Kwa masikitiko makubwa Familia ya Mohamed Nzaro na Balozi Eva Nzaro inatangaza kifo cha mtoto wao Ndalima Yusuph Nzaro kilichotokea jana Alhamisi Katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Michigan mjini Ann Arbor ambapo alikuwa amekimbizwa kutibiwa baada ya ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia Jumanne ya Oktoba 14, 2008.
Gari alilokuwa akiendesha marehemu liligongwa na gari nyingine wakati likisubiri taa za kuongozea magari.
TAARIFA ZA AJALI HIYO IPO HAPA http://www.clickondetroit.com/news/17709594/detail.html?taf=det
Mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu nyumbani Tanzania kwa mazishi inaendelea. Vile vile, utoaji wa heshima za mwisho mjini Detroit unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 18 Oktoba, 2008. Muda rasmi utatangazwa baada ya maandalizi kukamilika.
Familia inapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru na kuwaomba msaada wenu wa hali na mali katika kufanikisha safari hii ya mwisho ya kijana wao mpendwa Ndalima.
Michango kwa ajili ya msiba huu inaweza kupelekwa moja kwa moja kwenya akaunti maalum ifuatayo:
Bank Of America:
A/C Name: Mboja Nzaro (Dada wa Marehemu)
Routing No. 072000805
A/C No. 5407722411
Mawasiliano zaidi Kuhusu habari za msiba huu wasiliana na wafuatao:
Anna Royal Mfinanga 248-778- 6395
Abdul Kufakunoga 248-515- 5509
Salum Ndolanga 248-796-1267
Philemon Mnzava 248-417-5015
Leo The Saint 614-426-3422
Anna Royal Mfinanga 248-778- 6395
Abdul Kufakunoga 248-515- 5509
Salum Ndolanga 248-796-1267
Philemon Mnzava 248-417-5015
Leo The Saint 614-426-3422
Msiba huu kwa Detroit unafanyika nyumbani kwa binamu yake Ayubu Mfinanga.
Anuani ya Kwa Ayub:
Anuani ya Kwa Ayub:
22255 Hessel Detroit,
MI 48219
Tutaendelea kuwahabarisha kwa kadiri mipango inavyoendelea.
Asanteni kwa sala zenu, ushirikiano wenu na misaada yenu.
FAMILIA YA NZARO
Asanteni kwa sala zenu, ushirikiano wenu na misaada yenu.
FAMILIA YA NZARO
--------------------------------------------------
KWA NIABA YA WADAU WOTE GLOBU HII YA JAMII INATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU KWA MSIBA HUU MZITO AMBAO UMEGUSA HISIA ZETU SOTE NA KUTUTIA SIMANZI ISIVYOELEZEKA.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI NDUGU YETU NDALIMA
AMIN



NATOA POLE NA SALA ZANGU MUNGU AWAFARIJI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU CHA MOJONZI FAMILIA YA MOHAMED NZARO PAMOJA NA NDG, JAMAA NA MARAFIKI,
ReplyDeleteMdau
Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Ndalima.Poleni sana wafiwa.
ReplyDeleteRIP Yusuf.
ReplyDeleteNdali you will always be remembered go in peace brother and rest in peace. To your son,parents,Da Mboja,Iddi,Mwamvita may almighty god give you strength and courage.
ReplyDeleteNAMI NAUNGANA NA MTOA MAONI WA KWANZA KUWAKILISHA POLE ZANGU KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA MSIBA MKUBWA AMBAO KWA KWELI UMENIGUSA MIMI BINAFSI.JANA NILIPOSOMA AJALI HII NILIJIFUNZA KWAMBA KILA KUNAPOKUCHA NI MUUJIZA MKUBWA SANA MUNGU ANAOTUFANYIA KATIKA MAISHA YETU. HIVYO TUNAPASWA KUMUOMBA MUNGU NA KUSAMEHE WALIOTUKOSEA KILA SIKU KABLA YA KUANZA SAFARI NA TUNAPOMALIZA SIKU NA KWENDA KULALA. JAMBO LOLOTE LINAWEZA KUTOKEA.KIJANA HUYU MAREHEMU, HANA KOSA BARABARANI LAKINI IMESABABISHWA NA MTOTO MTOVU WA NIDHAMU BARABARANI. MUNGU AWATIE NGUVU NDUGU WA MAREHEMU HUKO MAREKANI, NASI TUNAWAOMBEA MASAFIRI SALAMA KURUDI BONGO KWA MAZISHI.
