marehemu abdel azizi
marafiki wakienda kumzika abdel azizi
mazishini nje kidogo ya kuala lumpur
Mmoja wa majeruhi wa kisanga hicho akiwa makaburini alikokuja kumzika Abdel, Bwana huyu ameshonwa nyuzi 18 kichwani.

Mwanafunzi wa mwaka wa Kwanza katika chuo cha HELP University Abdel Aziz Hassan Abdraman, 22, kutoka Chad ameuwawa jumapili usiku na vijana wanaokisiwa kuwa 20.

Katika tukio hilo Wanafunzi hao wa kiafrika walikutana na kundi la vijana wa Kimalay na kuaanza kushambuliwa.

Kabla ya tukio hilo MWanafunzi mmoja wa Kiafrika ambaye alikuwa amteremka kutoka katika Train alikutana na kundi hilo la vijana wa kimalay ambao walimtaka awapatie pesa au simu akipokaidi kufanya hivyo vijana hao walimvamia na kuanza kumpa kisago alifanikiwa kukimbia na kuomba msaada kwa wenzie ambao hawakuwa mbali na eneo la tukio.

Walijikusanya na kuamua kumpeleka mwenzao Hospitali wakiwa njiani walikutana na vijana wale ambao waliwabvamia tena na kuanza kuwapa kichapo huku wakitumia Nondo, Visu na Waya.

Marehemu alichomwa na kitu chenye ncha kali kinachoaminika kuwa ni kisu mgongoni kikatokea kifuani na alianguka hapo na kupoteza fahamu.
Juhudi za kumpatia msaada wa haraka zilishindikana kwani hakuna Tax aliyokubali wala gari ya kawaida kumpeleka Hospital mpaka msamalia alipoita Ambulance ambayo ilifika dakika 45 baadaye na marehemu alifariki akiwa njiani.

Kumekuwa na malalamiko toka kwa jumuiya ya Waafrica hapa Malaysia kwa vitendo vya kibaguzi wanavyokutana navyo hasa kutoka kwa wenyeji wamalay, ambapo mara nyingi wamekuwa wakipigwa na kutupia Waafrica maneno ya kejeli na dharau.


Hili ni tukio la 3 kwa waafrika kushambuliwa siku za karibuni na makundi ya Wamalay. Kumekuwa na malalamiko kuwa kumekuwa na ongezoko la waafrica Malaysia ambao Loca Malays wanaona kama wanaingiliwa hata kiutamaduni na hivyo kuleta rabsha.

Marehemu amezikwa leo katika makaburi ya Waislamu nje kidogo ya jiji la Kuala Lumpur kwa baraka za Familia yake.

Hivi sasa kuna zaidi ya Waafrica 10,000 kwa malaysia ambapo nchi ya Botswana ndio inayoongoza ikiwa na wanafuznzi zaidi ya elfu 4 hapa. Tanzania inawafunzi wasiopungua 800 kwa Malaysia pekee. nchi nyingine ni Zimbabwe, Kenya, Uganda, Afrika ya Kusini, Chad, Nigeria, MAli, Burkina FAso, Senegal, Mali Comoro na hata Shelisheli.

soma zaidi hapa
http://www.mmail.com.my/Victims_of_hate.aspx
Marehemu ameacha mke na mtoto mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Innallillahi wainaillaihi rajiun. Poleni kwa msiba na poleni kwa madhila yanayowakuta. Dawa ya hao nungu nungu ni ndogo tu, ni kuwaambia kuwa hizi habari tunazipeleka kwetu kuwaambia watu wa Africa wasilete wanafunzi tena huko Malaysia, halafu mtaona matokeo yake. Mkishatoa tamko hilo kwa kupitia umoja wenu, hata mkiongea na vyombo vya habari vya huko ni kuwaambia hicho ndicho mtakachofanya, nakwambia na ulinzi mtapatiwa. Kwanini nasema hivyo, kwa sababu elimu siku hizi ni biashara. Nyie kama wanafunzi kwa idadi mliyopo mnaingiza pesa nyingi kwenye nchi yao kupitia tuition fees, malazi, chakula, mavazi kiujumla na matumizi yoyote mnayofanya. Sasa mkinyamaza wataendelea kuwaua huku mnawalipa serikali yao mapesa kibao ambayo yanawapa wananchi wao kiburi.

