywa.
ReplyDeleteHater...By Maya A ngelou
A hater is someone who is jealous and envious and spends all
their time trying to make you look small so they can look tall.
They are very negative people to say the least. Nothing is ever good enough!
When you make your mark, you will always attract some haters...
That's why you have to be careful with whom you share your blessings and your dreams, because some folk can't handle seeing you blessed...
It's dangerous to be like somebody else... If God wanted you to be like somebody else, He would have given you what He gave them!......Right?
You never know what people have gone through to get what they have...
The problem I have with haters is that they see my glory,but they don't know my story...
If the grass looks greener on the other side of the fence, you can rest assured that the water bill is higher there too!
We've all got some haters among us!
Some people envy you because you can:
a) Have a relationship with God
b) Light up a room when you walk in
c) Start your own business
d) Tell a man / woman to hit the curb (if he / she isn't about the right thing)
e) Raise your children without both parents being in the home
Haters can't stand to see you happy.
Haters will never want to see you succeed.
Most of our haters are people who are supposed to be on our side.
How do you handle your undercover haters?
You can handle these haters by:
1. Knowing who you are & who your true friends are (VERY IMPORTANT!!)
2. Having a purpose to your life: Purpose does not mean having a job. You can have a job and still be unfulfilled. A purpose is having a clear sense of what God has called you to be. Your purpose is not defined by what others think about you.
3. By remembering what you have is by prerogative and not human manipulation.
Fulfill your dreams! You only have one life to live...when its your time to leave this earth, you 'want' to be able to say, 'I've lived my life and fulfilled 'my' dreams,... Now I'm ready to go HOME!
When God gives you favor, you can tell your haters, 'Don't look at me...Look at Who is in charge of me...'
Lakini uhuru unao kuliko kupoteza muda wa kusoma na kufilter mambo mabaya ni heri kila mtu anayetuma salamu zake wewe ufunge comment link. You can do that....and you know it...you choose to let people to comment on those pictures...so stop that now.....
ReplyDeleteNa huyo mtu akituma salamu zake ni kueleza tu yuko wapi na anawasalimia nani na nani...kama RTD salamu za mchana vile....that is it.....na kama akikucontact mtu ambaye picha yake umeiweka lakini yeye hakuituma au kuiapprove basi unaiondoa na kunakua hamna linaloharibika.
Na wewe pia unajukumu la kuweka picha ambazo zitakua hazichafui hewa huku. Sio kila picha unayopokea basi ni kuitundika bila kujali ninani watu wanaosoama humu kwenye blog...mimi nimetoka mbili sana na hii blog yako.....na nimeona toka ulivyoanza kuweka zile picha za mwanadada anayependa kukaa kaa nusu uchi ndio watu nao wakaanza kuchafua hali ya hewa.
So ushauri wangu ni kuwa ukiwaserious na watu watakuchukulia serious, ukiwaheshimu watu nao watakuheshi na pia usipoweka picha za kuwafanya watu kuwashwa na midomo basi wachafua hewa wataboleka na kuhamia kwenye blog zinazo wafaa.
Mimi ninabelieve kuna freedom of speech na kuna comments ambazo unazitupaga lakini hazina lolote katika kuchafua hewa kabisa labda ziko too deep for Tanzania people/Govt to handle the truth(ziwezi kukulaumu kwa vile unahitaji kukeep your job) Ila kuna zingine unaziweka na unajua fika zimetumwa na mtu kwa nia mbaya...
So you be a big man here...
Freedom of speech Bro michuzi nawala sio kuchafua hali ya hewa. Hizi itikadi za kisoshalisti kwamba habari njema ni ile inayom please mmiliki mwa hicho chombo cha habari au yule mwenye mamlaka imepitwa na wakati.
ReplyDeleteCheck CCN Bro.
THEY REPORT THE NEWS OUT AND YOU DECIDE.
Achana na hizo fikra za kizamani
Mdau wa demokrasia ya kweli
Wacha kubana bwana ruhusu comments ili watu tujue nani ni nani ili sisi washamba tusitatizike na kuingizwa mjini.
ReplyDeleteBaelezee bwana baswahili bamezoea kutukana watu matusi eti freedom of speech! Freedom of speech my foot! Ina mipaka yake ndio maana kuna sheria mbali mbali zimetungwa ama sivyo watu wangekuwa wanatukana wee na wakienda mahakamani wanapeta. Ila wanafikiri matusi ya kumtukana mtu kwenye blogu/internet hayako katika sheria au huwezi kukamatwa. Siku mmoja akidakwa huko aliko pamoja na kujificha kwenye screen ndio anashangaa. Na nyie mnaojidanganya eti mko kwenye Internet Cafe IP address ni ya mwenye cafe mnajisumbua hakuna lisilowezekana duniani kuna software zinarekodi picha yako bila kujijua, ukiona mahala unaambiwa click wewe unaclick tu au unaulizwa swali jibu yes or no unaclick kumbe picha ishachukuliwa zamani yoote baada ya sept 11.Kwa hiyo wala msiidanganye eti hawanioni wakikutaka popote pale utapatikana sasa endeleeni na hayo matusi yenu kwa mgongo wa freedom of speech siku mtu akiamua kuwachukulieni hatua mtakuma kuringa!
ReplyDeleteKaka michuzi mbona umeeanza na mikwara ya wachafuzi wa hali ya hewa nini maana ya freedom of speech.Mdau wa holland.
ReplyDeletesep 20 3 pm umenivunja mbavu...ndio kudanganyana huko.....ati click hapa umepigwa picha...hata kama computer haina camera basi picha imeshachukuliwa....ha hahahahahah.....
ReplyDeleteSheria za internet bado zimepitwa na wakati. Hakuna international law kwa haya mambo na ndio hicho kinachowakuna kichwa mataifa mengi.