Ifunda Tech. Sec. School
''Ifunda the glorious technical secondary school viva! With our motto, skill and efficiency, we shall build our nation strong,and our school, shall shine forever more, Ooh! God bless our School"
Jamani mwenzenu nimekumbuka enzi zile za 1986 mpaka 1991, nilipokuwa nikisoma shule hiyo hapo juu. Lakini inasikitisha kuona shule yetu maarufu ikidorora siku baada ya siku.
Nimemuomba uncle Michuzi aweke tangazo hili hapa ili tutoe michango yetu ya mawazo, nini kifanyike ili kuinusuru shule yetu, iliyotoa watu maarufu na wa muhimu katika sekta ya uhandisi hapa nchini Tanzania na duniani kwa ujumla.
Nitafurahi zaidi kujua ulisoma pale kipindi cha miaka ipi, jamani wadau naomba kuwakilisha.
Niliyekuwa Mkazi wa Chaburuma-E1/ E3/ E6 and F4
ENZI ZA KOCHA NALIMI!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Mdau leo hasa umegusa kwenyewe, tungepata na picha ingekuwa bomba sana. Nilikuwa hapo 1995-1998 Ifunda Tech (IFUTESCO). Nilikaa SEUTA kwa muda kabla ya kurudishwa kwenye bweni langu Chabruma F5/F4 /F3. Umenikumbusha sana Chair wa bweni letu alikuwa jamaa mmoja mpenda sifa sana kutoka kusini tulimuita "Muje" kutokana na kushindwa kwake kutamka neno " mje" kama alivyopenda kusema "Muje Bohari". Nimewakumbuka sana classmates wangu na zile safari za Kibaoni siku za mwisho wa wiki na kwenda kusali Masumbo bila kusahau mambo ya kukamua msituni.
    Mdau, Scandinavia

    ReplyDelete
  2. mdau wa ifunda 1997-2000 nimefurahi sana kwa kitendo cha kijasiri cha kurusha The Glorious...mimi ni mmoja wa wadau wa ifunda wa enzi hizo unga nilikua eletronics,MKWAWA,Block A1,A2(Independent Mob) kwa wadau wa ifunda umenikumbusha sana walimu wetu wa enzi hizo ambao wadau wa ifunda wanakumbuka a.k.a zao kama KISWELE,MBATA(mtaalamu wa kemia),COMANDOO,BONDIA, SHEBIDU(mtaalamu wa eletronics),KOCHA,ACTUALY(academic master)ZUNGU,TABIA(bana bana)nadhani wadau wa ifunda makumbuka hizi nondo za kufundisha... wa ifunda wanakumbuka msitu kwa mchibozzz,kufuga afro, kutengeneza cube za kupigia mchimbozzz, kutumia lamp holder kama socket ya jiko na pasi,roll call saa 12( ilikua ni noma sana kwa form one kama ukunyeshea kiunga na majina ya form one kama(nyoa, salamanda,njuka,school machine,insect)watu kama NYABASAMBA,UPUJU POWER,NYOKA MWEHU walikua kama sumu kwa form one, watalamu wa soccer kina WASAPE,DOTO wazee wa kikapu KABANGA,MIMI MWENYEWE,DAZ(sony).... wazee wa HIP HOP kina ambwene yesaya(AY),DATAZ wazee wa mchimbo BARAKA DUNGA,..... SIJUI WAKO WAPI BWANA...... WATU HAWA WOTE.... MIMI NIKO MOSHI... na sasa ni mtaalamu wa mabo ya computer na graphics design mwaweza kupata vituzz vyangu kidogo hapa www.kileleafrika.com,www.foot2afrika.net
    wawapa hiiii sana wana ifunda

