Timu ya soka ya Tanzanite Fc ya Atlanta wikiendi hii imefanya mauaji ya kutisha katika ligi daraja la tatu inayoendelea hapa Georgia.
Wakiwa wageni wa HCAG UF ya Lethonia GA waliweza kuwatandika wenyeji wao hao kwa bao 3-1. Hadi wanakwenda papumziko washindi walikuwa chini kwa bao moja bila.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Tanzanite wakijalibu kila njia kusawazisha mabao hayo. Iliwachukua dk. 15 kuswazisha bao hilo lililowekwa kimyani na mshambuliaji hatari Khamza Liganga "Liga".
Alikuwa Liga huyo huyo aliyewainua vitini washabiki pale alipopachika bao la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mzindwelha Ghaninze "Muzi".
Dakika ya 35 almanusura nyota ya mchezo wa leo Hadji Helper awapatie washindi bao baada ya kuunganisha krosi safi kutoka winga ya kulia iliyopigwa na Muzi. Alikuwa ni Khamza Liganga tena aliyepachika bao safi la ushindi baada ya kupokea krosi safi ya chini iliyopigwa na winga nyota mchachari Hadji helper.
Dakika ya 35 almanusura nyota ya mchezo wa leo Hadji Helper awapatie washindi bao baada ya kuunganisha krosi safi kutoka winga ya kulia iliyopigwa na Muzi. Alikuwa ni Khamza Liganga tena aliyepachika bao safi la ushindi baada ya kupokea krosi safi ya chini iliyopigwa na winga nyota mchachari Hadji helper.
Ushindi huo ni wa pili kwa timu hiyo inayoshiriki ligi hii kwa mara ya kwanza hapa USA.
Mechi ya hii imekuwa gumzo kubwa hapa Lethonia GA baada ya solid perfomance iliyoonyeshwa na wachezaji Hadji helper, Elvis Doto Mnyamuru, Khamza Liganga, Muzi, Capt. Fredrick Mburushi, Said "Jogoo" Chambuso, Adrei Savu, Aaron, malik, Abdulshareef, Sajo na Mbelkwa Dramin.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake,
Mungu Ibariki Tanzanite Fc.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake,
Mungu Ibariki Tanzanite Fc.


jitahidini mtanyakuwa kikombe.
ReplyDelete3-1 ni mauaji ya kutisha? mnasema kama vile hijawahi kutokea au ni vigumu mno timu kushinda 3-1!!!!!!
ReplyDeleteThese brothers are serious. The brothers know what they are doing. I am so proud of them. See how energetic they look. Keep up the good work. Well done and good luck in your games.
ReplyDeletemchangiaji wa tatu tusidanganyane bwana! serious gani? na unatutaka tuangalie nini? ukiangalia picha tu unaona kam wote hawako fit kabisa, vitambi vimefunikwa na jezi na ni wanene kupita kiasi. ENERGETIC? yeah yeah yeah
ReplyDelete