    Hivi karibuni kuna kijana kutoka Qatar wazazi wake matajiri walimpeleka mji mmoja UK kwenda kujifunza kiingereza, wakati wazazi wake wako kwenye ndege wanaenda kumfuata warudi naye kwao, inasemekana alishambuliwa na kundi la vijana wa kihuni akauawa, wazazi wake wakarudi na maiti badala ya mtoto aliye hai. Vijana wa Qatar nao wakasema watawaambia watu wa kwao wasipeleke wanafunzi UK, mbona hao vijana wahuni walikamatwa na ulinzi umeimarishwa. Kwenye mji mwingine pia wa UK mwaka jana waliwashambulia wanafunzi wa kutoka nchi za kiarabu, nao wakatishia kuiambia serikali yao isipeleke wanafunzi UK, huo mchezo umekoma kama si kupungua na hao wahuni walifikishwa mahakamani. Cha msingi ni kujua kuwa nyie si wanyonge, kwani ukifika Dar sasa hivi utakuta matangazo yamezagaa kutangaza uzuri wa vyuo Malaysia, na hali ya salama iliyopo. Mie mwenyewe nilikuwa nafikiria kuwa mwanangu akimaliza tu high school nampeleka huko Malaysia kusoma chuo kikuu, lakini hii habari imenifungua macho kwani kuna wazazi wengi kama mimi ambao tulikuwa tunafikiri kuwa huko angalau kuna unafuu. Sasa kama na wao wameanza hizo tabia chafu, dawa ni hiyo hiyo waambieni kuwa hizi habari tunazifikisha kwetu na kuwashauri watu wasilete tena wanafunzi kwenye vyuo vyao. Ni vyema ikatangazwa kwenye magazeti mengi iwezekanavyo ili wazazi ambao hawasomi habari kwenye mtandao wakafunguka macho, hata ikibidi kuandika barua kwa wahariri wa magazeti andikeni! Utaisikia balozi wao anavyojibu!!!

    ReplyDelete
  2. Hii thing imekuwa fashion dunia nzima, lakini hii pia inatokana na politics za wakubwa zetu kwani nchi zetu duniani kila kukicha wakubwa wanaongea juu ya immigration negatively sasa unadhani watoto watafanya nini, hii kitu inatakiwa kuwa addressed properly na international organs kama UN hivi, haya yatatokea sehemu nyingi hata USA, UK, CANADA na kwingineko kama tahadhali hazitachukuliwa. hii kitu Russia ndo usiseme usilogwe kwenda mjini mwanafunzi wa nchi ya nje utarudi jina na hao skinhead/vipara hawataki kabisa kuona mgeni. SASA ANAZIKWA HUKO HAPELEKWI KWAO! NDO SCHOLARSHIP ZA MALAY HIZO?

    ReplyDelete
  3. Poleni sana kwa dhahama iliyowapata. Dunia imejaa ubaguzi kwa wageni maana tumeona Sauzi, Urusi na sehemu nyingine. Tatizo kubwa ni vijana wenyeji kuona kuwa nyie mnapendelewa kwa kusoma kwenye vyuo vyao. Hawaelezwi kuwa wengi wenu mnalipiwa na wazazi wao na elimu muipatayo ni biashara kwa nchi na wananchi wao. Kwao waafrika ni wale wenye njaa kama Ethiopia na Darfur, mnalala kwenye miti n.k.
    Ushauri kwa wazazi Malaysia ni nchi yenye ubaguzi rasmi, upendeleo wa kila ktu kwanza ni wamalay. Ndio maana wanaugomvi na wamalaysia wenye asili ya kichina.
    Dawa yake muwe waangalifu na mtembee kwa makundi na kuweka buku sawasawa kwani ndicho mlichotumwa na wazazi wenu. Elimu ndio ufunguo wa dunia itawapeleka popote.

    ReplyDelete
  4. Innallillahi wainaillaihi rajiun. Poleni ndugu wafiwa na pole sana kwa mama wa mtoto maana hata mwili wa mwanae hawezi kuona hta kaburi lake. Ila jamani kwa nini tunaenda nchi ambazo hazitutaki? KWa nini tusirudi tuu tukaepusha shari?

    ReplyDelete
  5. INNALILAHI WAINNA ILAHIM RAJIUN.
    UKWELI HAYA MAMBO YA KUUANA YAKO ULIMWENGU MZIMA.AMA JANA TU KTK NCHI YA FINLAND KUMETOKEA MAUAJI KIJANA WA MIAKA 22 KUWAUWA WANAFUNZI 11 INGAWA NAE AMEJARIBU KUJIUA LKN HAJAFA YUKO HOSP.NI JAMBO LA KUSIKITISHA SANA VIJANA WADOGO NDIO WANAOFANYA MAUWAJI.HII ILIWAHI KUTOKEA PIA MWAKA JANA HUKO HUKO FINLAND.

    ReplyDelete
  6. Hao wengi wanaoenda Malay ni scholarship za kidini hivyo haitasaidia kuogomea kwenda huko kwa vile wengi wao ni wa scholarship hizo.

    ReplyDelete
  7. We Anon wa hapo mwisho nani kakwambia hawa wanakuwa sponsored, kwa taarifa yako wote walioko huku ni Private Sponsored kama hujui si lazima uongee.
    Ila poleni sana wafiwa, poleni wahanga wa mauaji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...