ReplyDeleteANNA
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi, pole sana idd nzaro, mboja pamoja na baba na mama, tunawasubiri huku Tanzania tushirikiane msibani. Ni ngumu sana kwa wakati huu lakini tunamuomba mwenyezi mungu awape subira na imani pole sana
ReplyDeletehellen - Rafiki yake marehemu swaumu
kwani nini? huko michigani ndiyo kunakuwa na habari hizi za kutisha kila siku. mola amlaze mahali pema peponi.
ReplyDeleteGod Rest is Soul in Peace. This is tragic..Mwenyenzi Mungu awajaze nguvu familia ya marehemu.
ReplyDeletePoleni wafiwa. Poleni watanzania wa Detroit. RIP our beloved young man. Grandma
ReplyDeleteInna Lilaahi wa Inna ilaihi raaji'una.
ReplyDeleteTunakuomba mwenyezi mungu umsamehe marehemu dhambi zake, umuepushe na adhabu ya kaburi, umuepushe na adhabu ya siku ya kiama, umpe kauli thabit siku ya mwisho na umpe malaika wema wamlinde mpaka siku ya kiyama.
Mwenyezi mungu tunakuomba uwajaze subira wafiwa haswa wazazi wake wawili, ndugu zake, jamaa na marafiki. Amin
RIP Yusuf, loh! Such handsome kaka. Poleni wafiwa
ReplyDeleteMungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. AMIN
ReplyDeleteJAMANI POLENI SANA SANA,NILISOMA JANA NIKASIKITIKA ROHONI NIKASEMA PENGINE HAJAUMIA SANA ATAPONA,MUNGU NDIYO MWEZA WA YOTE AWAPE FARAJA NDG NA MARAFIKI NA AIPOKEE ROHO YA MAREHEMU PAHALI PEMA PEPONI,SIKU YA SIKU NASI TUTAMUONA KWA KUWA NDIYO MAKAO YETU YA MILELE.
ReplyDeleteR.I.P Ndalima!
ReplyDeleteNatoa pole kwa wafiwa na kumuombea marehemu alazwe pema peponi. Naomba kuuliza tu kuhusu utumiaji wa neno "hayati" kwa sababu mimi nafikiri neno hili lina maanisha alotutoka lakini yuko hai nyoyoni mwetu - kwa kifupi "martyr". Sijui kama ni sahihi kulitumia kama mbadala wa neno "marehemu".
ReplyDeleteINNALILLAHI WAINNA ILAIHIRAJUUN!
ReplyDelete'hakika sisi sote ni wa M/Mungu na kwake tutarejea'
M/Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amiin!
Kwakweli sisi binadamu tuna kila sababu ya kumuomba na kumshukuru Mungu kwa kila siku anayotupa, kwani hatujui siku wala saa ya kutwaliwa. Kaka wa watu alikuwa na safari zake tu jamani, wala hakujua lililopo mbele yake.
ReplyDeleteHatuna jinsi sisi wengine tuliobaki... ni kumuomba Mungu tu na kujiweka tayari kwa saa ya kutwaliwa.
ULALE MAHALI PEMA KAKA YUSUPH JAMANI.. Ndugu, jamaa, marafiki na wazazi wa marehemu...tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi ya kuondokewa na kaka yetu mpendwa.
....BWANA ALITOA...NA BWANA AMETWAA.. JINA LAKE LIBARIKIWE... AMEN...
Poleni sana ndugu za marehemu.Ndalima nilisoma naye Oysterbay primary school ,alikua classmate wangu na pia nilikutana naye Dretoit MI, ni rafiki yangu ,kwa kweli kweli nita mmiss sana .
ReplyDeleteKitu kimenishangaza ni kwamba, juzi nilikutana na rafiki yangu mmoja ambaye sijakutana naye toka tumemaliza primary school hapo Oyterbay mwaka 1987. Akawa excited kuniona kasema "Miaka mingi tume poteana leo tunakutana na tuko hai wakati kuna magongwa na ajali nyingi ,wenzetu wengi wamefariki , Mungu mkubwa" sikujali kabisa usemi huo na cha ajabu tuka mzungumzia Ndalima, yeye akasema alikutana naye , mimi nikamwambia mara ya mwisho nimekutana na Ndalima 2003 kwenye harusi huko Michigan, baadaye usiku ndio napata taarifa ya ajali.
R.I.P Ndalima
kusema kweli imenistua hii habari!!
ReplyDeletejana nimesoma hii habari nanikajuwa atapona tu!!. kumbe ilikuwa ndiyo safari yake jamani!!