    ReplyDelete
  3. Sasa wewe mdau uliyepost tangazo hili hata jina lako umesahau kwani ni wengi tulikuwepo hapo kipindi hicho.
    Nakumbuka msitu wa ndovu, enzi za kudibua jikoni. Mwalimu Mwakalendile, na namkumbuka second head master mwalimu mhapa au mwenye kama alivyokuwa anapenda kusema alipokuwa uingereza wazungu walikuwa wanamuita M- happy.
    Nakumbuka wakati nafika ifunda kulikuwepo na walimu zaidi ya 90.
    Vipi jamani mazengo bado wanaonyesha movie na disco bado linapigwa?
    Mdau miaka ya 8o na ushee

    ReplyDelete
  4. mdau wa ifunda 1997-2000 umenifurahisha sana na hizo a.k.a za walimu hasa bana bana kwa maana kama wewe ulikuwa mhalifu kidogo huyo lazima alikuwa kama kituo cha polisi kwako, vipi majina kama vile shemeji na unaleta matani mnayakumbuka. kwa ujumla ni vizuri kuona watu wanakumbuka walikotoka. mdau wa 1995-1998 unamkumbuka pepe na mob yake? haya wadau wa ifunda glorious tuendeleze libeneke.
    Mdau wa ifunda 1993-1996.

    ReplyDelete
  5. da mkuu umenikumbusha mbali sana 1997-2000 kama denti la ifunda der camp pia 1999-2000 kama chair seuta,da manzoni 1997 ilikuwa tait form one is a school worker si ndio moto wa masingo( form one) kuna lijamaa la kutokea musoma huko li konko walikuwa wanaliita da jamaa lasha hadi limepitiliza! namkumbuka bro niliyemfagilia kwa uzungu (mpole) marehemu PAULO ANTONY KULEMBEKA pia masela wangu pabo,wasape sasa yuko italy,dereva,mbweze bro,pwaga sultani.dioniz rugai,mbinye the msongoz,ay,dataz,laddy j,sweetladdy,tinajimama na wengineo kibao,yaani hakuna camp kama la ifundiz. Kaguo,mbata,kocha ,mbungi,shebeduu na wengineo kina pertime(patiti) hongereni popote mlipo kwakutuweka sawa sasa tuko mjini.

    ReplyDelete
  6. mdau wa miaka ya 80 na ushee bado unaikumbuka mazengo, mimi nikisikia mazengo nakumbuka debe na minaziiiii lol lakini ndio maisha peter mimi favorite wangu alikua mbungi na per what per time time taken na bishoo Mabena aaah
    mdau wa miaka ya 90 na ushee

    ReplyDelete
  7. mdau wa mika 90 na ushee imenikumbusha mbali mambo ya minazii ilikuwa noma ticha akikubamba. Hivi Mbungi bado yupo?
    Hivi kuna sehemu watu walikuwa wanaenda kupata msosi tulikuwa tunakuita kwa mama mtu unaenda kupata vizibo unakuja kupata na nyuka.
    Na chama chetu cha mpira wa washangiliaje wasiochoka na bendera yetu tukiwa tunaenda tosa au njosi mambo yalikuwa mambo Ifunda ikiingia popote ilikuwa kama nyumbani
    Mdau wa miaka ya 80 na ushee

    ReplyDelete
  8. mdau 94-97 Ifunda ilikucha ile kishenzi miaka yetu hiyo rise za bongo flava ndio zilianza mida hiyo huku kuna mzee wa kidole juu (tizo mbegeta)na huku kuna jembe mzee wa east coast waacheni wakina AY watese maana zoezi walilolipata la kuwa juu kwenye competiotion ile haikuwa kazi ndogo.Nafurahi tunakutanishwa tena na wazee wa Mkwawa maana bila kuwa handsome kdg na kiingereza kingi lile bweni lilikuwa halikaliki Ifunda kulivyokuwa na baridi jamaa walikuwa wanaoga mara mbili kwa siku ili wakasimamishe minazi mazengo.Huwa nasema kuwa mtu yeyeote aliyepita the glorious hawezi kushindwa maisha. RIP wadau waliotuacha kama mzee Kasele,Paulo ...

