baadhi ya wachezaji wa albino magic team wakila jalamba leo uwanja wa ocean road
winga machachari wa timu hiyo akikata mbuga
beki mkali akidhibiti mashambulizi, n chini ni 'ronaldo' wa albino magic team

HABARI NJEMA KWA WANAHARAKATI WA UNYAMA DHIDI YA MAALBINO
HUKU KUKIWA NA WAHAKA JUU YA MSTAKABALI WA USALAMA WAO KUTOKANA NA VITENDO VIOVU VYA KUWATOA ROHO KWA IMANI ZA KIHIRIKINA, WADAU AMBAO NI ALBINO WAMEANZISHA RASMI TIMU YA SOKA INAYOJULIKANA KAMA 'ALBINO MAGIC TEAM' YENYE MAKAO YAKE KATIKA TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD DAR.
KWA MUJIBU WA MRATIBU WA TIMU HIYO, OSCAR HAULE, TIMU HIYO YENYE WACHEZAJI WA UMRI MBALIMBALI IMEANZA TIZI UWANJA WA OCEAN ROAD KILA SIKU JIONI, NA ENDAPO MAMBO YATAKUWA MSWANO WATACHEZA MECHI YAO YA KWANZA WIKI IJAYO NA TIMU AMBAYO ITATAJWA KARIBUNI.
PAMOJA NA KULA TIZI LA NGUVU KILA SIKU, TIMU HIYO HIVI SASA IKO KATIKA KUSAKA WAFADHILI AMBAO WATAWASAIDIA KUPATA VIFAA VYA MICHEZO PAMOJA NA MAHITAJI MUHIMU IKIWA NI PAMOJA NA MADAWA NA LISHE ILI KUJIWEKA FITI.
MDAU HAULE AMETOA WITO KWA ALBINO NCHI NZIMA KUJIUNGA PAMOJA NA KUANZISHA TIMU ZA MICHEZO MBALIMBALI IKIWA NI NJIA MOJAWAPO YA KUHAMASISHA UMMA KUWAONA KWAMBA WAO NI WANAJAMII KAMA WALIVYO WATU WENGINE.
AMETOA MWITO PIA KWA MAKAMPUNI NA WATU BINFASI KUISAIDIA ALBINO MAGIC TEAM KWA HALI NA MALI ILI HUKO MBELENI IKIWEZEKANA WAANZISHE LIGI YAO ILI KUENDELEZA LIBENEKE LA KUMALIZA DHANA POTOFU KWAMBA ALBINO HAWAWEZI KUFANYA JAMBO KATIKA JAMII NA PIA KUONDOA UNYANYAPAA WA KILA AINA UNAOWAKABILI.
MRATIBU HUYO AMESEMA WAKO TAYARI KUPOKEA MSAADA WA AINA YOYOTE ILI KUFANIKISHA AZAMA YAO YA KUJIKOMBOA WENYEWE KUTOKA KATIKA LINDI LA UNYANYASAJI NA UHARAMIA DHIDI YAO.
AMESEMA NAMBA YAO YA SIMU NI
+255 716 040 550
HAYA SHIME WADAU, NDUGU ZETU HAWA WAMEAMUA KUJIKOMBOA NA TUWASAIDIE KWA HALI NA MALI ILI NDOTO YAO ITIMIE...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wazo zuri sana

    ReplyDelete
  2. What a beutiful idea, watu inabidi waelewe kwamba albino ni watu kama wewe mwenye rangi ya kawaida. Hamna tofauti ya Ku Klux klan na hao wanaoua albinos. Ole wenu, Mungu amesema kisasi ni chake. Wasiwasi wangu ni jua na wako bila mashati. Angejitokeza mwenye uwezo awapatie nguo za michezo zenyekuwasitiri na caps sunglasses etc. Yeyote kati yetu anaweza pata mtoto albino, tusisahau, utamkimbia?

    ReplyDelete
  3. OSCA TUNASHUKURU SANA KWA HARAKATI HIZI ZA KUWASAIDIA ALBINO. NIA YAKO NI NZURI KABISA LAKINI PENGINE MIKAKATI YAKO YAWEZA ISIWE YA UFANISI SANA KWANI:

    1. NI NGUMU KUWAFANYA WANANCHI WAAMINI KUWA ALBINO NI SAWA NA WATU WENGINE KAMA WEWE MWANAHARAKATI UNAENDELEA KUUNDA TIMU YAO PEKEE. NI VEMA HIVYO TIMU IWE NA MCHANGANYIKO NA WENGINE. HATA HIVYO HAKUNA MASHINDANO MAKUBWA YA KIMATAIFA AU YA OLYMPIC YA ALBINO PEKEE AMBAYO TUNGESEMA KUWA TUWAANDAE KWA HAYO MASHINDANO. TUNAYO MASHINDANO YA WALEMAVU HIVYO WACHANGANYIKANE NA WENGINE PIA.

    2. MAPUUZI WAMEFANYA MAUAJI YA HAWA NDUGU ZETU KWA MITIZAMO YA KISHIRIKINA, SIONI KAMA INALETA PICHA YEYOTE YA MAANA KUITA HII TIMU 'ALBINO MAGIC TEAM' MAANA HAO WAVIVU WA KUFIKIRI WANAWEZA KUSEMA KUMBE KWELI HAWA JAMAA NI 'WANADAMU- MAGIC' WANAOWEZA KUFANYA 'MAGIC' SIO TU KATIKA MICHEZO BALI HATA KATIKA BIASHARA ZAO CHAFU. LITAFUTWE TU JINA ZURI AMBALO HALINYAYEPAI WALA HALILETI UTATA WOWOTE KATIKA TAFSIRI.

    ReplyDelete
  4. yeah yeah yeah,whatever nakubaliana nanyi wote kwamba ni wazo zuri ila nisichokuelewa wewe michuzi,sasa why did you put 'breaking nyuz' kwani kuna uajabu gani wa albino kuanza kucheza mpira.they are human beings like us. you make it sound so unreal!

    keshia

    ReplyDelete
  5. bless their hearts.

    ReplyDelete
  6. HILI WAZO NI ZURI LAKINI SERIKALI ITABIDI IWEKE ULINZI MKALI KUPEKUWA WOTE WATAKAOFIKA KUANGALIA MAZOEZI AU MECHI ZAO ILI HAO WATU WABAYA WASIJE WAKAINGIA NA VIJIPANGA VYAO NA KUWANYOFOA.

    ReplyDelete
  7. These are Good News!What a Blessing?Itapunguza sana Stigmatization.Give them more opportunities,public opinion will change!Wapewe elimu sana kuhusu Afya ya Miili yao,inahitaji extra care!Otherwise welcome aboard you all and praise the Lord!

    ReplyDelete
  8. Good Idea.Nakubaliana na comments za IMPOKOCHOLE na anayejiita Keshia.Bwana Oscar jitahidi kuwachanganya na watu wa kawaida kidogo,ukiwaundia timu yao naona kama bado unakuwa unawatenga na jamii vile.

    Nageukia kwako michuzi:Ukisema hiyo habari ni breaking news kidogo inaleta kaubaguzi ka mbali sana kama alivyosema huyo Keshia.Ngoja tuangalie jinsi ya kusaidia.Tatizo la nchi yetu sasa..Suala la albinos linaweza kugeuka kuwa...from history

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...