kundi la kidedea la muchacho likishangilia simba. furaha hii haipo tena kwa muda huu kwani kwa saa bundi amelia tena msimbazi na redio mbao zinadatisha kwamba safari hii kocha mserbia anawekwa kando na badala yake supa coach syllesaid mziray na abdallah king kibaden mputa wanachukua hatamu za benchi la ufundi kufuatia kuboronga kwa timu hiyo katika ligi kuu ya vodacom ambapo majuzi ilicahpwa 4-1 na toto afrika huko mwanza. tutaendelea kupashana..
kundi la kidedea la muchacho likishangilia simba. furaha hii haipo tena kwa muda huu kwani kwa saa bundi amelia tena msimbazi na redio mbao zinadatisha kwamba safari hii kocha mserbia anawekwa kando na badala yake supa coach syllesaid mziray na abdallah king kibaden mputa wanachukua hatamu za benchi la ufundi kufuatia kuboronga kwa timu hiyo katika ligi kuu ya vodacom ambapo majuzi ilicahpwa 4-1 na toto afrika huko mwanza. tutaendelea kupashana..

Simba=Tottenham Hotspurs.
ReplyDeleteNi kweli SIMBA ni wachovu kiasi hicho au wachezaji wamenunuliwa ili timu ifanye vibaya.
ReplyDeleteTutaona kama hawajaifunga YANGA
Nilikuwepo pale uwanja wa CCK Kirumba Mwanza siku Simba ilipobugizwa magoli manne kwa moja na vijana makinda kabisa wa Toto ya Mwanza.Timu ya sasa ya Simba ni Mbovu lazima niseme bila kuficha.Bado kuna matatizo kibao ya kiufundi katika Timu ile ambayo Kocha huyo Mserbia hawezi kuhusishwa nayo kwasababu alipoajiriwa kaikuta Timu imeshasajiliwa na wachezaji wapo tayari wawe wazuri au wabovu.Kuondolewa kwa Jamhuri kama kocha msaidizi nako naona kumechangia kabisa katika kuua morale ya wachezaji.Ili Simba iwe na nguvu ya ushindi lazima pawepo na vikosi viwili vya timu ya kwanza ya simba ili kusudi kila nafasi katika timu iwe inashindaniwa na wachezaji angalau watatu!Lazima pawepo na makocha wa ziada wa vitengo mbalimbali na siyo kutimua waliopo hata kama hawahusiki na ubovu wa usajili wa timu.Kocha Mkuu kama ni mgeni au wa kwetu wenyewe ili aweze kufanya kazi ya ukocha kikamilifu zaidi lazima kwanza ashirikishwe katika zoezi la kutafuta wachezaji wenye vipaji,potentials!Ashirikishwe katika kusajili wachezaji wa msimu ndipo akabidhiwe timu aifundishe akisaidiwa na makocha wasaidizi mbalimbali.Mapato ya Klabu lazima kwanza yanufaishe wachezaji wenyewe pili uwekezaji katika maendeleo ya klabu tatu ndiyo yaje maslahi ya viongozi wa klabu na siyo kinyume chake.Matawi ya Simba lazima yajishughulishe kikamilifu katika kufuatilia mienendo ya wachezaji wa Simba pamoja na ufanisi wa viongozi wa klabu.Likitokea dosari lolote shurti suala hilo lifikishwe panapohusika katika Klabu ili liweze kutatuliwa mara moja hata ikibidi Kiongozi wa Klabu kuachia ngazi.Kwa sasa kinachoweza kufanyika ni kuchuja wachezaji waliopo kwa kuwapima stamina zao na soccer skillz pamoja na uzalendo kwa Klabu na kuwaficha kabisa mafichoni ili wapewe nyenzo zote za kukabiliana na mtani wao Yanga!Baada ya mechi hiyo ya Yanga Klabu iitishe mkutano wa klabu ili kupata mapendekezo ya wanachama kuhusu nini kifanyike na kulinda mustakabali wa klabu hapo baadaye.Asisingiziwe Refa wala Manji katika kuboronga kwa Simba Mwanza.Hii timu haifai mbovu lazima isukwe upya!
ReplyDeleteBlog hii ni kwaajili ya kuelimisha,kufundisha,na kufurahisha jamii ila ina makosa kadhaa ya uwasilishwaji wa habari zinakuwa na kasoro nyingi.Nafikiri ni kwa sababu haina watu makini wanao fuatilia na kuhariri habari kwa umakini kama mimi.
ReplyDelete"fafanua kocha mserbia wa simba anayewekwa kando ni yupi.nadhani umemipatata
Bingwa wa kuhariri habari kwa umakini, "UMEMIPATATA"?
ReplyDeleteungehariri habari zako kwanza halafu ukosoe wengine! "UMEMIPATATA"?!
TVZ Kcartoon asante sana kumwambia bingwa wa kuhariri, hapa hakuna cha kuhariri tunachotaka ni concept kama imefika. Tunajua kocha siyo Mserbia lakini anachoongelea ni kocha.