TUSEME NINI BABA,HATUNA LA KUSEMA BALI TUNASHUKURU KWANI NI WEWE ULIYETOA NA NI WEWE UMEMCHUKUWA.
tulimpenda ndalima ila wewe umempenda zaidi!!
kusema kweli ni njia ya wote mbele yetu nyuma yako
habari imenistua ila nakutakia mapumziko mema!!
POLENI WAFIWA, NDUGU NA JAMAA WOOTE WA NDALIMA.. TUMUOMBEE APUMZIKE MAHALI PEMA..
ReplyDeletesiamini jaman dear cousin ndio umeniacha hivyo, ama kweli duniani tunapita mungu awape faraja note ndugu wa marehem Mboja, Iddy, Mwamvita ,Eddy pamoja na Moddy. tuko pamoja nanyi.
ReplyDeletecousin
Mungu amlaze Ndali mahali pema peponi. It was a shock to me still is,it remind me of my late bro Longo. Da Mboja, Mwamvita,Iddi, Mama na Baba poleni sana, I know the feeling.
ReplyDeleteNawapa pole ndugu,jamaa na marafiki wote kwa kuondokewa na Yusuph.
ReplyDeleteSisi wote tu wasafari na mwenzetu katutangulia nasi tutafuata.
Rest in Peace brother.Amen
Si wezi kuamini kabisa!!. Lakini cha muhimu nikujua kwamba sisi ni wa safiri hapa duniani. Poleni sana Baba,Mama, Dada Mboja, Iddi, Mwamvita, Eddy na Moddy. Mwenyezi mungu awape nguvu na awa fariji.
ReplyDeleteNdalima you will be greatly missed and thanks for being a great friend and brother.
RIP
Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi. Lakini zaidi alete faraja na nguvu kwa familia ya marehemu.
ReplyDeleteUkishapata matatizo una-appreciate sana maisha na kuona kwamba siku zetu zinahesabika. Kwasisi tuliobaki basi tuzidi kupendana na kudumisha yale aliyopigania marehemu.
Mdau
Texas
RIP Ndalima.
ReplyDeletePoleni sana Da Mboja, Iddi, Mwamvita, Ayubu, Baba na Mama.
Mpo kwenye sala zetu, na tupo pamoja kwenye msiba huu.
Kwa wakuu mliokua huko kuna mwenye simu ya Iddi, Ayubu au Da mboja?
Tunaomba mtuwekee pamoja na hizo mlizoweka.
This is a wake up call to us left behind. Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi. My dear people.. Pause and ask yourself, if this happens to you today, ARE YOU READY? Have you forgiven those who wronged you? Have you ask God to forgive your sins? Rest In Peace brother Yusuf Ndalima. Mwenyezi Mungu akulinde na adhabu ya Kaburi. Upumzike kwa amani katika usingizi wa milele.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa wote. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
RIP Ndalima. Poleni sana wafiwa.
ReplyDeleteR.I.P Ndali. Inna Lillahi Wainna Ilaihi Raajiun.
ReplyDeleteYou'll always be missed.
Pole sana Familia ya Mzee na Mama Nzaro. na ndugu zake Ndalima. Nina furaha moyoni kwamba nilipata kumfahamu Marehemu Ndalima na alikuwa kaka mtaratibu mno mwenye amani. Natumaini ameenda na amani na upendo kama alivyoishi hapa duniani. Wote tunaenda huko huko katika muda na nyakati tofauti. Tuwe tayari. tubebe misalaba yetu, tumshukuru Mwenyezi Mungu kila wakati kwa kutujalia familia zenye upendo, tuombe kuepushwa na majanga ya dunia. maana hatujui saa wala dakika na wala siku atakayokuja Mwana wa aliye juu!!!
ReplyDeleteR.I.P NDALIMA
You are very right Anon 17,2008 4:09. This is WAKE UP CALL! Are we ready for this. Sababu tuko barabarani kila siku. Tumshukuru Mungu kwa kila siku anayotupa hapa duniani. Tumrudie Mungu, tumwabudu katika roho na kweli. Bwana YESU asifiwe sana!
ReplyDeleteinalilah waina ilayhi rajiun.. mwenyezi mungu ailaze roho ya maehemu pahala pema peponi.. AMIN
ReplyDeletePOLENI SANA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI KWA MSIBA HUU....
HUYO MTOTO ALIESABABISHA AJALI DAWA YAKE NI KUTIWA NDANI YEYE NA HUYO MAMA YAKE MAANA NDIO ALIEMFUNDISHA KUWASHA GARI NA NA KUTIA GEA....MAANA WAPO WATU WAKUBWA HUMU HAWAJUI HATA KUZUNGUSHA USUKANI HUYO KAFUNDISHWA NA MAMA YAKE TU KWA SABABU WAO HUA HAWAJALI NAFSI ZAO...