    ReplyDelete
  9. Mdau wa 1997-2000 hapo juu umenikumbusha sana hizo namba pia umemsahau Mwl Mng`ong`o huyu jamaa alikuwa Mwl fresh sana, ndio alikuwa Mwl pekee alikuwa anaweza kuwatuliza wanafunzi kukiwa na migomo. Ebwana Huyu mshjaki Nyabasamba alikuwa ni noma. alikuwa anaondoka na kisadolini cha lita nne cha uji ha ha aha .....
    Mdau wa 1993-1996 namkumbuka sana Pepe na kampani lake la Mirambo walikuwa wanajiita Mazungu ba Chair wao jamaa mmoja alikua anaitwa Rajabu. Nakubaliana kabisa na mdau hapo juu kuwa jamaa waliosoma Ifunda hawawezi kushindwa Maisha kama tulivyokuwa tukisema. Mdau wa Moshi kama unapicha za enzi hizo unaweza kuscan na kumrushia Bro Michu atuwekee humu ndani, hasa za majengo, bila kusahau majirani zetu Ualimu. Ebwana bapo tupo pamoja wazee. Mdau Scandinavia

    ReplyDelete
  10. Yaani leo mnenikumbusha mbali sana wadau wakina nyabasamba jamaa alikuwa waziri wa chakula kweli maana msosi aliokuwa anakula si mchezo, wakina pepe na watoto wa kibaha jafari na wenzake, kasmiri mhindi huyu naye kwa kula hajambo lile sahani la kwa mama dakika mbili tu kalimaliza, mabishoo wa mirambo issa mlangila na frank ebwana wapo wapi hawa, wadau wa ifunda naomba contact zao wadau mnazo.
    shabani 1994 to 1997

    ReplyDelete
  11. sii mchezo hii inanikumbusha mbali sana.mimi nilikuwa pale 93-96 mirambo kama sijakosea.nawakumbuka sana maticha kama ptt,mabena, mbungi,kaguo,nkondokaya,olu,mwakalindile,masala na wengine wengi.hivi pepe na boni wako wapi since tumemaliza pale sijawahi kuwasikia tena.nakumbuka mchakamchaka na mbwiko za kumwaga.vilevile dora na rafiki zake nao sijawahi tena kuwasikia.ni mimi mdau wwsu.

    ReplyDelete
  12. Nasikia watoto wengi wa Ifunda wamejaa US especially H-Town wa miaka 92-97.Je vijana wa sas bado wanaendeleza umaarufu wa soccer na buku(kufaulu)au minazi mingi Sinza na Mazengo hall.We need to organize the class reunion soon wadau.

    ReplyDelete
  13. Ifunda mpoo?Je mnawafahamu wadau hawa,Myolele Ramso, Daniel Kaaya,Chriss Saul,Robert Ouko,Abby Senkoro,Ivo Mapunda,Msafiri,Chriss Ntyangiri,Pepe,Saimon Kichwa(Mkwawa),Happiness Kinyondo,Wambura,Dogo(Wa elimu),Kinyonga,Gervas Kafuku,Sylivester(Katibu),Kurwa Matimbwa(Toto tundu),Gasper Nondi,Tumaini Nkungu,Chizero Baseka,Lugabela E.Mwenye taarifa zao please nitumie kupitia ifunda123@yahoo.com

    ReplyDelete
  14. heeeee nyie wa ajabu!!yan mtu awauliza "TUFANYEJE KUINUSURU SHULE HII INAYODORORA??" nyie mwaleta ushakunaku apa,,ivi akili zimo kweli??
    somen ujumbe na mtoe maoni sio kustorisha,

