Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mh. Sophia Simba (katikati) na Mkurugenzi wa Mfuko wa Saratani ya Matiti, Angela Kuzilwa (shoto) wakicheza ngoma na mnenguaji wa kikundi cha Ten Best cha Amana, wakati wa maandamano kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya waliothirika na saratani ya matiti Tanzania, Dar es Salaam jana. Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania ilikuwa miongoni mwa wadhamini wakuu wa maandamano hayo yaliyoanzia Mnazi Mmoja hadi hospitali ya Ocean Road.


hivyo hizo michango zinatumikaje kusaidia hizo saratani?
ReplyDeletekwa sababu canser za matiti zinatibika haswa zikiwa ktk low stage.
je kuna mpango wowote wa kuchunguzwa kına mama kwa ajili ya early dıagnosıs au inalenga tu ktk matibabu?
naomba ufafanuzi kwa anayejua