ReplyDeletepoleni sana !!
ReplyDeletehuyu kijana simjui ila nilisoma habari za ajali jana ,leo nimefika na kukuta ameshakufa roho imeniuma mno
kweli tunapita
rest in peace my dear brother!
Hivi wazazi wengine mboma wako so irresponsible hivi. Kwanza hako katoto kametoa wapi funguo? Na nani aliyemuonyesha kuwasha gari. Soon tutasiki mara hawezi kushitakiwa kwa kuwa alikuwa na upungufu wa akili (Sijui wanasema autism) na vile alikufa ni mwafrika I tell yuo wote subirini nini watakachokifanya kwa huyo muuaji!!!! Haki lazima itendeke, najua hatuwezi kumrudisha kaka yetu duniani lakini haka katoto kanapaswa kufundishwa adabu ili iwe fundisho kwa wengine. Poleni wafiwa kusema kweli nina hasira sana, nikimwangalia mwanangu wa miaka 13 na mtu aje amchukue kipuuziu naman hii, this is not fare. Simjui personally, but it pains to see people dying innocently, Inshallah tunawaombea wazazi wetu waliopoteza kijana huyo Mwenyezi mungu awape tahfif na uvumilivu. ITS NOT EASY TO LOOSE A CHILD, DUUUH. POLENI.
ReplyDeleteThe family of Nzaro and friends.I was deeply saddened to hear of your loss. My thoughts are with you.
ReplyDeleteRest in peace Yusuf.You were the best friend that a person has ever asked for.Although we loved you dearly, we could not make you stay. A golden heart stopped beating, hardworking hands at rest. God broke our hearts to prove to us, He only takes the best.
Mungu ailaze Roho yako mahali pema peponi.
Kohai -Japan
My Condolences
ReplyDeleteINNALILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN
ReplyDeletePoleni sana wafiwa M/MUNGU amjaalie marehemu amlaze mahala pema peponi na awape subira wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu.
Surely life is too short!!! What a shock to all friends and family of the deceased? Rest in Peace brother, and stay strong all who knew and loved him dearly.
ReplyDeletePole sana mzee wangu mohamed nzaro,mama eva,iddi,mboja na mwawita.mungu amuweke peponi mdogo wangu ndali.posted by iqbal visram and family bukoba tanzania
ReplyDeletepoleni jamani.Its so sad. RIP.
ReplyDeleteJamani kaka wa watu...RIP
ReplyDeleteNilisoma hii habari jana asubuhi nikajua atapona tu.
Cha kushangaza ni kuwa usiku wakati naangalia news ikatokea habari ya mwizi mwingine wa gari kagonga watu na wamefariki wawili. Kilichonifanya nikuumbuke hii habari yake ni kuwa ni kama copycat ya hiyo ya huyu kaka. Gari lilikuwa linakimbizwa na police ni benzi na lililogongwa ni Honda na wao walikua wanasubiri green light hivi hivi.
I wonder kwanini bado wanachase hawa waizi wa magari hivi kila siku? Hilo gari linaworth kweli uhai wa mtu???
Another young life taken away b'se of car accident. This is definitely a life taken too early and so senselessly! But why do police continue to chase these stupid thieves?
ReplyDeleteMy heart and prayers go out to his family and friends.
RIP you will be missed
Poleni sana kwa msiba huu mzito wa mdogo wetu Ndalima. Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na hizi habari. Ni miaka mingi imepita tangu nimuone Ndalima lakini namkumbuka vizuri akiwa mtaratibu kama watu wanavyomuelezea.
ReplyDeleteMwamvita rafiki yangu, Da Mboja, Iddy, Eddy, baba, mama, mtoto wa Ndali, na ndugu wote tunawaombea mungu awape nguvu ya kuendelea. Mungu muweke mahali pema peponi Ndali. Milembe
RIP Ndalima, sikujui ila nimeumia sana baada ya kusoma taarifa hapa kwa michuzi juzi ulipata ajali the same day na mimi nilipata ajali lakini nikajisemea moyoni Mungu atusaidie,leo nimepata mshtuko sana baada ya kuona umeaga dunia.
ReplyDeleteMungu awape uvumilivu wapendwa wazazi wako Ndugu jamaa na marafiki sote tu wapitaji!
Amina kavira,umenikumbusha kuhusu Longo,kwa kweli ni msiba mkubwa ulionistua katika maisha yangu yote na still siamini kama longo amefariki.Mungu awaweke peponi my dear friend Longo Kavira na Ndalima.
ReplyDelete