    ReplyDelete
  15. mdau punguza hasira si unajua lazima tukumbuke ezi hizo swala nikukumbukana kupata mawasiliano then ndo tujue cha kufanya.Mdau hapo juu umenikubusha mbali sana mambo ya kina pabo,wasape, Doto (sasa yuko chuo cha masoka kilimanjaro ni mdau ambaye nilifanikiwa kuonana nae hivi karibuni maeneo fulani hapa moshi maarufu kwa kutengeneza mitura(bomu)...)... kwa wale wa 97-2000 watanikumbuka nilikua najulika kama RAS MEKU mimi mawasiliano yangu ni haya hapa webmaster@kileleafrika.com

    ReplyDelete
  16. aisee imenikuna sana point ya mmoja wetu nami naungana nae vitu vya muhimu kuinusuru shule yetu ifundiz der camp ni
    1.tuandae mikutano kama sio vikao ili vikutanishe wote wlosomeka pale kwa kila mikoa,kanda ,wilaya au hata vitongoji.

    2.tutengeneze vyama kila maeneo vitavyoshughulikia mambo yetu.

    3.tutengeneze maharambee japo kupata michango kidogo kwaajili ya chama na mabaki kupeleka shuleni ikasaidie patapohitajika.

    4.wachaguliwe viongozi waadilifu kipesa na si wenye tamaa kama uongozi wa black kwa rushwa! au six

    ReplyDelete
  17. aaaaaaah aaaaah du mdau hapo juu umenikuna sana kukumbuka mafisadi wa enzi hizo Mr Black na Mwenzie Giti..swala la kufanya swala lako na kuwa na chama cha wanaifunda ni zuri sana ila itakuwa vizuri ukitoa coments zako angalau basi acha ata email address yako kwani hatuwezi kuwa na harambeee,chama chetu cha wana ifunda,uongozi wa wana ifunda,kupata updates za events yoyote bila ya kuwa na mawasiliano. kwa mimi nadhani itakuwa vizuri tufungue website ya ifunda ambayo kila mwanaifunda ataweza kupata info,updates au events ambazo zimefanyika za wana The Glorious, vile vile ndani ya website hiyo kuweze piya kuwa na page moja wapo kwa ajili ya donation za The Glorious. Mimi ni mtaalamu wa kutengeneza mitandao kama
    www.kileleafrika.com,
    www.foot2afrika.com,
    www.girafficparkadventure.com
    mimi niko tayari kutengeneza website bure kwa heshima ya The Glorious... ila wadau wa The Glorious kama kuna mtu ana uwezo wakulipia domain name alipie huko alipo then anitumie jina la website yetu then naomba watu washauri nini kiwepo kwenye website ya The Glorious watume maoni yao na kama kuna mtu kwenye picha ziwe za wakati anasoma au mazingira ya sasa ifunda ilivyo basi nitumie nilianzishe libeneke la the The Glorious...... ni hayo tu wadau wa The Glorious

    ReplyDelete
  18. Bwana,bwana,bwanaa,nowadays people,....people,..people bwanaa,
    Wazee mnakumbuka people?eeh, Per TT,Mr.Mangu,wale wazungu wetu kama Mr.Ballet,Mr.Walsh(hata wazungu wenzake walikuwa hawamuelewi accent yake),Mr.Wilson,Miss Mitchelle, mambo ya 92-95 hayo.
    Nakumbuka enzi zile miaka ya 92 na 93 kulikuwa hakuna bongo fleva wala redio one wala cluods, hivyo tulikuwa wadau wachache sana tunaojua rhymes za HIP HOP na muziku wa viwanja.
    Jamani mankumbuka Sinza?
    Kupiga ishengoma wakati ukimaliza kunywa nyuka.
    Mimi nilukwa mdau wa Mirambo C2 then K6 kwenye ANGLE.Baadae nikahamia Chabu kwa ajili ya mchimbo na Kasanda John, hapo alikuwa anajiita Kandy boy, na mimi nilikuwa Mr.Chief rocker, kipindi kile nilikuwa mzee wa hiphop nikiwahusudu sana Das EFX,EPMD,Naughty by Nature,Run DMC, na makundi mengine ya wagumu HardCore Nigaz, Duuuu!kweli tumetoka mbali.Ila baadae nilibadili mfumo wa maisha na kuwa mtu wa dini seriously.
    Nina network ndogo ya watu wa Ifunda.Nina contact za Lugabela,Iqualptus Malle,Peter Westerberg,Lameck Francis,Akibe,Kwame makundi,Gatete,Gerald Gilo,Mrisho Muhsini,Ngusubila Mbope,nyabasamba,peter Benson,Rapha,Richard Makande,Salum Ramadhan,Joseph Timba,ismail Mwilenga,Jey4 wa J6(alikuwa na kina Cheche na Tutu).
    Napatikana kwa godfrey737@gmail.com