ReplyDeleteKweli watani zangu mmekwisha jumapili? ijayo. Tumawatuma Toto kwanza wafagie sisi tumalizie. Poleni
Tatizo la Simba sio uwezo bali ni siasa za mpira wa Bongo ambazo ni tamaa za baadhi ya mashabiki na viongozi. Kundi linalojiita "Friends of Simba" ni bora wangeitwa "Enemies of Simba" maana ndio wanaoimaliza Simba. Wameapa kwamba wasipopewa mgawo wa ufadhili wa TBL, basi ushindi kwa Simba utakuwa ni ndoto.
ReplyDeleteWamewanunua wachezaji wanawapa kila wanachotaka, hata kama Simba itaendelea kufungwa milele wachezaji wao wamehakikishiwa kulipwa pesa zao bila shida. Pili, ni uongozi mbovu kuanzia kwa Mwenyekiti hadi katibu wake hamna kitu na wala hawajui kilichowaleta Msimbazi, zaidi ya njaa zao. Simba pamekuwa mahali pa kumalizia shida zao za nyumbani. Badala ya viongozi kukaa chini na kupanga mikakati ya kisayansi kuiboresha timu, viongozi wenye akili timamu wanakaa kwa kauli moja wanapitisha hoja kwamba kwa kuwa timu inafungwa, basi ni bora wasome dua/kisomo cha Hal-badri na Maulid, ili timu iondokane na kipigo. Basi kama ni hivyo timu za Uarabuni zingekuwa mabingwa wa dunia, kama uhodari wa kusoma dua unasaidia kuleta ushindi. Yanahitajika mapinduzi makubwa kwenye klabu zetu. Na hata Yanga wasiifurahie hali hii , maana kawaida upepo ukiisha Simba unahamia Yanga, kwasababu chanzo cha matatizo ni kile kile. Unategemea nini kama sababu kuu zinazowafanya viongozi waombe na waingie madarakani ni kujiongozea kipato wao binafsi, kwa kukomba fedha za ufadhili na kuwadhulumu wachezaji na kujipatia umaarufu. Hata ukija TFF pia ni hivyo hivyo, hawana jipya kila kukicha badala ya kufikiri namna na kubuni mbinu za kuendeleza soka Bongo, watu wanafikiria namna gani watakula. Ufisadi hauko serikalini tu, bali uko kila mahali, we' chunguza utagundua. Klabuni ni kula, TFF taifa ni kula, TFF wilaya ni kula, yaani ni kula, kula, kula kwa kwenda mbele. Mungu Ibariki Tanzania.
Mkereketwa wa Mpira - Bongo
Acha Kibadeni na Mziray, hata angeletwa Skolari hapo, bado mambo sio mazuri, nakumbuka katika kuchangia kwangu moja ya habari za Simba katika blog hii hili la kufanya vibaya Simba nilishatabiri.
ReplyDeleteTatizo sio wachezaji, ulaji!!! ulaji mwanangu. Nilibashiri kwa kusema huyo Julio kuwepo hapo na kocha wa kigeni hata tungeomba kwa mungu na kudhikiri uchi kutwa mzima bado mambo yatakwenda ndivyo sivyo, na hao wanaoletwa kumbuka walikuwa pembeni tu siku zote wanaangalia jinsi gani ya kulamba ulaji.Narudia tena leo, kama kocha Maximo asingeletwa na mzee mwenyewe mbona tulikuwa tushamsahau nchini. makocha wazalendo, majungu baba, mwanangu usiambiwe ataletewa kocha mizengwee mpaka aonekane hajui kitu. Kwa kweli mpira wa bongo ushantia kichefchefu.
Q
Hivi simba hawa ndio wale waliokuwa wakisema wanaweza kucheza mechi mbili kwa wakati mmoja kwa kuwa wana vikosi viwili kabambe ? ( Seydou ndo alitoa kauli hiyo wakati wanacheza mechi za maandalizi )
ReplyDeleteTatizo kubwa la simba ni kuiangalia mechi ya yanga tu wanasahau kwamba kila timu kwenye ligi ina uwezo na nafasi sawa , jikomboeni kwenye mawazo ya kuifunga yanga tu badala yake muweke mikakati ya kuchukua ubingwa vinginevyo mwaka huu mutafukuzana sana . mimi sioni kama kuna hujuma yoyote simba ila tu ni wakati na kwamba ngoma ikivuma saana mwisho wake hupasuka ,
Mnazunguka tu wadau.... ishu ni kuwa ile Albadiri inawatafuna Simbwa !
ReplyDeleteAnon wa Tarehe October 20, 2008 10:50 PM. unasema mpira wa bongo ushakutia kichefchefu, usije tena hapa janvini usije ukatutapikia.
ReplyDeleteMimi nauliza wadau, hivi timu ya simba ni ya waislamu? mbona maalbadili yanazungumzwa? udini hadi mpirani du!!hii noma