Mtalaamu wa bongo flava Alikiba aliyekubalika na wengi na umahiri wake wa kupawagaisha watu atawakilisha vilivyo jukwaani huko Houston Texas ijumaa 10/24/08 ukimbi wa safari party hall.

wakazi wote wa Texas na kwengineko mnakaribisha mje kucheza cinderella, mac muga nakshi nakshi na vibao vibya kabisa alivyovidondosha karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. huyo dogo mtakuja mpatia kwikwi ya mwili kwa uchovu.Ijumaa H-Town alafu Jmosi Atl hiyo nomaa..teh teh

    ReplyDelete
  2. Mwaache afundishwe watu wakisema kubeba kupiga double shift ina maana gani????

    Bora ajifunze akienda home awaeleze vijana wenye kutaka kuzamia huko maisha ni nguvu zako. You work hard you play hard.

    ReplyDelete
  3. Swali ni je atarudi kweli au ndo mambo ya box?

    ReplyDelete
  4. Mweee anonymous hapo juu kama unamfahamu na ameshakuambia anataka kubeba box mshauri tena......

    Yaani akizamia huku na alivyo na kipaji chake cha kuimba nitamwona mjinga sana.

    Siku hizi ukizamia USA haina mpango kabisa. Mpaka uingie kwenye system utakoma na roho yako. Sijui ataimba wapi watu waende kumwangalia kila siku ili apate kula.

    Usidanganyike na unavyoviona sasa hivi. Unakula free na kulala free jirudie nyumbani kabla wenyeji wako hawajaanza kukuacha mwenyewe nyumbani peke yako kila siku. Utaangalia TV mpaka utachoka.Then share za bills zikianza hehe heheheheheh

    ReplyDelete
  5. na ukifika TZ wape salamu washikaji kuwa huku kuwa tunapiga sana wasijaribu kamwe hata kidogo kujilipua

    ReplyDelete
  6. dogo nimekuona kwenye shoo hiini funika bovu ila tabia ya kuchelewa ukumbini acha pia punguza mapepe

    ReplyDelete
  7. Wabongo vipi?? mbona mnatutupa? nyinyi mshatoka kimaisha mko huko STATE-UNYAMWEZINI halafu mwambia dogo tusijaribu kuja huko, nyie mbona hamrudi bongo? kwa nini? Mbona wasenegali, wanaijeria watu wa west wanapeana michongo kichizi, halafu nyie mnabana, au ndio mnataka muonekane wajanja peke yenu?? Acheni hizo. Hata kubeba box kwani si unaingiza masaa, who cares? kila mtu anataka pay check. Au hamtaki watu waje wawakute mumeolewa na vibabu vizee au mumeoa vibibi vizeee??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...