Kwa heshima kubwa na Taadhima wana Familia ya Nzaro waliopo Detroit Michigan wakiongozwa na Da Mboja Nzaro na Mwamvita Nzaro pamoja na rafiki wa kike wa Marehemu Saada Ali, wanapenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa niaba ya familia nzima ya Nzaro iliyoko nyumbani Tanzania pamoja na jamaa na ndugu wote kwa mwitikio mkubwa kutoka sehemu mbalimbali wa rambirambi, maneno ya faraja na misaada ya hali na mali iliyotolewa mpaka sasa.
Tunashukuru vyombo mbalimbali vya habari na hasa mitandao mbalimbali ya kiintaneti ya Watanzania ambayo imefungua kurasa zao na kubeba habari hizi za msiba ambao kwa familia yeyote ile ni mzigo wa majonzi usiobebeka. Kwa wanaokumbuka ni wiki moja tu familia yetu imetoka kumzika Baba mkubwa mzee Hamisi Mfinanga (baba yake na kina Ayubu Mfinanga) ndani ya wiki moja tunampoteza kaka yetu. Tumegubikwa na wingu la huzuni.
Michango na misaada yenu imewezesha kwa kiasi kikubwa kufanikisha shughuli za awali za kuundaa mwili kwa heshima za mwisho na hatimaye kwa safari ya nyumbani. Lengo letu la michango ili kuweza kumsafirisha Marehemu Ndali pamoja na mwanawe lilikuwa ni kufikia kiasi cha dola 16000. Hadi sasa tumefikia karibu asilimia 75 ya lengo hilo kutokana na ukarimu wenu, ukarimu ambao hatuwezi kamwe kuusahau na kwa hakika ni faraja ya wazazi nyumbani na bila ya shaka maneno peke yake hayawezi kutosha kuelezea shukrani yetu.
Tumekusudia kumsafirisha marehemu Ndalima Nzaro siku ya Jumanne na tunawaomba wale ambao wamekusudia kutusaidia kiasi chochote kile kuweza kufanya hivyo hasa leo ili tufikie lengo hilo.
Mwisho wa shughuli yote hii tutawapa taarifa ya michango yote na mchakato wa matumizi yake kwa ujumla. Tafadhali tuma mchango wowote kwa kutumia akaunti hii maalum:
Bank Of America: (Mwishoni mwa juma iliyokuwa Benki ya Lasalle imemaliza kuungana na BoA)
A/C Name: Philemon Mnzava/Mboja Nzaro
Routing No. 072000805
A/C No. 5407722411
Bank Location: Michigan
Swift Code: BOFAUS3N
Swift Code: BOFAUS3N
Tukiwa wenye mioyo ya shukrani, na macho yaliyolowa machozi tunatoa shukrani zetu za dhati kwa mwitikio wenu kwa saa hii ya majonzi ya familia yetu. Kama tunachakumwomba Mungu, ni awabariki na kuwalinda ninyi na familia zenu na aukumbuke wema wenu kwetu ili siku moja awalipe mara nyingi zaidi. Kwa habari za mazishi nyumbani Tanzania tutawapa taarifa ndani ya siku hizi mbili.
Katika msiba, Detroit;
Mboja Nzaro,
Mwamvita Nzaro,
Mohd Nzaro,
Saada Ali
Kwa niaba ya Familia ya Nzaro.
Kwa niaba ya Familia ya Nzaro.


Naomba msaada wa kujua Marehemu kwao hapa Daresalaama ni wapi? ningependa kwenda msibani.Nilikua nafahamu walipo ishi Oysterbay ila nadhani wamehama , naomba msaada wadau.
ReplyDeleteYani waBongo hamna msaada kabisa, nawauliza nyumbani kwa wazee wa marehemu hapa Bongo ndio hata jibu hakuna mmh. haya!
ReplyDelete