Baada ya muda wa takribani miezi miwili, mwanamuziki Ally Kiba (pichani jana akiwa uwanja wa ndege wa Orlando) arejea bongo kwa mapumziko mafupi. Ally Kiba anapenda kuwashukuru washabiki wote waliojitokeza kwenye shoo zake na kwa support kubwa aliyoipata.

"Ukarimu na uzalendo nilio onyeshwa muda wote niliyokuwepo hapa Marekani ni kitu ambacho kitakuwa moyoni daima. Nawashukuru kila mmoja wenu kwa kufanikisha ziara yangu na Mungu akipenda tutaonana tena hivi karibuni" Ally Kiba alisema haya kabla ya kupanda ndege kuelekea Tanzania.

Ally Kiba amemaliza ngwe ya kwanza ya tour yake na atarudi Marekani tarehe 11/25 kumalizia ngwe ya pili ambapo siku ya alhamisi 11/27/09 atakuwepo HOUSTON TEXAS kwa shoo maalumu ya Thanksgiving kabla ya kuelekea ATLANTA GEORGIA 11/28/08 ambapo anatarajiwa kuperform kwenye club kubwa na mashuhuri ATLANTA iitwayo "Club Dreams" kwenye kilele cha sikukuu ya Thanksgiving.

11/29/08 Ally Kiba ataelekea Oakland, Ca kuwatumbuiza washabiki wake wote wa magharibi ya marekani Tarehe 12/01 siku ya Ukimwi Duniani, pia anatarijiwa kufanya show maalumu huko New Hampshire kabla hajaelekea Seattle, kwa show nyingine tarehe 12/06.

Wakazi wote wa DALLAS TEXAS na vitongoji vyake MNAOMBWA mjitokeze kwa wingi kumuaga Ally tarehe 12/13/08 ambapo atafanya show yake ya mwisho nchini MAREKANI.
ALLY KIBA ANATARAJIA KUONDOKA 12/16/08 KURUDI TANZANIA TAYARI KWA SHEREHE ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA..
Aksanteni.
Kwa maelezo zaidi tafadhali nenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mwanamuziki wa Bongo flava aliefanya ziara ndefu ali kiba kavunja rekodi hakuna wa kumfikia.Viva Kiba

    ReplyDelete
  2. KWELI KAKA UNATISHA POZI LAKO TU NIMELIPENDA,LINAENDANA NA FUN YAKO!

    ReplyDelete
  3. Hiki kijamaa kumbe kiko handsome namna hii! Safi sana

    ReplyDelete
  4. Dogo sio siri umepata exposure kubwa sana maishani mwako kamwe huta sahau. Outlook ipo bomba, mavazi nk. Uko juu.
    Hakuna alipiga tour kama wewe bongo, katika historia ya bongo flava.

    ReplyDelete
  5. mungu amlinde na mapromota feki tu,wasiwe wasimfanye tourist fedha wachimbie wao..........!big up kiba.by usinijue1

    ReplyDelete
  6. Mbona OHIO mmetusahau? Ali Kiba njoo na huku basi

    ReplyDelete
  7. Kulikoni tena mbona inasemekana kuwa Ali Kiba atakuwa ujerumani na Sweden mwezi november?

    ReplyDelete
  8. mmmm majuu kuzuri yaani miezi miwili kang'aa hivyo. je angekaa mwaka

    ReplyDelete
  9. dogo umejindaa safi sana sema mie hujanifurahisha nadhani fanya hima tuwasiliane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...