    ReplyDelete
  19. aaah, wadau nilimaanisha Mr.Yates,yule mzungu aliyekuwa anfundisha Technical drawing, alikuwa haeleweki vizuri ung'eng'ge wake.Mshikaji alikuwa na jibwa lake moja hivi lilikuwa linamfuata popote anpoenda na pikipiki yake, mnamkumbukaaa?

    ReplyDelete
  20. Mzee Ismail Mwilenga hapa naongea.Napeperusha bendera ya Ifunda ndani ya Johanesburg South Africa.Ocupational:Production Manager Comapny:Filta Matix (pty) ltd. Contact:imwilenga@filtamatix.co.za or imwilenga@gmail.com Cell:+27 823 49 6754
    Mzee umenikumbusha mbali sana,japokuwa haujatupa jina lako.
    BIG UUP IFUNDA, LETS DO SOMETHING.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 09, 2010

    Isee hii mmenikubusha mbali sana Ismail Mwilenga, Ndoliki Ntapara .. Nakumbuka game sana game na Tosamaganga kwenye uwanja uliokua wa lugby zamani, Uswege na jamaa wa Tosa wakataka kunipiga baadaya ya kumuweka mfukoni Uswege aisee we acha tu game nyingine nakumbuka tumepiga Tosa nikaingia kipindi cha pili katikati nikawa na dogo Tumaini Mkungu tulikuwa tumeshapigwa 2-0 ikabidi nimzimishe Tamimu Seif jamaa alikuwa Ifunda long time akaenda tosa high school ..mdau 1991-1994 China

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 12, 2011

    nakumbuka kupata elimu forest kuna mshkaji mmoja raphael ernest sijui yupo wapi sasa ni mdau wa 1990-1993 kwani kila siku alikuwa matatani lakini cha ajabu watu walikuwa wanafaulu sana ,hawa watu walikuwa wana character za ajabu sana good perfomance lakini mahudhurio hafifu where is teacher nyakunga,mwalimu wa chemistry anayefundisha somo slow but sure simply thinking about time and space .nice to go there and take recent pics.

    ReplyDelete
  23. Siku hizi wameichakachua sana hii shule. Nilipita pale 97-2000, Seuta G2, Electronics nikabahatika kuwa wa elimu. Sitasahau presha ya kupata division one, kwa sababu ilikuwa ni kasumba kila anaekuwa wa elimu lazima aweke div one. napakosa sana banda beach bwana.

    ReplyDelete
  24. Nimebahatika kusoma shuleni hapo na niliishi Mirambo K-5,Ni wiki mbili tu tokea nichukue Cheti changu cha form 6. na nililazimisha na jamaa yangu tulie soma nae 2005-2006, na bahati mbaya zaidi jamaa yangu alikuta cheti chake kimekosewa picha so wakakituma tena baraza. Siamini kile ninachokiona kwenye picha (ofisi ya taaluma), niliingia ofisin hapo too sad walikuwa wanahifadhi vyeti kwenye Iron locker kwahivyo hakuna uwezekano hata wa cheti kimoja kubaki. We have to do something, it's real sad.
    Napatikana kwa email: amiriissa4@engineering.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...